Design a site like this with WordPress.com
Get started

Muhimu; Kama Uko Kwenye Mahusiano Yoyote Usiache Kusoma Ujumbe Huu Wa Mt.Augustino

Habari mpendwa rafiki na msomaji wa mtandao wa Kessy Deo? Ni matumaini yangu kuwa uko salama na umekuwa na mwisho mzuri wa juma. Katika mwisho huu wa juma ndugu rafiki ni fursa nzuri kwako kuweza kutenga muda wa kuongea na wewe binafsi lakini pia, kupitia wiki yako nzima ilikwendaje. Unapofanya tathimini unakuwa unapata matokeo ya jumla ni sehemu gani umefanya vema na wapi umefanya vibaya.

Kwahiyo, baada ya kufaya tathimini utapata matokeo ni sehemu gani uko imara na sehemu gani kuna udhaifu. Hivyo unapokwenda  kuianza wiki ya kesho unajua ni mambo gani unatakiwa kuyaboresha ili usifanye makosa tena. Ni muhimu pia kujifunza kupitia makosa tunayofanya kila siku badala ya kulaumu na kulalamika.

Rafiki, nipende kutumia nafasi hii kukualika tena katika makala yetu ya leo ili tuweze kujifunza wote kwa pamoja. Hivyo basi, karibu mpenzi msomaji tuweze kusafiri kwa pamoja katika somo letu la leo. Katika somo letu la leo tutakwenda kujifunza kuhusiana na kipimo cha upendo wetu ni nini? Karibu tujifunze rafiki.

Image result for love without measure

Mtakatifu Agustino enzi za uhai wake hapa duniani aliwahi kusema hivi ‘’kipimo cha upendo ni kupenda bila kipimo’’ kumbe basi, kipimo cha upendo wetu sisi binadamu ni kupenda bila kipimo. Je ni wangapi miongoni mwetu tumekuwa tunawapenda watu kulingana na vipimo unavyojichukulia sisi wenyewe.

SOMA; Mambo Muhimu Ya Mahusiano Niliyojifunza Katika Kitabu Cha Happier Marriage

Tunabaguana na kuwekana katika makundi mbalimbali kwa sababu ya kupenda wenzetu kwa vipimo vya vitu Fulani. Yule mtu mwenye kitu Fulani ndiyo unapaswa kumuonyesha upendo kwa sababu ya kipimo ulichojiwekea wewe mwenyewe. Haya tunayaona hata katika familia zetu kipimo cha upendo kinaonekana kulingana na thamani ya mtu huyo katika familia. Kwa mfano, mtoto anaye faulu darasani ataonekana kupendwa zaidi na mzazi kwa sababu amemwekea vipimo na shule ambaye hana akili za darasani ataonekana si kitu vivyo hivyo hata katika swala la kiuchumi Yule ambaye yuko vizuri kiuchumi basi ndio atapewa upendo zaidi.

Mpendwa msomaji, katika jamii zetu kunatokea mipasuko ya kila aina yote hii ni kwa sababu watu wamejiwekea wao wenyewe vipimo katika falsafa ya upendo. Falsafa ya upendo huwa haibagui kabisa ila sisi binadamu ndiyo tunaweka vipimo vyetu sisi wenyemwe. Kumbe binadamu ndiyo mtu anayekwenda kinyume na falsafa ya upendo kwa kujiwekea vipimo yeye mwenyewe.

soma; Ujumbe Muhimu Kwako Kutoka Kwa Bilionea Richard Branson

Wale watu tuliokuwa nao sasa tunapaswa kuwapenda bila ya kuweka vipimo. Tunasahau ya kwamba upendo huvumilia yote na wala haubagui kama ni hivyo kwanini sisi binadamu tunaendelea kutafutwa na ubinafsi katika maisha yetu? Tunatafutwa na ubinafsi kwa sababu ya kujiwekea vipimo katika upendo.

Hatua ya kuchukua, ondoa vipimo katika upendo na wapende watu wote kwa kufuata misingi na falsafa ya upendo. Tuishi katika kanuni ya dhahabu ambayo inasema mtendee mwenzako kama vile unavyotaka kutendewa wewe na kumbuka ya kwamba kipimo cha upendo ni kupenda bila kipimo. Shinda ubinafsi kwa kwa kupenda bila kipimo.

Mpendwa msomaji, mtakatifu Agustino ametualika sisi sote kuweza kujitafakari katika maisha yetu kuwa kipimo cha upendo ni kupenda bila kipimo. Kumbe basi, katika maisha yetu tunapaswa kuwapenda wenzetu bila kuwawekea vipimo. Tunaalikwa pia kuishi katika misingi ya falsafa ya upendo na tuweze kushinda ubinafsi wetu.

Nakutakia utekelezaji mwema katika haya ulijifunza leo. Mshirikishe na wenzako ili naye aweze kupata maarifa haya  kama wewe ulivyoyapata leo. Mshirikishe bila kuweka kipimo chochote juu yake na ili tuendelee kuwa karibu zaidi tafadhali jiunge na mtandao wetu HAPA. Lakini pia usisahu kupenda ukursa wetu wa facebook na kutembelea mtandao huu kila siku kwa makala za kujifunza.

Rafiki na mwalimu wako,

Deogratius Kessy

0717101505/0767101504

deokessy.dk@gmail.com

Asante sana

Published by Deogratius Kessy

Mwandishi,mwalimu na mjasiriamali. Unaweza kutembelea Blog yake ya www.kessydeo.home.blog kujifunza zaidi na unaweza kuwasiliana naye kwa namba 0717101505/0767101504 au kwa barua pepe deokessy.dk@gmail.com

Join the Conversation

2 Comments

Leave a comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: