Design a site like this with WordPress.com
Get started

Uchambuzi wa Kitabu;Mambo 31Niliyojifunza Kutoka Katika Kitabu cha Many Miles To Go

Habari ya leo mpendwa Rafiki na msomaji wa mtandao wa Kessy Deo? hongera kwa siku hii ya leo na karibu sana katika uchambuzi wa kitabu kama ilivyokawaida leo ninakwenda kukushirikisha wa kitabu cha Many Miles to Go kilichoandikwa na mwandishi mashuhuri duniani Brian Trancy na haya ni machache kati ya mengi.

Uchambuzi Wa kitabu; many Miles to go na mwandishi Brian Trancy

1. Unajifunza kufanikiwa kwa kuendelea kufanikiwa. Unapofanikiwa zaidi ndiyo unaongeza kasi zaidi ya kufanikiwa. Hatua moja ya kufanikiwa inakupa nguvu na uwezo Wa kujiamini kuendelea kufanikiwa zaidi.

2. Hakuna wa kukuzuia zaidi ya wewe mwenyewe. Ukiamua kuwa king’ang’anizi ng’ang’ania mpaka upate kile unachokitafuta. Usiishie njiani hata siku moja komaa na kile unachofanya mpaka upate matokeo.

3. Jenga tabia ya uadilifu, ukarimu, huruma, nk. Maisha yanaendeshwa na misingi uliyojiwekea na ukishakuwa na misingi tayari inakuwa tabia.

4. Unajifunza kuwa jasiri kwa kuwa jasiri, unajifunza kutatua kwa kutatua. Unajifunza kuendelea kwa kuendelea kwenda, kuendelea kung’ang’ania kwa kung’ang’ania.

5. Unathamani isiyokuwa na mipaka. Kila kitu unachokihitaji kipo ndani yako ni wewe tu kujitumia vizuri.

6. Angalia nyuma na jifunze kupitia uzoefu wako Wa maisha. Mpaka hapo ulipo unauzoefu mkubwa kama kusafiri tayari umeshasafiri safari hebu jifunze kupitia uzoefu wa safari ulizosafiri katika maisha yako.

7. Dunia imeundwa kuwa kama unataka kufurahia mazuri yake basi, uwe tayari na kuvumilia mabaya yake. Uwe unataka au usitake lazima uwe navyo vyote.

8. Nenda kijasiri sehemu ambayo hakuna mtu alishawahi kwenda kabla.

9. Kuwa mwaminifu na wewe mwenyewe. Umezaliwa kwa makubwa, kuwa na ndoto na fanya kazi ili kufanya ndoto yako kuwa kweli.

10. Kama unataka kufikia malengo fulani ya kifedha unaweza kufungua akaunti maalumu na ukawa unaweka huko kidogo kidogo mpaka unafikia lengo lako. Haba na haba hujaza kibaba.

11 Maelfu ya ndoto zinakufa kila siku bila kuzaliwa hii ni kwa sababu waotaji wa ndoto hizo wanakosa ujasiri wa kuchukua hatua ya kwanza nayo ni kufanya.

12. Ili kuikuza akili yako pendelea sana kuifikirisha katika kutafuta suluhusho kuliko matatizo.

13. Jifunze kupitia changamoto unazokutana nazo kila siku. Lenga kwenda mbele na jifunze kupitia yaliyopita na yaache yaende.

14. Jukumu la maisha yako ni lako mwenyewe. Usipowajibika hakuna mabadiliko yoyote utakayoweza kuyapata katika maisha yako. Wewe ndiyo kila kitu kwenye maisha yako, kila kitu, vitu vyote ni juu yako.

15. Maisha ni mafanikio ya matatizo yanayoendelea yanaweza kuwa makubwa au madogo. Ni kama mawimbi kwenye bahari huwa hayasimami ndiyo yaliyovyo matatizo kwenye maisha yetu.

16. Kuwa wazi kwa taarifa Mpya, kuwa tayari kupokea mrejesho na masahihisho binafsi. Jiweke tayari kuwa utakosea na utapata njia bora ya kutokea.

17. Goethe aliwahi kusema , kuwa na vingi lazima sisi wenyewe tuwe zaidi. Kwa mfano, kama wewe unakampuni unatakiwa kuwa na maarifa mengi kuliko, yaani wewe uwe zaidi ya kampuni.

18. Habari njema ni kwamba unaweza kujifunza kitu chochote unachohitaji kufanikiwa katika lengo lako. Kama unataka kujifunza na lugha inakuwa changamoto basi, jifunze, kama una kikwazo cha chochote kinachokuzuia wewe kushindwa kujifunza basi hakuna namna jifunze hiyo lugha Mpya kwani kutojifunza unajinyima mambo mengi sana.

19. Unapoamua kubadili fikra zako, umebadili maisha yako. Usipobadili fikra utabaki hapo hapo bila kuendelea mbele. Badili mtazamo kwani mtazamo wako wa akili ndiyo umebeba dira ya maisha yako.

20. Unapoanza safari ya kitu fulani na hujui utafikaje usihofu kama ni kutembea endelea kutembe, kama ni kuendesha baiskeli endelea kupiga pedeli, kama ni gari endelea kupiga gia, wako wasamaria watakusaidia mbele, waku watu wakarimu watakusaidia katika safari yako wewe nenda kila kitu kitajipa mbele ya safari huko huko.

21. Kitu pekee cha kufanya pale mambo yanapoenda vibaya muda mwingine ni hakuna. Kubaliana na hali iliyotokea, mambo mengine huwa yanajisahihisha yenyewe bila kufanya kitu.

22. Mshahiri Robert W. Service anasema, ni rahisi kupambana wakati mambo yote yako sahihi, au kila kitu kipo sawa.

23. Hakuna somo la bure. Kila changamoto unayopitia unalipia gharama fulani, hivyo usitegemee kupata somo la bure kwenye maisha jinsi unavyopata maumivu ya kitu fulani ndiyo gharama unayolipia.

25. Hesabu Baraka zako. Angalia mazuri katika kila hali utaona baraka zako. Ni

mwiko kwako kujihesabia mabaya kwenye maisha yako.

26. Ishi katika kiwango cha bajeti uliyojiwekea. Kila mtu huwa anajiwekea kikomo kwenye bajeti yake hivyo zingatia usitoke nje ya mipaka uliyojiwekea.

27.

27. Palipo na mashaka omba msaada ili upate uelekeo. Usisubiri upotee njia ndiyo uombe msaada wa kuuliza uelekeo sahihi.

28. Mafanikio makubwa yote yameanza na Imani kubwa. Kama unataka kufika mbali na kuwa na mafanikio makubwa basi anza kujenga Imani juu ya kile unachofanya.

29. Usilete maneno ya watu kuharibu ndoto yako. Kila mtu ana mtazamo wake na anayejua kile unachofanya ni wewe mwenyewe hivyo wanapoongea wewe wasikilize tu lakini katika kutenda ni kuamua kile ambacho unaona wewe ni sahihi kufanya.

30. Watu wengi huwa wanakata tamaa mapema pale wanapokaribia kupata mafanikio makubwa. Ni wazi huwa tunajidhulumu wenyewe kwa kukata tamaa mapema hivyo tusikubali kukata tamaa wakati hatujafanikiwa kwenye kile tunachokitafuta.

31. Tatizo letu siyo upungufu wa pesa kufanya wa kitu bali ni upungufu wa mawazo. Mawazo yakiwa mazuri hela zitakufuata na kwenda kule zinakohitajika.

Nakutakia kila la heri katika haya uliyojifunza leo. Kupata vitabu vizuri vya kiswahili kwa ajili ya kujisomea na kuongeza maarifa usisite kuwasiliana nami.

Rafiki na Mwalimu wako,
Deogratius Kessy
0717101505/0767101504
deokessy.dk@gmail.com
kessydeo@mtaalamu.net
Asante sana

Published by Deogratius Kessy

Mwandishi,mwalimu na mjasiriamali. Unaweza kutembelea Blog yake ya www.kessydeo.home.blog kujifunza zaidi na unaweza kuwasiliana naye kwa namba 0717101505/0767101504 au kwa barua pepe deokessy.dk@gmail.com

Join the Conversation

1 Comment

Leave a comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: