Design a site like this with WordPress.com
Get started

Hawa Ndiyo Watu Wa Kuepuka Kuwasubiria Katika Maisha Yako

Habari ya leo mpendwa rafiki na msomaji wa mtandao wa Kessy Deo? Ni matumaini yangu kuwa uko salama rafiki na unaendelea vema na majukumu yako ya kila siku. Leo ni siku nyingine tena ya kipekee kwetu ambayo Mungu ametujalia sisi sote zawadi ya uhai hivyo rafiki,tunaalikwa kuutumia vizuri muda wetu wa leo. Hakikisha leo unafanya kitu cha kipekee kuweka kumbukumbu katika maisha yako.

Mpendwa msomaji, napenda kukukaribisha tena katika makala yetu ya leo ili tuweze kujifunza wote kwa pamoja kile nilichokuandalia tena siku hii ya leo. Nakusihi sana tuweze kusafiri pamoja katika makala yetu ya leo mpaka tamati ya somo letu la leo.

Image result for WAITING PEOPLE TO DO DUTY IS LOST YOUR DREAM

Katika dunia ya leo ukisubiria watu watakuangusha tu, ni wangapi leo hii wameweza kuangushwa na watu? Watu walitumia mbinu ya kukuahidi mambo mengi katika maisha yako lakini mpaka leo hii ni wangapi wametekeleza? Bado unaendelea kusibiria mpaka leo bila hata kujifunza kupitia makosa?

Mpendwa msomaji, ukitaka kufanya jambo Fulani na kutegemea watu waje wabadilishe maisha yako lazima utaangushwa tu na ndoto zako zitapotea kama mshumaa unavyopotea katika upepo. Kama unataka kitu chochote kitokee katika maisha yako basi ni wewe ndiyo utaweza kulifanya na siyo kuwasubiria watu waje wakutengenezee maisha yako.

SOMA; Muhimu; Usiache Kusoma Hapa Kama Bado Hujajua Kiu Yako Ni Nini

Watu wako bize na kufanya mambo yao hakuna mtu anayefikiria maisha yako zaidi ya wewe mwenyewe. Ukisubiria watu waje wabadilishe maisha yako utachelewa sana rafiki. Ili maisha yako uyabadilishe usiwasubirie watu waje kubadilisha maisha yako. Kama wewe hujachukua hatua ya kubadilisha maisha yako mwenyewe. Mtegemee wewe katika maisha yako ndiyo ataweza kutimiza ndoto zako.

Rafiki, kama unawasubiria watu waje wabadilishe maisha yako watakuangusha, kama unasubiria watu waje ili utimize ndoto zako jua kabisa watakuangusha pia. Ukijiwekea juhudi katika maisha yako mwenyewe kutafuta kile unachotaka utakipata rafiki lakini ukiendelea kusubiria watu watakuangusha bure. Hakuna mtu au kiongozi serikalini anakosa usingizi kwa sababu ya kukufikria wewe. Endelea kuweka juhudi bila kusahau kumtegemea Mungu kwani binadamu watakuangusha tu.

Hatua ya kuchukua leo, usiwasubirie watu waje kukufanyia kile unachotaka kwenye maisha yako. Bali inuka wewe mwenyewe na kafanye kile unachotaka kwenye maisha yako. Ukiwasubiria watu watakuangusha na kukuchelewesha kutimiza ndoto zako hapa duniani.

Mwisho, kuwasubiria watu waje wabadilishe maisha yako ni kupoteza muda rafiki. Fanya kile unachojua bila kusubiria ruhusa na baadaye utafika mbali sana. usikubali mtu akukatishe tamaa kwani wewe ni mshindi na bado uko hai utaweza kutimiza ndoto zako kama utapambana kuzitimiza.

MUHIMU;  Mambo Muhimu Unayoweza Kujifunza Kutoka Katika Kitabu Cha You Were Born Rich

Nakutakia utekelezaji mwema katika haya uliyojifunza leo. Mshirikishe na wenzako ili naye aweze kupata maarifa haya kama wewe ulivyoyapata leo. Mshirikishe bila kuweka kipimo chochote juu yake na ili tuendelee kuwa karibu zaidi tafadhali jiunge na mtandao wetu HAPA. Lakini pia usisahu kupenda ukursa wetu wa facebook na kutembelea mtandao huu kila siku kwa makala za kujifunza.

Rafiki na mwalimu wako,

Deogratius Kessy

0717101505/0767101504

deokessy.dk@gmail.com

Asante sana

 

Published by Deogratius Kessy

Mwandishi,mwalimu na mjasiriamali. Unaweza kutembelea Blog yake ya www.kessydeo.home.blog kujifunza zaidi na unaweza kuwasiliana naye kwa namba 0717101505/0767101504 au kwa barua pepe deokessy.dk@gmail.com

Leave a comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: