Rafiki,
Huwa mara nyingi tunasikia kauli kama hii jifunze kutokana na makosa yako, lakinini kuna kauli moja ambayo wengi wetu huwa hatujiambii kama tunavyojiambia au kuwaambia wengine wajifunze kutokana na makosa yao.
Mara nyingi tukijifunza kutokana na makosa yetu huwa haina hamasa sana katika maisha yetu,
Muda mwingine tunakata tamaa kutokana na makosa tuliyofanya hivyo tunakuwa hatutamani tena kurudia kile tulichofanya hapo awali. Hivyo basi ,
Usijifunze kutokana na makosa yako bali,
Jifunze kutokana na mafanikio yako. Hapa ndiyo ushindi ulipo, mara nyingi ukijifunza kwenye mafanikio yako huwezi kushindwa kwa sababu tayari umeshakuwa mshindi lakini ukienda tofauti na hapo ni shida. ukiwachukua watu wawili mmoja kajifunza kwenye mafanikio na mwingine kajifunza kwenye makosa yupi atakua bora sana na mwenye hamasa?
Tunaalikwa sana kujifunza kutokana na mafanikio yetu kwa sababu kwenye mafanikio yetu tuna uhakika wa kushinda zaidi kwa sababu rejea inatupa picha nzuri ya kushinda. Siku zote ushindi huwa una hamasisha ushindi ndiyo maana nakuambia rafiki pendelea sana kujifunza kwenye mafanikio yako zaidi kuliko kwenye kufeli kwako.
Kujifunza kupitia mafanikio yako ni njia ya uhakika zaidi ukilinganisha na njia ya kujifunza kwenye makosa yako.
SOMA; Akili Yako Iwaze Kitu Hiki Ili Uwe Na Mafanikio Makubwa
Kujifunza kwenye makosa huwa hayatupi sana hamasa kama tukijifunza kwenye mafanikio yetu. kujifunza kwenye mafanikio yetu yanatupa hamasa siyo tu hamasa hata yanatubariki na kutupa nguvu ya kufanya tena, kujiamini na kuwa bora zaidi.
Hatua ya kuchukua leo; Jaribu kuangalia ni mambo gani ambayo umefaulu sana katika maisha yako. vuta picha ya maisha yako ni maeneno gani una mafanikio sana na angalia mbinu unazotumia kufaulu maeneo hayo sasa uzirudishe kwenye yale maeneo ambayo unafeli sana.
Kwahiyo, kwenye kitabu cha Rework, mwandishi anatualika tujifunze kwenye mafanikio yetu na siyo kwenye makosa yetu. japo zote ni njia za kujifunza ila njia sahihi na ya uhakika zaidi ni kujifunza njia ya kujifunza kutokana mafanikio yako.
Muhimu; kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la mimi ni mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa. Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga bofya hapa au nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha ya kiswahili bonyeza hapa.
Ukawe na siku bora sana rafiki.
Rafiki na mwalimu wako,
Deogratius kessy
0717101505/0767101504
deokessy.dk@gmail.com // kessydeo@mtaalamu.net
Asante sana