Design a site like this with WordPress.com
Get started

Kama umeweka Mipango Na Malengo Yoyote Mwaka Huu Usiache Kusoma Hapa

Habari ya leo rafiki? Leo ni siku ya tatu ya mwezi wa kwanza, kama kuna kitu ulianza kufanya kila siku tokea mwaka huu uanze na bado unaendelea kufanya basi endelea kila siku na msimamo huo huo baada ya mwezi huu wa kwanza kitu hicho kitakuwa ni tabia kwako.

Kwa mfano, unataka nidhamu ya kujijengea kuamka kila siku muda huo uliopanga bila kuacha na ulijewekea utaanza tarehe moja na mpaka leo tarehe tatu hujaanza bado hujachelewa anza sasa, usisubiri mpaka mwezi ujao ndiyo uanze bali anzia siku inayofuata.

Rafiki, najua huu ni mwaka mpya na huenda umeweka mipango yako mbalimbali ya kuitimiza mwaka huu. Ni vizuri sana kuweka mipango kuliko kuishi bila mipango. Lakini rafiki ninakwenda kukupa tahadhari juu ya mipango uliyopanga mwaka huu.

Vizuri kwa kupanga lakini katika mipango uliyopanga mwaka huu unatakiwa kujiandaa kupokea matokeo tofauti na vile ulivyopanga kupata. Kwa sababu kuweka mipango siyo ndiyo njia ya uhakika ya kuthibitisha kuwa umefanikiwa kupata.

Mambo yanaweza kwenda tofauti kabisa na ulivyopanga, yule uliyekuwa unamtegemea atakusaidia katika mipango uliyopanga huenda asikusaidie, huenda asikupe ushirikiano uliotegemea ungeupata.

Kwahiyo, jiandae kiakili kukabiliana na matokeo yoyote utakayopata iwe ni kupata au kukosa kwa sababu yote ni sehemu ya maisha. Mambo yanabadilika na watu wanabadilika hivyo ni marufuku kuweka tegemeo lako kwa watu asilimia mia moja.

Huwa nawashauri watu chochote unachotegemea kukipata jiandae kisaikolojia kupata matokeo yoyote kwa sababu kama ulijiwekea utafanikiwa kupata kitu fulani na ulijipa asilimia 100 mambo yakienda ndivyo siyo utaumia sana na litakutesa hilo jambo na kukufanya ushindwe kuendelea na mambo mengine.

Ukomavu wa mtu uko katika kupokea aina yoyote ya matokeo anayopata iwe ni faida au hasara halafu utulivu wake wa akili uko pale pale yaani unakuwa huendeshwi na matukio. Hii inaitwa huna cha kupoteza yaani you have nothing to lose.

Kwahiyo, jiandae rafiki yangu kukabiliana na hali yoyote hapo mbele yako na chochote kitachotokea ona ni kitu cha kawaida wala kisikufanye ushindwe kuendelea na maisha yako ya kawaida.

Hatua ya kuchukua leo, jiandae kiakili kukabiliana na matokeo yoyote, hata pale mambo yanavyokwenda tofauti huwezi kuumia utaona ni kitu cha kawaida tu.

Kila mtu anapaswa kuishi maisha ya kujiandaa na chochote kwa sababu hata hivi ambavyo tunavyoleo unaweza ukavikosa na kunyang’anywa kwahiyo, ukijiandaa na siku ukinyang’anywa haitokuumiza.

Karibu sana rafiki ujiunge na familia ya Mimi ni mshindi, jiunge na mfumo wetu wa kupokea makala kupitia email list, hapo chini kabisa kuna fomu ijaze. Pia, kuna vitabu vizuri sana vilivyoandikwa kwa lugha nzuri na rahisi ya kiswahili chukua hatua ya kununua ili vikusaidie kukupa maarifa ndani ya mwaka huu. Vitabu vyetu ni Funga ndoa na utajiri, kwanini msamaha na ongea lugha yako vyote vitatu viko katika mfumo wa nakala tete yaani soft copy na bei ya kila kitabu ni elfu tano tu. Karibu sana

Rafiki na Mwalimu wako,
Deogratius Kessy
0717101505/0767101504.

Published by Deogratius Kessy

Mwandishi,mwalimu na mjasiriamali. Unaweza kutembelea Blog yake ya www.kessydeo.home.blog kujifunza zaidi na unaweza kuwasiliana naye kwa namba 0717101505/0767101504 au kwa barua pepe deokessy.dk@gmail.com

Leave a comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: