Design a site like this with WordPress.com
Get started

Uchambuzi Wa Kitabu Cha The Power of Purspose(Nguvu ya Kusudi)

Habari ya leo mpendwa rafiki na msomaji wa mtandao wa Kessy Deo? Ni matumaini yangu kuwa hujambo na unaendelea vizuri. Hongera kwa zawadi ya siku hii ya leo kwani leo ni siku nyingine bora na ya kipekee sana katika maisha yako hivyo basi, itumie vizuri rafiki siku yako ya leo.

Ndugu mpendwa, napenda kutumia fursa hii kukualika tena katika makala yetu ya leo ili tuweze kujifunza wote kwa pamoja. Leo nitakwenda kukushirikisha mambo muhimu niliyojifunza katika kitabu cha The Power of Purpose kilichoandikwa na mwandishi Richard J. Leider. Nitakushirikisha machache tu kati ya mengi lakini yatakwenda kubadilisha maisha yako kama ukiyafanyia kazi, furaha yangu nikukuona unabadilika na kuachana na maisha ya kimazoea hivyo karibu sana tujifunze.

Mambo Muhimu Niliyojifunza Katika Kitabu cha The Power of Purpose( Tafuta maana, Ishi bora na muda mrefu). (nguvu ya dhumuni,au kusudi) kilichoandikwa na mwandishi Richard J.Leider ni kama ifuatavyo;

Utangulizi,
Dhumuni au malengo yako makuu ni yapi?
Nini kina kutoa au  kinachokufanya kutoka kitandani asubuhi?

Kujua dhumuni lako hapa duniani ndiyo maana yenyewe. Mwandishi ametumia neno power, lenye maana nguvu yaani uwezo wa kutenda, kufanya au kuzalisha kitu.

Karibu nikushirikishe machache kupitia Kitabu hiki cha The power of Purpose.

1. Bila kuwa na kusudi , hakuna Maisha, bila kuwa na kusudi tumekuwa. Kusudi ndiyo linatufanya tuweze kuishi Maisha yenye maana hapa duniani. Je unajua kusudi la Maisha yako hapa duniani?

2. Dhumuni linamwezesha mtu kuishi muda mrefu na kuishi Maisha bora na yenye maana hapa duniani.

3. Kusudi lako ndiyo linaonesha utu wako na huruma yako.
Bila kusudi au dhumuni ni ngumu watu kukujua wewe ni nani.
Tafuta nini kusudi lako hapa duniani?

4. Kila mtu hapa duniani amekuja na zawadi ya kipekee. Hivyo basi. Tunaalikwa wote kuweza kutumia zawadi tulizopewa na hatimaye kutoa thamani duniani.
Usikubali kufa na thamani yako Bali kubali kuitoa na Kuijaza dunia.

5. Dhumuni au kusudi ndiyo kinachotupa ujasiri.
Dhumuni au kusudi ndiyo hutuwezesha sisi kuwa binadamu. Kama huna kusudi bado hujawa binadamu.

6. Watu ambao wanakusudi, lengo, wana ndoto na dira huwa wanakuwa na furaha katika maisha yao ukilingalisha na wote ambao hawana.
Pia, ndiyo watu wanaoishi maisha mazuri.

SOMA;Uchambuzi Wa Kitabu Cha Noble Purpose(Furaha Ya Kuishi Maisha Yenye Maana)

7. Mwandikie mtu barua pepe au ujumbe Wa kuandika na mkono kwa shukrani juu ya kitu Fulani.
Kumwandikia mtu ujumbe wa shukrani ni jambo chanya linalokuongezea hamasa ya kupata ushindi katika maisha yako.

8. Kuna watu wanaojitoa kwa ajili ya wengine kwenda na kuacha alama. Kwa mfano, Dr Reusch, ni mtu aliyepanda mlima Kilimanjaro unaopatikana bara la afrika nchini Tanzania. Ameandika vitabu vingi katika lugha mbalimbali, kama vile kijerumani, kiswahili na nk.
Ni mtu anayejua lugha zaidi ya 20 hapa duniani na zote kaziandikia vitabu.
Hapa, tunajifunza kuwa unapokuwa unajua lugha nyingi ni kutumia fursa hiyo kuandika vitabu kupitia lugha hizo.

9. Unatakiwa kufanya jambo litakalo acha alama katika Maisha ya watu. Ili uache alama katika maisha yako saidia watu wengine.

10. Katika kutafuta maana, mtu Marian w Edelman aliwahi kusema kuwa, huduma ndiyo kodi tunayolipa kwa ajili ya kuishi. Ndiyo kusudi kuu katika maisha yetu na wala mambo unayofanya kwa muda wako.

11. Watu wengi wanauliza nini maisha yamewafanyia. Mwandishi anasema tunatakiwa kuacha kuliza swali hilo na badala yake kuacha maisha yakuulize wewe.

12. Hamasa huwa inakuja kwa wote wanaoitafuta. Unapoanza ndiyo kusudi lako huanza kuonekana.
Usisubiri kupewa hamasa bali tafuta kusudi lako.

SOMA; Mambo Muhimu Yakujifunza Kutoka Katika Kitabu Cha The School Of Greatness

13. Ni machaguo yetu yaliyotufanya tuwe hivi tulivyo leo. Nguvu na vipaji tunavyotumia kila siku kutafuta maana, ni kwa sababu tunaviamini vitu hivyo.

14. Kuanzia leo unatakiwa kujiambia kuwa hujazaliwa bure. Umezaliwa kwa sababu ndiyo uko duniani. Umekuja duniani kutimiza kusudi lako na siyo kukaa bure, tambua umekuja dunia kwa sababu na utakiwa ukamilishe kusudi lako.

15. Fikiri kwa ukubwa, moja vitu ambavyo huwa wanajiaribia ni kufikiria vitu vidogo. Vitu vidogo vinauwa uwezo wako, vinashindwa kudhihirisha ile nguvu ya dhumuni au kusudi lililoko ndani yako.
Fikiria makubwa.

16. Hatuwezi kubaki watoto daima. Bali tunasonga mbele kupitia hatua mbalimbali za hekima na ukuaji.
Mtu lazima ukuwe siyo tu kimwili bali kiakili ambayo ndiyo hekima yenyewe.

17. Jifikirie mwenyewe kwa namna mpya. Ni zawadi gani uliyopewa kwa ajili ya kusaidia wengine? Una imba? Unafundisha wengine? Na mengine mengi.
Lazima ujue dhumuni au kusudi lako ili uwasaidie wengine.yake .

18. Licha ya kutokuwa na elimu ya juu na kazi kubwa bado kila mtu ana zawadi ndani yake. Kila mtu ndani ya kusudi la maisha yake ana kitu cha kipekee cha kuweza kuwasaidia wengine. Usife na kipaji chako bali kitoe ili kiweze kusaidia wengine.

19. Wasaidie vijana kutambua kusudi lao, kuza nguvu zao, timiza ndoto zao kwenye kile kitu wanachokipenda.
Waalike katika dunia ya kufanya kazi kwa nguvu Na furaha.

20. Kila mtu ana hadithi yake ya kusimulia hapa duniani. Hadithi zetu ni yale mambo tunayofanya kwa ajili ya wenzetu.
Huwezi kutengeneza hadithi kama maisha yako hujajitoa kwa ajili ya wengine.
Saidia watu kwa kipaji ulichonacho na ifanye dunia kuwa mahali salama kuishi kwa kila mmoja wetu.

21. Tumia kipaji chako kuleta utofauti duniani.
Kama una andika kuleta tofauti duniani, kama unaimba,basi imba kuleta utofauti duniani. Unazalisha mboga mboga, matunda basi, zalisha kuleta utofauti duniani.
Chochote unachofanya fanya kuleta utofauti duniani.

Kupata vitabu vya kujisomea Bonyeza maandishi haya.

Kila la heri rafiki,
Deogratius Kessy
0717101505/0767101504
deokessy.dk@gmail.com
Asante sana.

Published by Deogratius Kessy

Mwandishi,mwalimu na mjasiriamali. Unaweza kutembelea Blog yake ya www.kessydeo.home.blog kujifunza zaidi na unaweza kuwasiliana naye kwa namba 0717101505/0767101504 au kwa barua pepe deokessy.dk@gmail.com

Join the Conversation

1 Comment

Leave a comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: