Design a site like this with WordPress.com
Get started

Wafahamu Watu Wenye Roho Ya Kaini Wanaoishi Kwenye Jamii Yetu

Habari ya leo mpendwa rafiki na msomaji wa mtandao wa Kessy Deo? Ni matumaini yangu kuwa  unaendelea salama kiafya bila kusahau katika shughuli za ujenzi wa taifa. Tunamshukuru Mungu kwa kuweza kutustahilisha tena siku hii ya leo ambapo mimi na wewe tumepata nafasi ya kuwasiliana tena na kuendelea kujifunza.

Mpendwa rafiki napenda kutumia nafasi hii kukuualika tena katika somo letu la leo tuweze kujifunza na kutafakari wote kwa pamoja. Ndugu,  nakusihi karibu tuweze kusafiri pamoja hadi tamati ya somo letu la leo. Karibu sana rafiki.

Image result for jealousy
ANGALIA HIYO PICHA HAPO JUU JINSI GANI WAKINA KAINI WANAVYOUMIA MIOYO YAO. ONA JINSI MIOYO YAO ILIVYOKUWA HAIPENDI KUONA WENZAO WAKIFURAHIA

Katika tafakari na somo letu la leo tutakwenda kujifunza somo lenye kichwa kinachosema, hawa ndiyo watu wenye roho ya Kaini. Mpendwa msomaji, dunia ya leo watu wamekumbwa na hali ya kuishi katika maisha ya chuki na wivu. Hili tunaliona hata katika familia zetu, ndugu, jamaa na marafiki ni namna gani chuki na wivu unavyoendelea kuwatafuna na kusambaratisha kabisa familia. Familia ngapi leo hii hazielewani kwa sababu ya wivu, na chuki? Watu wanaishi na roho ya kaini ndani ya mioyo yao na wala siyo ya  Abeli.

Mpendwa msomaji, waswahili wanasema nyumba usiyolala hujui hila yake,  kumbe basi, katika familia zetu kuna mambo mengi yanayofanyika na kuwapelekea watu kuishi maisha ya kutokuwa na furaha. Wengi wamekuwa wajane lakini bado wako na wenza wao, watoto wamekuwa yatima wakati bado wako na wazazi wao hii yote ni kwa sababu ya kukosa upendo na malezi bora.  Mpendwa msomaji, naposema watu wenye roho ya kaini ni wale watu wanaoishi katika hali ya wivu na chuki, hawa ni wale watu wanaoeneza na kuhubiri habari hasi na kufanya maisha ya watu kuwa ya visasi.

SOMA;  Muhimu; Kama Uko Kwenye Mahusiano Yoyote Usiache Kusoma Ujumbe Huu Wa Mt.Augustino

Mpendwa rafiki, katika familia zetu roho za kina kaini zinaendelea kuzaa mauti kwani siku zote chuki huzaa chuki na hatimaye mauti lakini upendo huzaa upendo. Ndugu msomaji, familia ambayo imejaa roho ya kaini ni familia hatari zinazosambaratisha mahusiano ya kiujirani, ndugu, jamaa na hata marafiki. Baba akiwa na roho ya kaini,mama akiwa na roho ya kaini , watoto nao watakuwa na roho hiyo hiyo ya kaini kwani mara nyingi mtoto anapokea kutoka kwa mzazi.

Mpendwa msomaji, sasa tukijaribu kuangalia kila idara ya maisha yetu tunaona ni jinsi gani roho huyu wa kaini anavyowamaliza watu na kuwatawala watu wakiishi na majeraha na mipasuko mikubwa katika maisha yao. Kwa mfano, watu wa roho ya kaini tuko nao makazini kwetu, ambao hawapendi kumuona mwenzao akifanikiwa hata kupandishwa cheo wakiona wenzao amepanda ngazi roho zinawauma na wengine wanadiriki kwenda hata kwa waganga wa kienyeji kwa sababu ya kutawaliwa na roho ya kaini.

Ndugu, kama uko kwenye roho hii ya kaini toka itakumaliza na utakufa ukiwa na maumivu moyoni. Siku hizi  tunaona hata kwenye baadhi ya nyumba zetu za ibada zinavyohubiri chuki badala ya upendo, watu wako katika nyumba za ibada lakini bado wanaonesheana vidole kila mmoja akijiona yeye ndiye anastahili kuliko wengine.

MUHIMU SANA KWAKO; Chanzo Kikuu Cha Wivu, Matokeo Yake Na Jinsi Ya Kuondokana Na Wivu.

Angalia hata katika marafiki waliosoma pamoja wanavyooneana wivu na kuwa na roho za chuki, utasikia, wakiambiana kauli kama hizi, iweje tusome wote wewe upate kazi na mimi nisipate kazi?, haya na wale walioko makazini roho ya kaini nayo inawatawala na kuwaumiza wakisema iweje wewe upandishwe cheo na mimi nisipandishwe cheo?, iweje wewe umekuja hapa kazini juzi juzi tu  bosi anakupenda wewe na kukupa madaraka?. Jamani roho ya kaini ambayo ni ya wivu na chuki ni roho mbaya sana ambayo chanzo chake kilianzia tangu hapo zamani kwa ndugu zetu wa mwanzo yaani kaini na abeli.

Mpendwa msomaji, napenda nikurudishe kidogo katika maandiko ya kitabu cha mwanzo ili tuweze kuona kisa cha kaini na abeli kilikuwaje, ndugu hawa wawili walizaliwa na adamu na hawa.  Baada ya ndugu hawa wawili kuzaliwa, baadaye  mmoja alikuwa ni mkulima na mwingine ni mfugaji, siku moja walialikwa kwenda kumtolea Mungu sadaka kama fungu lao la kumi. Sasa abeli sadaka yake ilimpendeza sana Mwenyezi Mungu kwani alitoa kwa moyo kwa kumtolea sadaka iliyonona sehemu ya mifugo yake.

Mpendwa msomaji, sasa kaini sadaka yake haikumpendeza Mungu kwani hakutoa kwa moyo na alitoa kisichonona. Hivyo roho ya wivu na chuki ndivyo ilivyoanzia hapo baada yaMungu kumtakabali Abeli kwahiyo, Kaini alipatwa na roho ya wivu na chuki na hatimaye aliishia kumuuwa ndugu yake kwani siku zote roho ya wivu na chuki huzaa mauti kama yalivyomkuta ndugu yetu Kaini kwa nduguye.

Hatua ya kuchukua leo, wivu na chukia  ni sumu mbaya inayosambaa kwa kasi katika jamii yetu. Ili tuiponye sumu hii ni watu kurudi katika kuishi maisha yanayompenda Mwenyezi Mungu na kufanya kazi kwa bidii na maarifa ili tuweze kupata kile tunachokitaka katika maisha yetu. Tukumbuke ya kwamba utayapata yote kama ukifahamu ya kuwa jukumu la maisha yako ni wewe wenyewe na siyo mtu mwingine.

Kwa kuhitimisha, somo letu la leo kupitia kisa cha Kaini na  nduguye tunaalikwa sisi sote tuweze kuishi maisha yanayompendeza Mungu na tuache kuishi na roho za visasi na wivu. Kwani visasi,chuki na wivu ndiyo kansa inayowatafuna watu wengi katika jamii yetu. Usimwonee mwezako wivu juu ya kitu Fulani bali weka juhudi na wewe utapata  kile unachokitaka.

Nakutakia utekelezaji mwema katika haya ulijifunza leo. Mshirikishe na wenzako ili naye aweze kupata maarifa haya kama wewe ulivyoyapata leo. Mshirikishe bila kuweka kipimo chochote juu yake na ili tuendelee kuwa karibu zaidi tafadhali jiunge na mtandao wetu HAPA. Lakini pia usisahu kupenda ukursa wetu wa facebook na kutembelea mtandao huu kila siku kwa makala za kujifunza.

Rafiki na mwalimu wako,

Deogratius Kessy

0717101505/0767101504

deokessy.dk@gmail.com

Asante sana

 

Published by Deogratius Kessy

Mwandishi,mwalimu na mjasiriamali. Unaweza kutembelea Blog yake ya www.kessydeo.home.blog kujifunza zaidi na unaweza kuwasiliana naye kwa namba 0717101505/0767101504 au kwa barua pepe deokessy.dk@gmail.com

Leave a comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: