Mpendwa rafiki yangu,
Mafanikio yana mambo mengi, ni mjumuisho wa mambo mengi na siyo kitu kimoja. Hivyo basi,
Usione mtu kafanikiwa ukazani ni kitu kimoja, hapana ni mkusanyiko wa mambo mengi. Kama unataka kufanya jambo lako muhimu sana ni vema ukalifanya muda wa asubuhi kabla dunia haijaamka.
Sasa katika huo muda wa asubuhi unatakiwa utawale kile unachofanya, sasa umetenga muda wako wa dhahabu halafu kuna watu wanataka tena wautumie yale masaa yako matakatifu.
Rafiki,huwezi kufanikiwa katika maisha yako kama unataka kumfurahisha kila mtu. Usipokuwa na mipaka katika maisha yako utakua unawafurahisha watu na ukiwa mtu wa kufurahisha watu na mambo yako yatachelewa.
Hakuna kazi ngumu kama kazi ya kufurahisha watu, hapa duniani huwezi kamwe kumfurahisha kila mtu bali mtu pekee ambaye unaweza kumfurahisha hapa duniani ni wewe mwenyewe.
Watu wana changamoto zao, hivyo ukiwa ni mtu wa kutaka kusikiliza kila mtu anachosema utashangaa muda wako wote unaishia hujafanya kitu chochote kile. Unatakiwa kuwa mkali na muda wako usipokuwa mkali utawaruhusu watu kutumia muda wako vile wanavyotaka wao na siyo unavyotaka wewe.
SOMA; Kabla Hujajali Watu Wengine; Mjali Kwanza Mtu Huyu
Pangilia muda wako, na usitake kumfurahisha kila mtu kwa kumpa muda wako, kuna watu wao hawana mambo ya kufanya hivyo wanatumia muda wa wenzao kuuchezea. Unatakiwa kuwa na msimamo na wala usimuonee mtu huruma kumwambia hapana.
Kuna watu wamekuwa wanaumizwa kila siku kwa sababu tu ya kusema ndiyo, wanaogopa kusema hapa ili waonekane wanajali na wanataka kuwafurahisha. Hatuwezi kufika kwa namna hiyo bali tunaweza kufanikiwa kama tutaka kujifurahisha sisi wenyewe.
Hatua ya kuchukua leo; jali mambo yako, jifurahishe wewe mwenyewe, kazi ya kumfurahisha kila mtu hapa duniani ni ngumu huiwezi.
Kwahiyo,huwezi kuwa na mafanikio makubwa kama unataka kumfurahisha kila mtu. Maisha ni mafupi kumsikiliza kila mtu anachotaka kusema. Jisikilize mwenyewe kwani mafanikio yako ni kujisikiliza kile unachotaka wewe.
Muhimu; kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la mimi ni mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa. Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga bofya hapa au nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha ya kiswahili bonyeza hapa.
Ukawe na siku bora sana rafiki.
Rafiki na mwalimu wako,
Deogratius kessy
0717101505/0767101504
deokessy.dk@gmail.com // kessydeo@mtaalamu.net
Asante sana