Design a site like this with WordPress.com
Get started

Hii Ndiyo Bidhaa Ambayo Huruhusiwi Kununua Ukienda Sokoni

Mpendwa rafiki yangu,

Natumaini kila mmoja wetu ananunua na linapokuja suala la kununua hisia zinakuwa mbele kuliko fikra. Watu wengi wanapoteza fedha nyingi katika manunuzi ambayo hayana tija.

Unapokwenda sokoni au kununua kitu chochote unatakiwa uwe makini sana la sivyo utajikuta unanunua hata vile ambavyo hukupanga na kuja kushtuka fedha imeisha.

Hivyo basi, unapoenda kufanya manunuzi hakikisha umeandika au kuorodhesha mahitaji yako yote katika karatasi na hiyo karatasi ndiyo iwe mwongozo wako kwa sababu kama huna mwongozo utajikuta unamaliza fedha katika manunuzi ambayo hata hukupangilia.

Kama kitu hakipo katika list yako wala usijisumbue kununua, hata bei iwe rahisi na muuzaji akushawishi namna gani usikubali wewe fuata mwongozo. Ukienda kufanya manunuzi kama ulikuwa hujapangilia nini cha kununua wauzaji watakushawishi na kukupangia nini unapaswa kununua hata kama ulikuwa hujapangilia.

Unatakiwa kuwa mkali sana katika matumizi ya fedha, ukiona kama hukupangilia kununua usinunue kwa sababu mara nyingi watu huwa wananunua kwa hisia halafu baadaye wanakuja kutathimini kwa akili kumbe hichi nilichonunua kilikuwa hakina hata maana. Hujawahi kwenda sehemu ukashawishika kununua kitu ambacho hata kilikuwa siyo muhimu na sasa unacho ndani lakini wala hukitumii je ungeitumia hiyo fedha kuweka akiba au kuwekeza ungekuwa mbali kiasi gani?

SOMA; Jambo Moja Muhimu La Kuzingatia Kabla Ya Kufanya Manunuzi Ili Kuepuka Kunasa Katika Mtego Huu

Punguza matumizi yasiyokuwa ya ulazima  na tumia fedha zako vizuri. Usinunue kwa hisia bali nunua ukiwa na fikra kamili.

Ukikutana na kitu ghafla na ukakipenda na ukawa na wasiwasi huenda utakikosa jipe mwezi mmoja kwanza kujifikiria je ni muhimu kuwa na kitu hicho ukijipa muda utashangaa mwenyewe kuona siyo muhimu.

Hatua ya kuchukua leo, usiongoze na hisia katika kununua bali ongozwa na akili. Kuwa na orodha yako ya kununua na usinunue kile ambacho hukupanga kununua.

Kwahiyo, usipokuwa makini katika manunuzi utakuwa ni mtu wa majuto kila siku. Zingatia haya uliyojifunza na utaokoa kiasi kikubwa cha fedha na utatumia fedha hizo kufanya mambo mafanikio.

Muhimu; kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la mimi ni mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa. Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga bofya hapa au nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha ya kiswahili bonyeza hapa.

Ukawe na siku bora sana rafiki.

Rafiki na mwalimu wako,

Deogratius kessy

0717101505/0767101504

deokessy.dk@gmail.com // kessydeo@mtaalamu.net

Asante sana

 

 

Published by Deogratius Kessy

Mwandishi,mwalimu na mjasiriamali. Unaweza kutembelea Blog yake ya www.kessydeo.home.blog kujifunza zaidi na unaweza kuwasiliana naye kwa namba 0717101505/0767101504 au kwa barua pepe deokessy.dk@gmail.com

Leave a comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: