Mpendwa rafiki,
Licha ya watu kukusanya fedha kila siku lakini kinachowarudisha watu nyuma nidhamu ya fedha. Kila fedha ina thamani inategemea inaingia katika mkono wa nani. Je mkono wako ukisha pesa inapandisha tamani ya pesa au inashusha thamani ya pesa? Thamani ya pesa iko katika mikono ya mtu je mikoni yako ni ya dhahabu katika pesa?

Watu ni rahisi sana kutumia lakini ni ngumu kujua kila fedha yao wanayotumia imetukika katika maeneo gani. Hivi rafiki kwa mfano tu wa kawaida nikikuambia naomba jumla ya mapato na matumizi ya mwezi machi utaweza kuniambia ni kiasi gani? ukimuuliza mwingine atakutolea macho. Nilikuwa sehemu moja nafundisha nikamuuliza ndugu mmoja ukiweza kunitajia jumla ya mapato na matumizi yako ya mwezi januari nakupa zawadi akasema hajui na aliishia kucheka tu.
Katika biashara , kazi watu wakipata hela ikiisha bila kujua utasikia wakianza kulalamika ni chuma ulete. Natumaini umeshawahi kuyasikia haya katika jamii yako kwa wafanyabishara wengi wakilalamika kuwa kuna tatizo la chuma ulete. Je umeshawahi kusikia benki yoyote imetangaza au kulalamika kuwa chuna chuma ulete wanawaibia hela zao? Kama hujawahi kusikia ni kwanini wao hawalalakimi na ndiyo wanadhamana ya kutuza fedha nyingi ukilinganisha na wewe? Kama wewe ulishawahi kusikia benki inalalamika juu ya chuma ulete tafadhali naomba uniambe rafiki.
Kwanini huwajawahi kusikia benki wanalalamika juu ya chuma ulete? Kwa sababu benki kila siku wanahakikisha wanafanya mahesabu kwa kila senti inayoingia na kutoka. Lazima wahakikishe kiasi cha hela iliyotoka na iloyoingia zinabalansi vizuri. Je wewe unafanya hivyo? Unaandika kila siku matumizi yako? unafanya biashara unalalamika kuna chuma ulete je huwa una fanya mahesabu kila siku kuhakikisha umepata kiasi gani, umetumia kiasi gani?
SOMA; Njia Nzuri Ya Kugundua Fedha Zako Zinaenda Wapi
Shida kubwa ya chuma ulete ni kutoandika kila senti inaoingia katika mkono wako na ile inayotoka. Ukiwa ni mtu tu wewe wa kutumia tu na pale unapokuja kuishiwa unaanza kumtafuta mchawai yuko wapi kumbe mchawi ni wewe mwenyewe.
Benki ni sehemu pekee inayowafundisha watu kuwa na nidhamu ya fedha. Kama huwa nidhamu ya fedha basi nenda benki kaongee nao waambie wewe huna nidhamu ya fedha halafu watakufundisha kama wewe mwenye umeshindwa kujiongoza na kukosa nidhamu binafsi.
Hatua ya kuchukua leo, kama unataka usikie chuma ulete katika maisha yako basi hakikisha unajua kila fedha inayoingia na inayotoka kwa kuandika na kupiga mahesabu vizuri. Kuwa kama benki na tengeneza mfumo kama benki utakaokulazimisha kila siku hesabu zikamilike.
Hivyo basi, kama wewe ni mfanyabiashara mdogo jipe nidhamu ya fedha na kamwe hutosikia chuma ulete. Kila siku piga hesabu zako vizuri kama benki wanaweza kukaa chini kila siku baaada ya kufunga mpaka wahakikishe hesabu zimekamilika kwanini wewe ushindwe na haitoweza kukuchukulia hata muda mrefu. Fanya hivyo kujua wapi fedha zako zinaenda.
SOMA; Njia Rahisi Ya Kujijua Kama Bado Hauna Uhuru Wa Kifedha
MUHIMU; Kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la MIMI NI MSHINDI jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa. Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga bofya HAPA. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha ya Kiswahili bonyeza Hapa.
Ukawe na siku bora sana rafiki.
Rafiki na mwalimu wako,
Deogratius Kessy
0717101505/0767101504
deokessy.dk@gmail.com // kessydeo@mtaalamu.net
Asante sana