Habari ya leo mpendwa rafiki na msomaji wa mtandao wa Kessy Deo? Ni matumaini yangu kuwa uko salama siku hii ya leo hivyo leo ni nafasi nyingine ya kipekee sana kwetu kwenda kuweka juhudi katika kile unachokifanya. Hongera sana rafiki kwa zawadi ya siku hii ya leo katika maisha yako kwahiyo, tunaalikwa kumshukuru Mungu kwa kuweza kutustahilisha tena siku hii ya leo.
BONYEZA HAPA KUPATA KITABU CHA KUJISOMEA
Mpendwa rafiki, napenda kuchukua nafasi hii kukualika tena katika makala yetu ya leo ili tuweze kujifunza wote kwa pamoja mambo muhimu niliyoweza kukuandalia siku hii ya leo. Karibu sana mpenzi msomaji tusafiri pamoja mpaka pale tamati ya somo letu la leo.
Katika makala yetu ya leo tutakwenda kujifunza wote kwa pamoja faida za kumpa mtu nafasi ya kukosea. Muda mwingine unapaswa kumpa mtu nafasi ya kukosea katika jambo Fulani kwanini umpe nafasi ya kukosea ? ndiyo ukimpa nafasi ya kukosea atajifunza kupitia makosa aliyofanya.
Inawezekana hapo ulipo kuna watu wako wa karibu unawaelekeza jambo Fulani sahihi lakini hawataki kukusikiliza kile unachowaambia na kuona kile wanachofanya ndiyo sahihi kumbe siyo sahihi. Sasa ukimwacha akosee atajifunza na atakuja kukuheshimu tu kwa kile ulichomwambia hivyo huhitaji kumlazimisha mtu kufanya kitu sahihi bali mpe nafasi ya kukosea atajifunza.
Unaweza kutumia mbinu katika mambo mengi kwa mfano, unamwambia mwanafunzi asome kwa bidii halafu hataki kukusikia mwache akosee halafu ndiyo atapata picha ya kile ulichokuwa unamwambia ni sahihi. Rafiki, binadamu ni watu wagumu sana kubadilika unaweza ukampa mbinu mbalimbali katika maisha yake akadharau na baadaye anakuja kukosea sasa akikosea ndiyo atajifunza na kuweka heshima.
SOMA; Kitu Muhimu Kinachojenga Mahusiano Yetu
Tunapewa ushauri elekezi kutoka kwa matabibu wetu wa afya juu ya ulaji mzuri lakini watu hawasikii usiwalazimishe waache wakosee ndiyo watajifunza. Kuna msemo mmoja wa waswahili unasema mtoto akilia wewe mpe akijikata atajifunza. Inawezekana unawaelezea watu umuhimu wa kujali afya zao lakini hawasikii waaache wakosee wakishapata shida katika afya yao watakuja kujua umuhimu wa kutunza afya zao.
Watu wanahubiriwa umuhimu wa kujali muda katika maisha yao lakini hawaoni umuhimu waache wakosee watakuja kuona umuhimu wake. Utajisumbua sana kumbadilisha mtu kama hataki kubadilika. Mtu anaamua kubadilika kwa uamuzi wake mwenyewe na hiyari yake mwenye na wala siyo kulazimishwa.
SOMA; Hii Ndio Mbinu Bora Ya Kumsaidia Mtu Ambaye Hajui Kwenda Na Muda Kwenye Maisha Yake
Hatua ya kuchukua leo, usiwalazimishe watu juu ya jambo Fulani, bali wewe wape nafasi ya kukosea watakuja kujifunza kupitia makosa yao. Kumlazimisha binadamu abadilike ni sawa na kuhamisha maji baharini. Binadmu wana asili ya ukaidi pale wanapoambiwa kitu. Wewe mwambie mtu ukweli yeye ndiyo ataamua kubadilika au kubaki kama vile alivyo mwachie kazi hiyo ya kubadilika, wewe timiza wajibu wako tu .
Mwisho, muda mwingine unatakiwa kuwapa watu nafasi ya kukosea ili waweze kujifunza kwa kile walichokuwa wanaambiwa ni sahihi kufanya katika maisha yao. Waalimishe watu juu ya kitu Fulani lakini usiwalazimishe kuchukua hatua juu ya jambo hilo. Kuwalazimsha ni sawa na kuhamisha maji baharini na utapoteza wakati wako bure.
Nakutakia utekelezaji mwema katika haya uliyojifunza leo. Mshirikishe na wenzako ili naye aweze kupata maarifa haya kama wewe ulivyoyapata leo. Mshirikishe bila kuweka kipimo chochote juu yake na ili tuendelee kuwa karibu zaidi tafadhali jiunge na mtandao wetu HAPA. Lakini pia usisahu kupenda ukursa wetu wa facebook na kutembelea mtandao huu kila siku kwa makala za kujifunza.
Rafiki na mwalimu wako,
Deogratius Kessy
0717101505/0767101504
Asante sana