Design a site like this with WordPress.com
Get started

Ifahamu Thamani Ya Binadamu Unayopaswa Kuwa Nayo

Habari ya leo mpendwa rafiki na msomaji wa mtandao wa Kessy Deo? Ni matumaini yangu kuwa umeamka salama na umeinza siku yako kwa hamasa ya kufanya kilicho bora na kupata matokeo bora. Hongera pia, kwa zawadi ya siku hii ya leo kama falsafa yetu ya kila siku kwa wanafanikio ni kutumia muda wetu vizuri kila siku kwa mambo chanya yanayoleta athari chanya katika maisha yetu na siyo athari hasi.

whatsapp-image-2016-09-30-at-16-29-22BONYEZA HAPA KUPATA KITABU CHA FUNGA NDOA NA UTAJIRI

Mpendwa msomaji, nipende kutumia fursa hii kukualika tena katika makala yetu ya leo ili tuweze kujifunza wote kwa pamoja. karibu sana rafiki na tuambatane wote kwa pamoja mpaka mwisho wa somo letu la leo.

Katika makala yetu ya jana tulijifunza somo zuri sana ambalo linamhusu mtu yeyote Yule ambaye yuko katika mahusiano. Na habari njema ni kwamba hakuna binadamu ambaye hayuko katika mahusiano hivyo basi, kama hukupata nafasi ya kuisoma basi usijali rafiki bonyeza HAPA kuweza kuisoma makala ya jana.

Mpendwa msomaji, katika makala yetu ya leo tutakwenda kujifunza kitu muhimu sana ambacho unapaswa kuwa nacho kwenye maisha yako. Je ni kitu gani hicho? Tuendelee kuwa pamoja mpaka mwisho wa darasa letu utaweza kujua ni kitu gani.

Katika hali ya kawaida kabisa katika dunia ya leo kama huna thamani yoyote ile unayotoa utaonekana huna maana yoyote ile. Hivyo basi, rafiki, katika maisha yako jitahidi sana uweze kuwa na thamani yoyote ile unayotoa la sivyo kama huna chochote unachotoa kwa wengine ni fedhea kubwa.

Mpendwa rafiki, thamani ya mtu ni kitu, kama huna kitu chochote hata wale watu wa karibu kwako watakudharau tu. Hivyo ni vema ujitahidi hata uwe na kitu chochote ambacho hata kama ni kidogo utajivunia una kitu Fulani. Utajivunia una thamani Fulani unayoitoa. Kama huna kitu watu watakudharau hivyo endelea kuweka juhudi kubwa ili  uweze kuwa na kitu ambacho kitaonesha thamani yako hata kama ni kidogo.

SOMA; Jipe Nafasi Hii Muhimu Kwenye Maisha Yako

Mpendwa msomaji, kumbuka ya kuwa aliyenacho atazidi kuongezewa hivyo jitahidi kuwa na kitu ili uweze kuongezewa katika maisha yako. Usipokuwa na kitu watu watakuwa wanakupa upendo kwa vipimo vyao wao wenyewe. Mtakatifu Augustino aliwahi kusema, kipimo cha upendo ni kupenda bila kipimo lakini binadamu wengi wanapima upendo kulingana kitu ambacho anacho mtu na siyo ule upendo wa kutoka moyoni.

Rafiki, usipokuwa na kitu duniani utadharaulika huo ndio ukweli bora kuwa na kitu hata kama ni kidogo lakini ni cha kwa kwako.  Waswahili wanasema, mkono mtupu haulambwi hivyo basi jitahidi angalau na wewe mkono wako uwe na kitu ili uweze kujenga heshima.

Hatua ya kuchukua leo, jitahidi kuwa na thamani yoyote ile unayotoa kwa wengine. Thamani yako itaonekana pale unapotoa kitu ndio maana tunasema thamani ya mtu ni kitu. Kama huna kitu ni fedhea kubwa itakayokufanya uendelee kuona dunia si sehemu salama kuishi.

Mpendwa msomaji, kila mmoja wetu anaalikwa kuwa  na kitu au thamani anayotoa kwa wengine. usipokuwa na  thamani yoyote unayotoa hapa duniani au kuwa na kitu chochote utaendelea kudharaulika na binadamu watakuwa wanakupima kulingana na thamani yako.

SOMA KALI NYINGINE; Mambo Muhimu Unayoweza Kujifunza Kutoka Katika Kitabu Cha The 50 Cent

Nakutakia utekelezaji mwema katika haya ulijifunza leo. Mshirikishe na wenzako ili naye aweze kupata maarifa haya  kama wewe ulivyoyapata leo. Mshirikishe bila kuweka kipimo chochote juu yake na ili tuendelee kuwa karibu zaidi tafadhali jiunge na mtandao wetu HAPA. Lakini pia usisahu kupenda ukursa wetu wa facebook na kutembelea mtandao huu kila siku kwa makala za kujifunza.

Rafiki na mwalimu wako,

Deogratius Kessy

0717101505/0767101504

deokessy.dk@gmail.com

Asante sana

 

Published by Deogratius Kessy

Mwandishi,mwalimu na mjasiriamali. Unaweza kutembelea Blog yake ya www.kessydeo.home.blog kujifunza zaidi na unaweza kuwasiliana naye kwa namba 0717101505/0767101504 au kwa barua pepe deokessy.dk@gmail.com

Leave a comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: