Design a site like this with WordPress.com
Get started

Hivi Ndivyo Unavyoweza Kusafiri Nchi Nyingi Duniani

Habari mpendwa rafiki na msomaji wa mtandao wa Kessy Deo? Ni matumaini yangu kuwa uko salama rafiki na unaendelea kuwajibika katika majukumu yako. Hongera sana rafiki kwa zawadi ya siku hii ya leo hivyo tunaalikwa kumshukuru Mungu kwa zawadi ya uhai. Leo ni tarehe moja ya mwezi wa pili mwaka elfu mbili na kumi na saba(2/1/2017) hivyo mpendwa rafiki, napenda kutumia nafasi hii kukutakia heri ya mwezi mpya wa pili. Mwezi mmoja sasa umepita tangu tuanze mwaka mpya.

Image result for happy new month images

Rafiki, muda ni mali usikubali kuupoteza bure jaribu kufanya kitu kwa ajili ya kuukomboa wakati wako kuliko kukaa bure waswahili wanasema mkaa bure si sawa na mtembea bure. Mpendwa msomaji, nipende kutumia nafasi hii kukukaribisha tena katika makala yetu ya leo tuweze kujifunza wote kwa pamoja.

Katika makala yetu ya leo tutakwenda kujifunza jinsi unavyoweza kusafiri nchi nyingi duniani. Kwahiyo, nakualika tuweze kusafiri pamoja mpaka tamati ya somo letu nililokuandalia leo. Karibu sana rafiki yangu tujifunze wote kwa pamoja.

Mpendwa rafiki, shauku yako leo nikutaka kujua unawezaje kusafiri nyingi duniani? Rafiki, njia nzuri unayoweza kuitumia kusafiri nchi nyingi duniani ukiwa umekaa hapo hapo ulipo ni kwa njia ya kusoma vitabu au kwa njia ya kujifunza. Katika kujifunza kwangu kupitia kusoma vitabu mbalimbali na watu waliofanikiwa na wenye maarifa mpaka sasa nimeweza kusafiri nyingi duniani. Kwahiyo, nimeona ni vema rafiki nikushirikishe na wewe mbinu hii ya kusoma vitabu utashangaa unasafiri nchi duniani bila hata kutegemea.

SOMA;  Hivi Ndivyo Unavyoweza Kutumika Kama Baraka Kuendeleza Duniani

Mpendwa msomaji, unapaswa kujifunza kuijuwa vizuri nchi au sehemu mbalimbali unazotaka kwenda vizuri kabla ya kufika sehemu husika. Utawezaje kuzijua sehemu mbalimbali na mambo mbalimbali duniani? Ni kwa njia ya kujifunza,kupitia kusoma vitabu mbalimbali vinavyoelezea mambo husika. Kama unataka kwenda marekani tafuta vitabu vinavyoelezea nchi ya marekani, soma maandiko mbalimbali ya waandishi tofauti tofauti utajifunza vitu vingi sana.

Rafiki, inawezekana wewe ni Mtanzania lakini hujui vizuri historia ya nchi yako na mambo mengi yaliyoko Tanzania. Kujifunza hakuna mwisho,endelea kusafiri nchi nyingi utakavyo kupitia kusoma. Utajifunza tamaduni za maisha yao, shughuli za kiuchumi na siri nyingine mbalimbali walizotumia wenzetu hatimaye kupiga hatua kimaendeleo. Usipojifunza utaishia kusafiri ndani ya mkoa, wilaya na hutoweza kuzifikia nchi nyingi duniani bila kuthubutu kujifunza. Huwezi kujua mambo mengi kama hutochukua jukumu la kujifunza.

SOMA;  Mambo Muhimu Unayoweza Kujifunza Kutoka Katika Kitabu Cha Emotional intelligence work

Rafiki, huwezi kusafiri mbali kiimani kama wewe hutaki kujifunza mambo, maandiko mbalimbali ya kiimani. Kuna vitabu vya kiimani chukua soma utajifunza mambo mengi uliyokuwa huyajui utashangaa unasafiri mbali sana kiimani.

Hatua ya kuchukua leo, amua leo kuchukua hatua ya kujifunza ili uweze kusafiri nchi mbalimbali duniani. Soma vitabu ili uweze kupata maarifa mbalimbali. Jifunze sana kwani jinsi unavyojifunza utajigundua kuwa hujui mambo mengi. Unayeridhika na maarifa ni dalili tosha ya kuanguka. Kama hujui wapi utapata vitabu vya kusoma tafadhali wasiliana na mimi kupitia namba hii 0717101505 utaweza kupata vitabu na pia tunaakualika katika klabu yetu ya kusoma vitabu viwili kwa wiki.

Kwa kuhitimisha, elimu haina mwisho. Kujifunza kila siku iwe ni kama mfumo wa maisha yako vile. Kama unavyokula kila siku na wewe jifunze hivyo hivyo, usipojifunza utashangaa wenzako wanajua mambo mengi wewe unaendelea kujivunia na elimu uliyonayo ya darasani wenzako wakiendelea kutanua wigo wa maarifa mbalimbali. Siri ya kujua mambo ni kujifunza.

Nakutakia utekelezaji mwema katika haya uliyojifunza leo. Mshirikishe na wenzako ili naye aweze kupata maarifa haya kama wewe ulivyoyapata leo. Mshirikishe bila kuweka kipimo chochote juu yake na ili tuendelee kuwa karibu zaidi tafadhali jiunge na mtandao wetu HAPA. Lakini pia usisahu kupenda ukursa wetu wa facebook na kutembelea mtandao huu kila siku kwa makala za kujifunza.

Rafiki na mwalimu wako,

Deogratius Kessy

0717101505/0767101504

deokessy.dk@gmail.com

Asante sana

 

Published by Deogratius Kessy

Mwandishi,mwalimu na mjasiriamali. Unaweza kutembelea Blog yake ya www.kessydeo.home.blog kujifunza zaidi na unaweza kuwasiliana naye kwa namba 0717101505/0767101504 au kwa barua pepe deokessy.dk@gmail.com

Leave a comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: