Mpendwa rafiki yangu,
Linapokuja suala la fedha basi watu wengi nidhamu binafsi juu ya fedha hawana. Watu wakiwa hawana fedha, wanakua na mipango mizuri sana lakini wakishazipata fedha hizo ile mipango yote mizuri inapotea.
Wengi wanalalamika kuwa wakipata fedha haikai na pale fedha inapoisha ndiyo akili huwa inarudi.
Kuna kile kiwango cha fedha ambacho watu huwa wanakua nacho akilini. Wasipokuwa nacho watafanya kila mbinu ili kuhakikisha wahakuwa nacho lakini hata kiwango kikiwa kikubwa yaani mtu amepata fedha nyingi kuliko zile alizokuwa anapata atahakikisha anazitumia mpaka fedha zile zinaisha ndiyo akili itatulia. Natumaini huwa unawaona watu wakipata fedha dunia nzima watajua kama wanafedha na wakiwa hawana utawajua tena.
Sehemu pekee ambayo wanaweza wakafundishwa nidhamu ya fedha ni benki.
Benki huwa inamfundisha kila mtu thamani ya fedha, ukienda kukopa utapangiwa masharti tena yenye riba hata kama fedha ni yako na ukikiuka masharti hayo lazima sheria itakuadhibu vikali.
Unaweza ukajifunza nidhamu ya fedha kupitia benki, nenda kawaambie wewe huna nidhamu ya fedha hata kuweka akiba kwako ni shida waambie wawe wanakukata kama ni mshahara wako kiasi fulani cha fedha hata kabla hakijakufikia.
Njia nyingine ni kupunguza kiasi cha fedha unachokipata na unaiaminisha akili yako katika kiwango hicho na akili itaamini kuwa una kiasi fulani hivyo hata bajeti unazoweka zitakuwa ndani ya kile kiasi.
Hatua ya kuchukua leo; kuwa na nidhamu ya fedha, mtafute hata mtu ambaye unamwamini kupitia akauti yako ya simu kama Tigo pesa au mpesa unaweka namba za siri mbili na yeye mbili hivyo ukitaka kutoa fedha mpaka yeye aweke na wewe uweke.
Kwa namna hiyo utajifunza nidhamu binafsi ya fedha na utaweka akiba zako huko.
Hivyo basi, usikubali fedha ikutawale, ila wewe unatakiwa kuitawala fedha.
Jali fedha yako, tunza fedha.
Kila la heri rafiki yangu.
Rafiki na mwalimu wako,
Deogratius Kessy
Jiunge na mimi ni mshindi nimezaliwa kushinda kupitia namba 0717101505 na kupata vitabu vya kujisomea.