Design a site like this with WordPress.com
Get started

Kitu Muhimu Kinachojenga Mahusiano Yetu

Habari ya leo mpendwa rafiki na msomaji wa mtandao wa Kessy Deo? Ni matumaini yangu kuwa uliamka salama siku hii ya leo. Hongera pia rafiki yangu kwa zawadi ya siku hii ya leo kwahiyo, tunaalikwa sisi sote kumshukuru Mungu tulioweza kustahilishwa kuvuta pumzi tena siku ya leo. Ni vema basi, tuitumie vizuri zawadi yetu ya leo tuliyopewa katika hali chanya na siyo hasi.

Image result for trust relationship quotes

Mpendwa rafiki, napenda kutumia nafasi hii kukualika tena katika makala yetu ya leo tuweze kujifunza wote kwa pamoja yale mambo mazuri niliyoweza kukuandalia siku hii ya leo. Leo ndiyo siku ya mwisho ya mwezi wa kwanza na tumebakiza miezi kumi na moja tu hivyo rafiki siku zinakimbia na kama hujaamua kuchukua hatua siku zinaenda na wewe ukiendelea kubaki hapo hapo ulipo. Jenga nidhamu ya kupitia mambo yako kwa uaminifu na tembea na rafiki yako wa utekelezaji kila siku utaweza kufika pale unapopataka.

Mpendwa msomaji, katika somo letu la leo tutakwenda kujifunza wote kwa pamoja kitu muhimu kinachojenga uhusiano wetu. Je ni kitu gani hiko kinachojenga uhusiano wetu? Karibu tusafiri pamoja mpaka tamati ya makala yetu ili uweze kujua nilichokuandalia siku hii ya leo.

Mpendwa msomaji, kila binadamu ambaye amezaliwa na mwanamke basi yuko katika mahusiano. Mtu mwingine akisikia mahusiano basi moja kwa moja anafikiria mahusiano ya kimapenzi. Kuna mahusiano ya kifamilia, ndugu, wenza, marafiki, jamaa nakadhalika. Kumbe basi, binadamu sisi asili au chimbuko letu linatokana na mahusiano kulingana na vinasaba tulivyokuwa navyo.

SOMA;Jambo Linaloleta Mpasuko Katika Familia

Mpendwa rafiki na msomaji wa mtandao Kessy Deo, malengo mahususi ya somo letu la leo ni kufahamu kitu muhimu kinachojenga uhusiano wetu. Kitu kinachojenga uhusiano wetu ni uaminifu. Uhusiano unajengwa kwenye uaminifu au wakoloni wanasema hivi relathionship is build on trust.

 Ndugu msomaji, licha ya uhusiano kujengwa kwenye uaminifu habari njema ni kwamba uaminifu unajengwa penye uhakika. Mpenzi msomaji, ni nani kati yetu anaweza kujenga uhusiano mahali ambapo hakuna uhakika? Hata wateja katika biashara, wanajenga uhusiano kwenye uhakika. Sehemu ambayo inatoa huduma bora basi mteja atajenga uhusiano bora. Katika mahusiano yako hakikisha unakuwa na uhakika ili uweze kujenga uhusiano imara.

SOMA; Muhimu; Kama Uko Kwenye Mahusiano Yoyote Usiache Kusoma Ujumbe Huu Wa Mt.Augustino

Hatua ya kuchukua leo, leo umejifunza ya kuwa uhusiano unajengwa na uaminifu, hivyo jifunze kuwa mwaminifu kwenye kila idara ya maisha yako. Uaminifu unalipa katika karni hii na ni bidhaa adimu sana kupatikana. Pia katika mahusiano yako iwe ya kibiashara, kiimani,kimapenzi,siasa yaani kila idara hakikisha unakuwa na kitu muhimu nacho ni uhakika. Kumbuka kuwa uaminifu unajengwa penye uhakika.

Kwa kuhitimisha, katika somo letu la leo tumeweza kualikwa sisi sote kuwa uhusiano unajengwa kwenye uaminifu. Hakuna mtu atakayejenga uhusiano na mtu ambaye si mwaminifu. Lakini kumbuka ya kwamba uaminifu wenyewe unajengwa penye uhakika. Uhakika ni imani chanya anayofikiria mtu kuipata kutoka sehemu Fulani. Uhakika ndiyo thamani ya pekee watu wanayoitafuta katika huduma unayotoa.

Nakutakia utekelezaji mwema katika haya ulijifunza leo. Mshirikishe na wenzako ili naye aweze kupata maarifa haya  kama wewe ulivyoyapata leo. Mshirikishe bila kuweka kipimo chochote juu yake na ili tuendelee kuwa karibu zaidi tafadhali jiunge na mtandao wetu HAPA. Lakini pia usisahu kupenda ukursa wetu wa facebook na kutembelea mtandao huu kila siku kwa makala za kujifunza.

Rafiki na mwalimu wako,

Deogratius Kessy

0717101505/0767101504

deokessy.dk@gmail.com

Asante sana

 

Published by Deogratius Kessy

Mwandishi,mwalimu na mjasiriamali. Unaweza kutembelea Blog yake ya www.kessydeo.home.blog kujifunza zaidi na unaweza kuwasiliana naye kwa namba 0717101505/0767101504 au kwa barua pepe deokessy.dk@gmail.com

Leave a comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: