Design a site like this with WordPress.com
Get started

Mambo Muhimu Unayoweza Kujifunza Kutoka Katika Kitabu Cha The Essentials Of Business Etiquette

Habari ya wakati huu mpendwa rafiki na msomaji wa mtandao wa Kessy Deo? ni matumaini yangu kuwa umeamka salama siku hii ya leo. Leo ni siku nyingine bora sana na ya kipekee kwetu hivyo tunaalikwa kumshukuru Mungu kwa zawadi ya siku hii ya leo. Rafiki, tumia muda wako vema kwa manufaa yako mwenyewe na dunia nzima.

Karibu sana rafiki katika makala yetu ya leo ambapo leo nitakwenda kukushirikisha mambo muhimu niliyojifunza katika uchambuzi wa kitabu. Nitakwenda kukushirikisha mambo machache kati ya mengi kupitia kitabu hiki. Karibu tuanze pamoja hadi tamati ya somo letu la leo. Kitabu hiki kimeandikwa na mwandishi Barbara Pachter.

Image result for the essentials of business etiquette pdf
Mambo 20 niliyojifunza katika kitabu cha The Essentials of Business etiquette na Barbara Pachter ni kama ifuatavyo;
1. Jina ni muhimu sana. Kila mtu ana jina lake na amepewa jina ili atambulike yeye ni nani. Jina linatambulisha biashara ya mtu. Jina linabeba biashara au kitu unachofanya.
Kama unamwita mtu jina lake mwite kiufasaha na siyo jina la utani. Mara nyingi pendelea kumuita mtu jina lake halisi ni bora zaidi kuliko jina la utani.

2. Wakati mwingine jina la mtu linaweza kuwa gumu hata kumpa mtu shida kulitamka. Kama unaona jina lako ni refu na gumu kutamka lifupishe. Pili kama jina lako la mwanzo ni rahisi kulika la mwisho basi tumia la mwanzo vivyo hivyo kwa la mwanzo kama ni gumu tumia la mwisho. Jina rahisi linarahisisha kuliko jina gumu kutamkwa.
3. Salamu ni kitu muhimu sana katika maisha ya binadamu. Salamu inalinda na kujenga uhusiano wa kijamii. Mtu akikusalimia unatakiwa umjibu na kumsalimu pia na siyo kukaa kimya. Vilevile angalia salamu unazomsalimia mtu je zinaendana kundi rika lake? Hivyo ni muhimu kuzingatia salamu.

4. Kama mfanyabiashara wa dunia ya leo unahitaji kuwa na kitu kinachoitwa kadi ya biashara. Kadi hii unatakiwa kujaza taarifa zako binafsi za muhimu kama vile wewe ni nani,anuani yako nk. Hii inakusaidia kujitangaza unapokuwa na kadi ya biashara kwani inakutambulisha wewe ni nani na taarifa zako zote muhimu ziko pale.

5. Dunia ya leo iko bize watu wako bize katika sehemu mbalimbali. Mitandao ya kijamii nayo inawafanya watu kupoteza umakini katika kazi au hata katika kumsikiliza mtu. Huwezi kuongea huku unasikiliza hivyo ni muhimu kuacha shughuli nyingine na kujitoa kumsikiliza mtu.

6. Mshukuru mtu anapokusaidia kuhusu jambo fulani. Mwandikie mtu asante hata kwa meseji kwa kujali jitihada zake za kukuandikia ujumbe. Toa asante au shukurani pale unaposaidiwa.

7. Unapoongea na mtu ongea kwa uso wa furaha siyo kwa kisirani. Lugha ya mwili nayo ni muhimu kama vile viashiria vya kichwa, mikono nk. Usiongee na mtu kwa kisirani bali onyesha shauku ya kuongea naye.

8. Unapoongea mbele ya kadamnasi ongea kwa sauti. Waangalie watu machoni yaani uso wako ungalie watu siyo unaongea na mtu halafu unaangalia pembeni. Mwangalie mtu machoni ili upate majibu sahihi wakati anaongea.

9. Jizuie kusema nadhani au nafikiria kitu fulani unapoongea na watu. Unapoulizwa swali lini utaenda kutembelea mbuga za wanyama usijibu nafikiria au nadhani badala yake sema nitaenda…. nadhani au nafikiria huwa inamaanisha hauko sahihi na kitu unachokisema hivyo ni vema kuwa makini.

10. Malumbano ya kujadili mambo ya siasa,dini katika sehemu ya kazi si mazuri. Malumbano ya siasa au dini yamejaa ushabiki ambao unaweza kuleta madhara makubwa sana kwa wateja lakini pia kuwakwaza watu wengine na hata wafanyakazi wenzako. Hivyo ni vema ukajaribu kuepuka mambo ya mijadala katika kazi inayoweza kuibua hisia mbalimbali.

11. Ni muhimu kuzingatia uvaaji kulingana na tukio.
Kama hujaenda kwenye tukio muulizie hata yule mwandaaji dressing code. Pili zingatia vivalio yaani accessories kama cheni,pete na saa. Kwa mwanaume na mwanamke kama mfanyabiashara saa ni muhimu kuwa nayo kwa ajili ya wakati na siyo kila muda kuangalia simu.

12. Kupata chakula pamoja na mteja au wateja wako ni njia mojawapo ya kujenga ukaribu na uhusiano mzuri. Lengo lako wewe siyo chakula bali lengo lako wewe linakuwa ni biashara. Kujenga ukaribu na uhusiano na watu ni njia kujenga mtandao. Na mtandao wa watu ulionao ndio watakaokuwezesha wewe kufika mbali. Wanasema ukitaka kwenda haraka nenda peke yako lakini ukitaka kwenda mbali zaidi nenda watu.

SOMA;  Zifahamu Aina Mbili (02) Za Wateja Katika Biashara Yako au Huduma Unayotoa

13. Ukiwa katika meza ya chakula jaribu kuwa mbali na simu. Weka mtetemo au ukimya ili usipate usumbufu na akili yako yote iwe kwenye chakula na uoneshe ushirikiano na wenzako mnapokuwa mezani mnakula. Tabia ya kula huku unashughulika na simu na mambo mengine siyo nzuri kabisa hivyo basi jiepuke.

14. Unapokuwa uko kwenye hotel unasubiria chakula baada ya kuagiza tumia muda huo kusoma kitabu. Unaweza kutumia fursa ya kusubiria katika kusoma kitabu.

15. Unapohudhuria katika sherehe fulani unatakiwa kuzingatia yafuatayo;
uvaaji,usinywe pombe kupita kiasi, usipost vitu hasi katika mtandao kuhusiana na tukio hilo. Toa asante kwa mwandaji wa shughuli.

16. Moja ya vitu unavyotakiwa kuwa makini navyo ni mitandao ya kijamii. Kuwa makini na habari unazokua unaandika. Epuka kuandika habari hasi juu ya kampuni fulani au mtu fulani. Pendelea kuandika vitu chanya na epuka kuandika mambo yanayoweza kuibua hisia za watu.

17. ombe kupita kiasi, usipost vitu hasi katika mtandao kuhusiana na tukio hilo. Toa asante kwa mwandaji wa shughuli.

16. Moja ya vitu unavyotakiwa kuwa makini navyo ni mitandao ya kijamii. Kuwa makini na habari unazokua unaandika. Epuka kuandika habari hasi juu ya kampuni fulani au mtu fulani. Pendelea kuandika vitu chanya na epuka kuandika mambo yanayoweza kuibua hisia za watu.

17. Epuka kuandika vifupi katika meseji. Unamtumia mtu ujumbe wenyewe vifupi inachukua muda wa kuelewa ni nini umekiandika pili itampatia mkanganyiko na kushindwa kujua lipi la kujibu na hivyo kumuacha njia panda. Hivyo ni vizuri kumtumia mtu ujumbe kamili kuliko vifupi. Mfano kuna ugonjwa wa vifupi umeingia kwasasa mtu anakutumia ujumbe xaxa akimaanisha sasa.

SOMA; Mambo Muhimu Unayoweza Kujifunza Kutoka Katika Kitabu Cha The 50 Cent

18. Epuka kuongea lugha ya mtaani au lugha ambayo siyo rasmi katika biashara na mazungumzo kazini. Pendelea kutumia lugha rasmi unapoongea na watu mambo ya biashara nk.

19. Inapotokea mtu anakupa pongezi juu ya kitu fulani pokea pongezi hiyo kwa kusema asante. Siyo vizuri mtu anakupa pongezi halafu unaikataa unamvunja nguvu hata yule aliyetumia nguvu na wake kukupongeza. Hivyo pokea pongezi

20. Katika maisha yetu huwa tunakuwa na mtu ambaye anakuhamasisha na kukuaminisha kuwa mambo yanawezekana na kufanya ndoto yako kuwa katika hali ya uhalisia. Mtu huyo ni role models au mentor natumaini kila mtu ana mtu anamvutia katika maisha yake na jinsi anavyofanya mambo katika jamii.

Nakutakia kila la heri rafiki katika haya uliyojifunza leo.
Rafiki na mwalimu wako,
Deogratius Kessy
0717101505/0767101504
deokessy.dk@gmail.com
Asante.

Published by Deogratius Kessy

Mwandishi,mwalimu na mjasiriamali. Unaweza kutembelea Blog yake ya www.kessydeo.home.blog kujifunza zaidi na unaweza kuwasiliana naye kwa namba 0717101505/0767101504 au kwa barua pepe deokessy.dk@gmail.com

Leave a comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: