Design a site like this with WordPress.com
Get started

Adui Wako Mkubwa Mwaka 2018

Heri ya mwaka mpya 2018 rafiki. Kama unasoma hapa naamini wote tumestahilishwa kuingia mwaka 2018 kwa furaha, amani na mafanikio makubwa ndani ya mwaka huu mpya wa 2018.

Mabadiliko makubwa ya mwaka 2018 kwa siku ya leo na zijazo ni tarehe pekee yake. Kwa sababu gani hii ndiyo asili yake kama jua ulilo liona jana ndilo jua hilo hilo utakalo liona leo. Lakini,
Mabadiliko makubwa ndani ya mwaka mpya 2018 yapo endapo utabadili mfumo wa maisha yako uliokuwa unaishi. Kama utachukua hatua ya kubadili na kuishi yale ambayo umepangilia kufanya basi mwaka huu utakuwa mwaka bora kuliko miaka mingine yote.

Haina haja hata ya kuandika malengo kama utaendelea kuishi maisha yale yale halafu unategemea kupata mafanikio makubwa. Ni uongo rafiki yangu, kama unataka uwe mwaka mpya kweli kwako basi anza na kubadilika wewe mwenyewe kwanza na vingine vitabadilika.

Rafiki, kwa kuwa leo ni mwaka mpya, basi napenda kutushirikisha adui mkubwa wa mwaka 2018 kwako na jinsi ya kuwa naye makini adui huleo, Adui mkubwa kwako mwaka 2018 ni ujinga.

Ndugu, ujinga ndiyo adui mkubwa kwako, ujinga ni kama ukungu unaokuzuia kuona mbele. Kwa kuwa umeshamfahamu adui wako ni ujinga unabidi uchukue hatua sasa za kumkabili adui huyu. Je namna gani unaweza kumkabili adui huyu?

Anza kuwa rafiki wa kutafuta maarifa an ujinga ataanza kuondoka mwenyewe, usikubali mwaka huu kuendelea kumkumbatia ujinga. Tafuta maarifa na maarifa yatakupa mwanga ndani ya mwaka 2018.

Tafuta marafiki chanya, njia nyingine ya kumuondoa ujinga ni kuwa na marafiki chanya ambao wanawaza katika mabadiliko chanya tu. Ukiendelea kubaki na marafiki hasi, makundi hasi basi, utaendelea kupata matokeo yale yale. Huwezi kupata matokeo mapya kama utaendelea kubaki na mtazamo ule ule na marafiki wale wale hasi. Jiondoe kabisa kwenye sehemu ambayo haikupi faida chanya na tafuta watu chanya wa kuambatana nao mwaka 2018.

Usipojenga mtandao na watu chanya basi umechagua kubaki hapo hapo ulipo, badili watu uliokuwa unaambatana nao kama walikuwa ni mtandao hasi basi, jiondoe na anza na watu chanya watakaokupa mwaka ndani ya mwaka 2018.

Rafiki, ujinga uko kila idara ya maisha yetu, ujinga katika masuala ya fedha, muda na mambo mengine mengi. Kama unaona unajinga eneo fulani chukua hatua sasa ya kujifunza na toka katika ujinga huo na anza mabadiliko chanya kwenye maisha yako.

Hatua ya kuchukua leo, mabadiliko ya mwaka mpya ni pale wewe mwenyewe utakapoamua kubadilika lakini usipoamua kubadilika mambo yatabaki kama yaliyokuwa hapo awali.

Rafiki, kama kuna kitu hukijui ni bora ukajifunza kuliko kuendelea kubaki na ujinga, kujisifia kuwa hujui kitu fulani siyo sifa nzuri bali ni sifa mbaya ambayo haitakusaidia hata kidogo, kitakachokusaidia ni kuchukua hatua ya kujifunza sasa.

Rafiki, karibu sana mwaka 2018, karibu ujiunge na familia ya mtandao huu kupitia kundi la wasapu liitwalo Mimi ni mshindi, nimezaliwa kushinda. Kujiunga na kundi hilo na kupata maarifa chanya kila siku tuwasiliane ili uweze kujiunga. Pia, kuna vitabu nilivyoviandika vinavyopatikana katika mfumo wa soft copy kama vile Funga ndoa na utajiri, kwanini msamaha na ongea lugha yako, sauti yako ya ndani ndiyo mafanikio yako.

Rafiki na mwalimu wako,
Deogratius Kessy
0717101505/0767101504,
deokessy.dk@gmail.com, kessydeo@mtaalamu.net
Asante sana

Published by Deogratius Kessy

Mwandishi,mwalimu na mjasiriamali. Unaweza kutembelea Blog yake ya www.kessydeo.home.blog kujifunza zaidi na unaweza kuwasiliana naye kwa namba 0717101505/0767101504 au kwa barua pepe deokessy.dk@gmail.com

Leave a comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: