Design a site like this with WordPress.com
Get started

Hakuna Kitu Kigumu Kufanya Kama Hiki Kwenye Maisha Yako

Hakuna kitu kigumu kama kumbadilisha mtu tabia. Watu wanataka kuishi kama vile walivyo hata kama unaona kitu fulani ni cha msaada kwao bado watakuona wewe unajisumbua kwa kile unachotaka kufanya. Watu wamezaliwa na tabia zao ambazo zina zaidi ya miaka ishirini leo hii uje umbadilishe mtu ni ngumu sana.

No automatic alt text available.

Hata umwamasishe mtu kiasi gani juu ya kubadilisha tabia fulani katika maisha yake bado ataona kama vile wewe unayetaka kumbadilisha ndiyo hauko sahihi.  Kwa mfano, mtu ana zaidi ya miaka 30 hapa duniani na amekuwa katika utamaduni wake hakuna watu anayewaona wakiwa na ule utamaduni wa kusoma vitabu leo hii umwambie anze kusoma hata weza kukuelewa haraka. Kwa sababu ile tabia kwake imeshajijenga miaka na miaka halafu wewe unataka kumbadilisha lazima atakuona mtu wa ajabu.

Rafiki, kuna kitu kinaitwa haiba. Sasa haiba kwa lugha rahisi ni jinsi vile mtu alivyo, jinsi unavyoina tabia yake. Kila mtu hapa ana haiba yake ndani yake hivyo ni vizuri kujua haiba ya mtu unayetaka kumbadilisha kwa sababu watu wengine wanafanya kile wanachofanya kwa sababu ndiyo haiba yao.

Lakini mtu pekee wa kuweza kumbadilisha hapa duniani wewe mwenyewe, ukitaka kubadilsha tabia za watu utapata shida. Unachotakiwa wewe ni kuishi tabia zile unazopenda na kama mtu anaona zinamfaa atazifuata yeye mwenyewe. Kuwa sehemu ya mabadiliko unayotaka kuyaona katika eneo fulani la maisha yako na usipoteze muda kumbadilisha mtu aishi vile unavyotaka wewe bali wewe ishi vile unavyotaka wewe na kama ni mtu anayetaka kubadilika atabadilika.

SOMA; Hii Ndiyo Kazi Ngumu Kuliko Kazi Zote Duniani

Watu ambao ni rahisi sana kubadilika ni wale wenye kiu ya mabadiliko ya kweli kutoka ndani. Mtu ambaye anataka kubadilika huwezi kutumia nguvu kumbadilisha kwa sababu yeye mwenyewe anayapenda mabadiliko. Mzigo mkubwa ni kutaka kumbadilisha mtu ambaye hataki kubadilika, wanasema ni rahisi kumpeleka punda mtoni akanywe maji lakini si rahisi kumlazimisha kunywa maji.

Kazi yako kubwa iwe ni kuwapeleka watu kunywa maji lakini usiwalazimishe kunywa maji. Hapa namaanisha kuwa wahamasishe watu vile unavyotaka wawe lakini usiwalazimishe kubadilika. Mtu anayechukua hatua za kubadilika kwa hiyari ni moja kati ya watu wazuri sana walioweza kujitambua na unaweza kumwamasisha chochote na akafanya bila hata kusukumwa.

Hatua ya kuchukua leo rafiki, usimlazimishe mtu kubadili tabia yake, bali wewe ishi kile unachopenda wewe na kama atakipenda ataamua kubadilika mwenyewe. Kwa mfano, mimi wajibu wangu ni kukuandikia hapa kila siku hivyo kuamua kuchukua hatua ni wewe mwenyewe uamue kubadilika au kubaki kama ulivyo na wale wanaoona kuguswa wanachukua hatua kweli.

Kwahiyo, kila kitu katika maisha yetu kimejengwa na tabia. Kama ukiweza kubdili tabia basi utaweza kufanya chochote kile. Mtu anayependa mabadiliko ya kweli ya kutoka ndani hawezi kutafuta sababu lakini yule asiyependa mabadiliko ni rahisi kutafuta sababu kila siku kwanini asifanye au kwanini asibadilike.

MUHIMU; Kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la MIMI NI MSHINDI jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa. Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga bofya HAPA. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha ya Kiswahili bonyeza Hapa.

Ukawe na siku bora sana rafiki.

Rafiki na mwalimu wako,

Deogratius Kessy

0717101505/0767101504

deokessy.dk@gmail.com // kessydeo@mtaalamu.net

Asante sana 

Published by Deogratius Kessy

Mwandishi,mwalimu na mjasiriamali. Unaweza kutembelea Blog yake ya www.kessydeo.home.blog kujifunza zaidi na unaweza kuwasiliana naye kwa namba 0717101505/0767101504 au kwa barua pepe deokessy.dk@gmail.com

Join the Conversation

1 Comment

Leave a comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: