Habari za leo mpendwa rafiki na msomaji wa mtandao Kessy Deo? Ni matumaini yangu kuwa u buheri wa afya na unaendelea vema pia katika shughuli zako za kila siku. Hongera sana rfaiki kwa zawadi ya siku hii ya leo natumaini utautumia vema muda wako.
Mpendwa rafiki na msomaji, nipende kutumia nafasi hii kukualika tena katika kipindi chetu cha leo ili tuweze kujifunza wote kwa pamoja yale mazuri niliyoweza kukuandalia siku hii ya leo.
Kupitia makala yetu ya leo tutakwenda kujifunza umuhimu wa ufuatiliaji wa mipango yako. Tafadhali, karibu tusafiri pamoja mpaka pale tamati ya kipindi chetu cha leo.
Mara nyingi unapokuwa umepanga mipango yako unahitaji ufuatiliaji ili mambo yaweze kukamilika na mbinu wezeshi inayotumika katika kukamilisha mambo yako ni ufuatiliaji. Kama una jambo lako lolote huwezi kupata matokeo bora kama hutumii mbinu wezeshi ya kukusaidia kufanikiwa kwenye jambo lolote lile.
Kama una mifugo yako huna muda wa kufuatilia jua kabisa huwezi kupata matokeo bora katika mifugo yako. Kama una biashara huifuatilii ujue kabisa itapoteza mwelekeo wake tu. Biashara inahitaji ufuatiliaji wa karibu sana, hakuna jambo lolote litakaloweza kutokea kwenye maisha yako kama hujaamua kuchukua hatua ya kufuatilia.
SOMA; Huyu Ndiye Rafiki Muhimu Unayepaswa Kutembea Naye Katika Safari Ya Mafanikio
Kama una mtoto yuko shule anasoma basi hakikisha unatumia mbinu wezeshi ya kumfuatilia katika masomo yake. Mfuatilie mienendo yake na jua uimara na udhaifu wake uko wapi. Hakuna mtu mwenye muda ya kufuatilia mambo yako mpaka wewe mwenyewe uamue kufuatilia kwa ukaribu. Una mradi wako wowote basi tumia mbinu wezeshi ya kufuatilia kwa ukaribu mpaka kupata matokeo bora.
Mpendwa msomaji, kama unataka kufanikiwa katika mipango yako basi kuwa na mbinu wezeshi ya ufuatiliaji hatua kwa hatua. Usipofuatilia mambo yako hakuna mtu atakaye hangaika kufuatilia mambo yako, jitahidi kufuatilia mipango yako yote uliyojiwekea mpaka ufanikiwe bila kukata tamaa. Usipofuatilia maendeleo yako mwenyewe usitegemee kuna mtu atakuja kukusaidia kufuatilia kama wewe hujaamua kufuatilia kile unachotaka.
SOMA; Hawa Ndiyo Watu Wa Kuepuka Kuwasubiria Katika Maisha Yako
Hatua ya kuchukua leo, ili upate matokeo bora kwenye mambo yako basi weka juhudi ya kufuatilia, kama unamdai mtu hela basi tumia mbinu wezeshi ya kumfuatilia mpaka akulipe au una tafuta michango ya kitu Fulani basi wafuatilie watu kwa kuwakumbusha ili wakupatie michango kwani usipowafuatilia hutopata kile unachokitaka.
Kwahiyo, tumealikwa katika somo letu la leo kuwa kuna umuhimu mkubwa sana wa kufuatilia kila jambo ambalo tunataka litokee katika maisha yetu. Fuatilia chochote unachotaka utakipata lakini ukikaa kimya hutopata matokeo yoyote yale. Una mipango mingi uliyojiwekea hakikisha unaifuatilia mpaka uitekeleze. Anza kufuatilia ya kwako kwanza badala ya kufuatilia ya wengine.
Nakutakia utekelezaji mwema katika haya ulijifunza leo. Mshirikishe na wenzako ili naye aweze kupata maarifa haya kama wewe ulivyoyapata leo. Mshirikishe bila kuweka kipimo chochote juu yake na ili tuendelee kuwa karibu zaidi tafadhali jiunge na mtandao wetu HAPA. Lakini pia usisahu kupenda ukursa wetu wa facebook na kutembelea mtandao huu kila siku kwa makala za kujifunza.
Rafiki na mwalimu wako,
Deogratius Kessy
0717101505/0767101504
Asante sana