Design a site like this with WordPress.com
Get started

Kitu Cha Kutomnyima Mtoto Katika Malezi

Mpendwa rafiki yangu,

Wazazi wengi wanawapenda watoto wao na hilo ni jambo zuri mzazi kuwajibika katika swala la upendo. Tunawalea watoto utafikiri kama vile tutaishi nao milele tuna watukuza watoto kwa kuwapa kile wanachotaka katika maisha yao.

Watoto wamekuwa wanawaendesha wazazi wakisema wanataka kitu fulani wazazi wasipokuwa nacho basi hapo nyumbani mtoto atasusa na wazazi watajitahidi kadiri ya uwezo wao kufanikisha kile anachotaka mtoto wao na kumpatia. Watoto wamekuwa ndiyo mabosi wanawaendesha wazazi wao, watoto wanalelewa kama vile yai kama wasemavyo waswahili.

Baada ya muda watoto wakianza kuharibika kadiri ya malezi wazazi wanaanza kutafuta msaada, kwanini mambo yameenda hivi au vile. Mzazi usipomfuatilia mtoto wako basi ujue unamwaribu na kumjenga wewe mwenyewe. Jukumu la malezi liko mikononi mwako hivyo ni vema kila siku kujua watoto au mtoto wako anaendeleaje, fanya kikao na kila mmoja umsikilize na siyo kumwachia msaidizi wa kazi tu.

Image result for TEACH YOUR CHILD TO LEARN CHALLENGES

Katika malezi ya mtoto hutakiwi kumyima mtoto adhabu. Utakapomyima adhabu pale anapokosa jua wewe ndiyo umechangia kumharibu mtoto wako na hivyo umekuwa na deni. Baadaye mtoto atakuja kukulaumu kwa uzembe wako kwanini hujampatia malezi bora.

Unatakiwa kumfundisha mtoto wako kukosa, hata kama unacho muda mwingine mwambie huna ili ajue duniani kuna kupata na kukosa. Hakuna mtu aliye na mkataba wa uhakika kuwa watoto au mtoto aliye naye ataishi naye milele hivyo usimlee mtoto malezi ya kitandawazi mlee mtoto ili aweze kujitegemea hata kama haupo ataishi misingi uliyomfundisha.

SOMA; Uwekezaji Muhimu Uliosaulika Katika Malezi Ya Watoto Kwenye Karni Ya 21

Mtoto akifanya kosa mpatie adhabu mwambie kwanini unamwadhibu na nini atakiwa kufanya ili asirudie kosa. Baada ya kumwadhibu endelea kumfanya kuwa rafiki yako ili aone kumbe kuadhibiwa ni siyo kujenga uadui na wewe mzazi. Tusiwanyime watoto adhabu, mpe kadiri ya mastahili yake.

Hatua ya kuchukua leo; mfundishe mtoto kukosa, mpatie adhabu pale anapofanya kosa. Mfundishe misingi ya maisha ili awe mtoto bora. Toa adhabu kwa kiasi kadiri ya mtoto na kosa na usimwadhibu mtoto ukiwa na hasira bali kuwa kawaida tu ndiyo umwadhibu.

Hivyo basi, mlee mtoto katika njia ipasayo naye hata iacha hata akiwa mzee. Wakati mzuri wa kukarabati paa la nyumba yako ni sasa wakati jua linawaka usisubiri mpaka wakati wa mvua. Wajibika ili mtoto awe bora.

Muhimu; kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la mimi ni mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa. Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga bofya hapa au nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha ya kiswahili bonyeza hapa.

Ukawe na siku bora sana rafiki.

Rafiki na mwalimu wako,

Deogratius kessy

0717101505/0767101504

deokessy.dk@gmail.com // kessydeo@mtaalamu.net

Asante sana

 

Published by Deogratius Kessy

Mwandishi,mwalimu na mjasiriamali. Unaweza kutembelea Blog yake ya www.kessydeo.home.blog kujifunza zaidi na unaweza kuwasiliana naye kwa namba 0717101505/0767101504 au kwa barua pepe deokessy.dk@gmail.com

Leave a comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: