Design a site like this with WordPress.com
Get started

Kauli Mbaya Ya Kuepuka Kujiambia Mwaka 2018

Rafiki, leo ni ukurasa mpya kabisa wa maisha yetu hivyo ni nafasi nzuri kwetu kuitumia vizuri zawadi tuliyoipata leo.

Ukianza kufikiria kwenye uhaba tena mwaka huu wa 2018 tarajia kupokea uhaba kwa sababu hakuna kitu ambacho mtu anakipata tofauti na ile picha aliyojijengea akili mwake. Kile unachokifikiria ndicho unachokuwa kama utafikiria katika ushindi muda mwingi basi ushindi ndiyo utakua unatawala maisha yako.

Unakutana na mtu anajiambia kauli mbaya kama hii katika maisha yake eti nimekosa nini mimi” hii siyo kauli ya kujiuliza kabisa mwaka huu eti umekosa nini mimi kwa sababu tu mipango yako haijaenda sawa kama ulivyopanga, mambo yako bado hayajakaa vizuri kile unachokitafuta bado hujakipata kwahiyo ukiangalia mambo yanavyokuendea kitu sahihi unachoona cha kujiuliza ni umekosa nini. Rafiki, hii siyo kauli kabisa ya kujiuliza kwa sababu ukianza kujiuliza umekosa nini utapata urodha ndefu ya mambo ambayo huna. Muda mwingine utakiwa kushukuru hata kwa kila jambo.

Hata kama umepatwa na kitu gani bado una nafasi kubwa ya kushinda kwenye maisha yako. Ukiaguka bado una nafasi ya kuamka na kuendelea na safari, kuwa mtu wa shukrani hebu shukuru tu hata kwa zawadi ya mwaka mpya kwa sababu kama ukiendelea kutokua na shukrani utaendelea kuishi maisha magumu sana, fikiria wenzako wote walioshindwa kuendelea na maisha hapa duniani halafu wewe umeipata bado unalalamika eti umekosa nini, kauli kama hii ni hasi sana, wewe jivunie hata kwa kuwa hai siyo mwaka wa kujiuliza umekosa nini bali ni mwaka mpya kuthubutu na kushukuru kwa matokeo au hatua ndogo ndogo unazopiga kila siku. Haijalishi unafanya nini lakini hakikisha unasogea mbele kama unaweza kukimbia kimbia, kama unaweza kutembea tembea ili mradi tu usogee.

Mwaka mpya ni mwaka wa kuchagua kubadilika na kusogea. Usikubali kila mwaka kubaki hapo hapo na kauli za nimekosa nini badala yake anza kufurahia na kushukuru baraka ulizonazo.

Kila mtu ana kitu cha kipekee ndani yake. Jikubali kuwa wewe ni mshindi na kubali kuuza upekee wako na watu watanunua upekee wako kwa sababu upekee wa mtu utatoa thamani ambayo haifanani na mtu mwingine yoyo yule. Wewe ni mshindi na umezaliwa hivyo mwaka huu ni mwaka wa kufikiria ushindi na siyo udhaifu wako bali fikiria ubora wako tu.

Hatua ya kuchukua leo, acha mara moja kauli za kujiona wewe hustahili kuwa bora au kupata mafanikio hapa duniani kwa sababu tu ya kupata changamoto kidogo. Maisha yana changamoto hivyo ni vema ukakabiliana nazo na kadiri unavyotatua ndivyo unatengeneza nafasi nzuri kwako kwa kuona fursa kubwa mbel yako.

Kwahiyo, udhaifu mkubwa ni pale unapojiona wewe kuna kitu umekosa kwenye maisha yako ndiyo maana unaanza kujiuliza kauli hasi, haujakosa kitu bali una dhahabu ndani yako ila hutaki kuitumia vizuri, hebu leo fanya zoezi la kuandika mambo 50 unayoweza kufanya halafu yafanyie kazi na chagua kimoja unachopenda kufanya na kifanye kwa moyo.

Kumbuka kujiunga na mfumo wetu wa kupokea makala katika email yako, lakini pia usisahu kujiunga na kundi letu la wa wasapu la Mimi ni mshindi ili uweze kujifunza na kufaidika na kupiga hatua kwenye maisha yako.

Rafiki na Mwalimu wako,
Deogratius Kessy
0717101505/0767101504
deokessy.dk@gmail.com, kessydeo@mtaalamu.net
Asante sana

Published by Deogratius Kessy

Mwandishi,mwalimu na mjasiriamali. Unaweza kutembelea Blog yake ya www.kessydeo.home.blog kujifunza zaidi na unaweza kuwasiliana naye kwa namba 0717101505/0767101504 au kwa barua pepe deokessy.dk@gmail.com

Leave a comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: