Mpendwa rafiki,
Kuna mambo ambayo kila mtu anaweza kufanya katika maisha yake. Kuna watu wanasema mambo ni magumu lakini hata mambo yawe ni magumu kiasi gani watu kila kukicha hawaachi kufanya biashara hiyo, je unajua ni biashara gani? ni biashara ambayo imefanywa na wengi na inaendelea kufanywa na wengi na wanaoamua kuifanya kwa vitendo kweli inawalipa na kuwafanya wapate mafanikio makubwa sana.

Wengi wanaishia kupata hasara katika biashara hii kwa sababu wakishaamua kuifanya wanaweka mikono mifukoni huku wakisubiri biashara hiyo itajiendesha yenyewe na yeye abakie kuvuna tu. Yaani mtu akishapanda yeye wala hana hata wasiwasi anasubiria avune tu. Ni kama vile mtu anayewasha moto ni rahisi kuwasha moto lakini ili moto uendelee kuwaka unatakiwa uendelee kuchochea ili upate nishati hali kadhalika hata kwa mwendesha baiskeli ili aweze kubaki katika mwendo wake wa baiskeli lazima endelee kupiga pedeli bila kuchoka. Kumbe maisha ni safari na siyo kuanzisha na kuacha bali kuendelea kukifanya kile kitu kila siku ili kupata matokeo mazuri.
SOMA; Jinsi Wafanyabiashara Wanavyofukuza Wateja Wao
Hakuna kitu kirahisi kufanya duniani kama hiki, hakuna biashara rahisi inayopendwa kufanywa na kila mtu kama hii na hiyo siyo nyingine bali ni biashara ya kupanga. Kitu ambacho ni kirahisi kwa kila mmoja wetu basi ni kupanga kwa hilo kila mtu anaweza lakini je kufanya? Ni wangapi tumepanga mambo mengi mwaka kufanya na huenda hata yale tuliyopanga hakuna hata moja tuliyoyafanyia kazi? Tena huwa tunapata hamasa kweli katika kupanga lakini shida iko katika utekelezaji tu.
Kila siku mamilioni ya watu wanaishia kufanya biashara hii na kupata hasara tu kwa sababu kama umeamua kupanga mipango yako bila kuchukua hatua ni sawa na bure. Nina kubali kabisa kuwa watu wanapanga mipango kweli tena mizuri lakini je wangapi wanaitekeleza mipango yao?
Rafiki, kama unapenda kufanya biashara hii ya kupanga tu mipango bila kuchukua hatua ni bora kuacha kuipanga. Kwa sababu kama unapanga kila siku na huchukui hatua ni kupoteza muda tu, yaani unakaa wewe mwenyewe kwa akili yako timamu unaweka mipango yako vizuri lakini katika utekelezaji unakuja kujisaliti wewe mwenyewe. Mfano mzuri uko hata katika nidhamu ya kuamka mapema asubuhi ni wangapi wanaweka alamu lakini ikianza tu kulia wanakimbilia kuizima mara moja ili iwaondolee kero na aendelee kupiga usingizi.
SOMA;Kama Unataka Kufanikiwa Kwenye Mipango Yako Nunua Vitu Hivi Viwili
Hatua ya kuchukua leo, kila kitu kinahitaji kufanyiwa kazi ili kiweze kuonekana katika matokeo. Biashara nzuri ni ya kufanya na kuanzia leo acha kufanya biashara ya kupanga kama unapanga basi fanyia kazi kile ulichopanga kufanya kwa wakati siyo tu kuishi kupanga lakini muda unaenda na huchukui hatua.
Hivyo basi, kila mtu anapenda kufanikiwa lakini wale wanaopanga na kuchukua hatua ndiyo wanafanikiwa lakini wengine wote wanaishia kutamani na kusema. Ingia urafiki na kufanya kwa vitendo na vunja urafiki na mipango ambayo haitekelezeki.
MUHIMU; Kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la MIMI NI MSHINDI jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa. Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga bofya HAPA au nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha ya Kiswahili bonyeza Hapa.
Ukawe na siku bora sana rafiki.
Rafiki na mwalimu wako,
Deogratius Kessy
0717101505/0767101504
deokessy.dk@gmail.com // kessydeo@mtaalamu.net
Asante sana