Design a site like this with WordPress.com
Get started

Jeshi Muhimu Unalopaswa Kuliheshimu Hapa Duniani Kuliko Majeshi Yote

Habari ya leo mpendwa rafiki na msomaji wa mtandao wa Kessy Deo? Ni imani yangu kuwa hujambo na unaendelea vizuri huku ukiwa umeianza siku yako kwa ushindi mkubwa. Kuna watu kila siku lazima waianze siku yao kwa ushindi mkubwa na wengine wanaanza siku yao kwa kushindwa kabla hata hajamaliza siku yake.

Hakuna mtaji wa kuanza siku yako kwa ushindi bali ni kuamua tu kujijengea nidhamu binafsi ambayo hakuna mtu yeyote Yule anayekusimamia, sasa changamoto ya watu wengi wanapenda kuwa na nidhamu mpaka pale anaposimamiwa na watu wengine ndiyo anaweza kufanya kitu kwa ufanisi. Leo ni siku bora sana na ya kipekee kwetu tunakwenda kufanya makubwa na kutegemea kupata makubwa hivyo tunaalikwa sote kuweza kutumia vizuri zawadi ya siku hii ya leo kwani leo ni muda kwahiyo jali muda wako sana.

Mpendwa msomaji, napenda kutumia nafasi hii kukualika tena katika makala yetu ya leo ili tuweze kujifunza wote kwa pamoja mambo mazuri niliyoweza kukuandalia siku hii ya leo. Karibu sana mpenzi msomaji, nakusihi sana tuweze kusafiri pamoja mpaka pale mwisho wa kipindi chetu cha leo. Leo tutakwenda kujifunza jeshi muhimu unalopaswa kuliheshimu hapa duniani je wajua ni jeshi gani? Karibu tuweze kujifunza wote kwa pamoja.

SOMA;  Haya Ndiyo Mafanikio Ya Kwanza Unayopaswa Kuwa Nayo Katika Maisha Yako

Kila mtu huwa ana ndoto ya maisha yake ambayo anataka kuyafikia hapa duniani, kila mtu anatamani kufikia kiwango Fulani cha mafanikio,kwahiyo tunaweza kusema kila mtu anakiu yake au shauku yake juu ya ndoto yake hapa duniani. Kila mtu anataka kufanikiwa katika jambo Fulani, inategemeana na malengo ya mtu aliyejiwekea lakini mafanikio yetu yote yamegawanyika katika sehemu kuu tatu nazo ni kiakili, kiroho na kimwili.

Changamoto kubwa ni kwamba ndoto zetu zote haziwezi kukamilisha zenyewe bila kuwa na jeshi muhimu ambalo ni watu. Watu ni rasilimali moja ya rasilimali muhimu sana hapa duniani kwa sababu huwezi kutimiza ndoto zako bila watu, mafanikio yako yanategemea watu sana ili yaweze kukamilika. Kuna watu huwa wanajisemea eti wao ni jeshi la mtu mmoja lakini wanajidanganya wao wenyewe duniani hakuna jeshi la mtu mmoja. Kwa mfano, katika timu ya mpira hata wewe uwe mchezaji bora kiasi gani huwezi kucheza peke yako uwanjani lazima utawategemea wenzako ili uweze kuonesha ubora wako.

SOMA; Wafahamu Watu Wanaofanya Mambo Makubwa Duniani

Mpendwa msomaji, katika maisha yetu sisi binadamu tunahitaji watu ili tuweze kufanikiwa, kwahiyo,tunatakiwa tujenge mahusiano mazuri na watu, tuwaheshimu watu wanaotuzunguka bila kujali na kuweka vipmo vyovyote juu yao. Kila mtu ana nafasi yake hapa duniani usije hata siku moja kudharau watu waheshimu na wachukulie vile walivyo najua kila mmoja ana kilema chake yaani udhaifu wake lakini usimhukumu mtu kwa macho ya kibinadamu bali wewe kazana kujihukumu wewe mwenyewe kwanza.

Bila kuwa na mahusiano mazuri na watu ni ngumu kufikia ndoto zako, kama una toa huduma yoyote utahitaji watu wakuwapatia huduma yako na wala siyo miti, kwahiyo jenga mahusiano mazuri na watu waheshimu kwani kila mmoja ana umuhimu wake na kila mtu ana kitu chake cha kipekee hapa duniani ambacho mtu mwingine hana.

Hatua ya kuchukuaa leo, kujitegemea siyo kujitosheleza hivyo jenga mahusiano mazuri na watu na waheshimu wapende kama vile unavyojipenda wewe.

Kwahiyo, mpendwa msomaji, binadamu sisi ni viumbe wa kutegemeana na hakuna jeshi la mtu mmoja kila mtu anamtegemea mwenzake ili aweze kujitosheleza ndiyo nasema kujitegemea siyo kujitosheleza kwa kila kitu bado unahitaji watu ili kujitosheleza ili kufikia mafanikio makubwa kwenye maisha yako.

Nakutakia kila la heri rafiki yangu, na endelea kutembelea mtandao huu kujifunza kila siku na hivyo basi, usisahau kujiunga na mtandao wetu HAPA bila kusahau kupenda ukurusa wetu wa facebook. Asante sana na kuwa na siku bora yenye furaha na mafanikio makubwa.

Rafiki na mwalimu wako,

Deogratius Kessy

0717101505/0767101504 au barua pepe, deokessy.dk@gmail.com

Asante sana

 

Published by Deogratius Kessy

Mwandishi,mwalimu na mjasiriamali. Unaweza kutembelea Blog yake ya www.kessydeo.home.blog kujifunza zaidi na unaweza kuwasiliana naye kwa namba 0717101505/0767101504 au kwa barua pepe deokessy.dk@gmail.com

Leave a comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: