Mpendwa rafiki yangu,
Mtu mmoja alisema hakuna kazi ngumu kama kuongoza watu, ni bora kuongoza kondoo wataweza kwenda njia moja lakini siyo watu. Kuongoza watu ni kama vile kuswaga paka kila mmoja atakimbilia njia yake anayetaka yeye lakini ukiswaga kondoo wote wataenda njia moja.
Hapa unaweza kuona kuwa ni ngumu sana kuwabadilisha watu vile unavyotaka wewe. Lakini iko njia ya kutaka kumbadilisha mtu na ndiyo njia tunayokwenda kujifunza sasa.
Mtu amezaliwa na tabia yake halafu wewe unataka kumbadilisha kwa siku moja ni kitu ambacho hakiwezekani. Ukitaka kumbadilisha mwenza wako njia rahisi ni wewe kuanza kubadilika. Kile ambacho wewe unataka utendewe hebu anza na wewe kumtendea mwenzako.
Tunapenda sana kuona mabadiliko kutoka kwa wengine lakini hatupendi kuona mabadiliko kutoka kwetu. Watu wanapoteza muda mwingi kulalamika kuwa wenza wao hawataki kubadilika wakati wao hawachukui hatua ya kubadilika. Kama mwenza wako hataki kubadilika mwache asili itambadilisha, fanya kazi ya kujibadilisha kwanza wewe mwenyewe.
SOMA; Kansa Inayomaliza Wanandoa Wengi
Wanandoa wengi wanapata shida ya kuwabadilisha wenza wao wakati wao hawataki kubadilika. Kuwa sehemu ya mabadiliko unayotaka kuyaona kwa mwenza wako. Pia, katika maisha ya ndoa inabidi kutumia kanuni ya almasi (platinum rule) ambayo inasema hivi,mfanyie mwenzako kile ambacho yeye anapenda kufanyiwa. Ndiyo, umemkuta mwenzako kuna kitu anapenda hivyo wewe unataka kumbadilisha vile unavyotaka wewe. Tuko tufaouti, siyo kile nachopenda mimi na wewe utakipenda inatakiwa umpe uhuru mwenzako lakini uhuru bila nidhamu ni kazi bure.
Maisha yana pande mbili raha na maana. Kuna muda mtu anatakiwa kupata raha na kuna muda unatakiwa kuishi maana. Usiegemee tu upande mmoja wa maana au wa raha kila upande una sehemu yake.
Mpatie mwenza wako kile anachopenda yeye na yeye atakupa kile unachotaka wewe. Mpe uhuru wa kutumia vizuri kanuni ya almasi. Kanuni ya dhahabu inasema mtendee mwingine kile ambacho wewe unataka kutendewa, sasa kuna kitu ambacho wewe utapenda kutendewa lakini mwenzako hakipendi ndiyo maana kuna kanuni ya almasi inayokwenda kuleta usawa.
Hatua ya kuchukua leo; kama unataka kumbadilisha mwenza wako jibadilishe kwanza wewe mwenyewe. mtendee mwenza wako kile ambacho anapenda kutendewa.
Hivyo basi, kuwa sehemu ya mabadiliko unayotaka kuyaona kutoka kwa mwenza wako. Ukitaka mwenzako abadilike anza kwanza kujibadilisha wewe mwenyewe.
Muhimu; kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la mimi ni mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa. Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga bofya hapa au nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha ya kiswahili bonyeza hapa.
Ukawe na siku bora sana rafiki.
Rafiki na mwalimu wako,
Deogratius kessy
0717101505/0767101504
deokessy.dk@gmail.com // kessydeo@mtaalamu.net
Asante sana