Mpendwa rafiki yangu,
Kwa wale wanaoishi katika majiji kitu kinachoitwa foleni imekuwa ni kitu cha kawaida sana. lakini mimi siko hapa kukushirikisha foleni ya barabarani. Muda wetu umekuwa mfupi sana na mambo ya kufanya ni mengi sana tunajikuta tunajiambia tutafanya kesho na kesho imekuwa kesho mpaka mwaka unaisha.
Mambo siyo marahisi kama unavyofikiria ila inawezekana kama ukiamua. Kama mambo yamekuwa mengi una muda mchache inabidi sasa upunguze mambo ambayo hayana umuhimu kwako na uelekeze nguvu kubwa katika yale mambo muhimu tu. Huna muda wa kufanya kila kitu ila una muda wa kufanya mambo muhimu tu.
Muda mzuri ambao hauna foleni katika maisha yako ni asubuhi na mapema. Kama siku ikianza wewe unakosa muda yaani mambo ni mengi unakua na foleni nyingi hivyo unashindwa kufanya mambo yako basi amka asubuhi na mapema. Muda wa alfajiri ni muda ambao hauna hata foleni muda ambao wengine wamelala yaani dunia inakua imelala hivyo kuna kuwa na utulivu mkubwa sana wa kufanya mambo yako.
Amka asubuhi kuanzia saa 10 alfajiri ianze siku yako, kile kitu ambacho ni muhimu kwako anza kukifanya. Anza kujitumikia wewe mwenyewe muda huo kabla dunia haijaamka umeshamaliza kufanya mambo yako yote muhimu.
SOMA; Huu Ndiyo Muda Mzuri Wa Kujipatia Ushindi Wa Uhakika
Wale ambao wanasema hawana muda wa kusoma, kufanya mazoezi, kuandika, kufanya kitu cha ziada kwa ajili ya maisha yako basi muda upo. Acha kitanda na nenda kajitumie kwanza wewe mwenyewe, ni aibu sana kukurupuka kutoka kitandani na kwenda kuwatumikia wengine kabla yaw ewe kujitumikia.
Anza siku yako mapema, ipangilie itakuwaje, andika mipango yako yote ya siku, andika ndoto zako na nenda kaifanyie kazi. Huu muda hauna foleni unatakiwa kuutumia vizuri kwa mambo muhimu na siyo kuingia kwenye mitandao ya kijamii.
Hatua ya kuchukua leo; muda ambao hauna foleni basi ni kuanzia asubuhi ya saa kumi mpaka kumi na mbili. Unaweza kufanya mambo yako yote bila usumbufu wa dunia na mara nyingi kelele za dunia huwa zinaanza kuanzia saa moja.
Hivyo basi, kama huna muda basi punguza kulala sana na amka mapema tumia muda huo kufanya yale mambo yako binafsi yanayokusaidia katika ukuaji na maendeleo yako binafsi.
Muhimu; kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la mimi ni mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa. Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga bofya hapa au nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha ya kiswahili bonyeza hapa.
Ukawe na siku bora sana rafiki.
Rafiki na mwalimu wako,
Deogratius kessy
0717101505/0767101504
deokessy.dk@gmail.com // kessydeo@mtaalamu.net
Asante sana