Design a site like this with WordPress.com
Get started

Jipe Nafasi Hii Muhimu Kwenye Maisha Yako

Habari ya wakati huu mpendwa rafiki na msomaji wa mtandao wa Kessy Deo? Ni imani yangu kuwa uko salama na unaendelea vizuri kutimiza wajibu wako wa kila siku kwenye maisha yako. Hongera sana rafiki kwa zawadi ya maisha uliyoweza kuipata siku hii ya leo na amini wewe ni mwanamafanikio hivyo huwezi kuacha muda au siku yako iende bure tu bila kuthubutu kutenda jambo chanya.

Jana tulijifunza jinsi ya kushinda kuahirisha mambo na kama hukupata nafasi ya kusoma jana isome HAPA hiyo makala halafu uendelee na makala ya leo.  Basi mpendwa msomaji, nitumie nafasi hii kukualika katika makala yetu ya leo na hongera pia kama ulisoma makala ya jana ambayo nimekuwekea link hapo juu.

Rafiki, leo napenda kukushirikisha kitu kimoja muhimu sana kwenye maisha yako ambacho ni kujipa nafasi moja muhimu kwenye maisha yako ambayo nafasi hiyo ni kujaribu kuthubutu kwenye mambo ambayo unasita kuyafanya kila siku. Usiogope kuhoji pale panapowezekena kuhoji na usikubali kitu chochote kifanyike katika maisha yako bila kuhoji usikubali kuendeshwa wakati kuna nafasi ya kujaribu kuthubutu au kuhoji juu ya kitu hiko.

SOMA; Ujumbe Muhimu Kwako Kutoka Kwa Bilionea Richard Branson

Mpendwa msomaji, kuna mambo mengi sana yanatokea katika maisha na tunashindwa kuthubutu hata kuhoji kwanini kimetokea. Wengine wanakubali kuteswa hata sehemu zao za kazi kwa kuogopa kuhoji hata kama ni haki yake mwenyewe kwa kuhofia kufukuzwa kazi au kupoteza kazi yake. Hivyo unakuta watu wanaishi katika minyororo ambayo wamejichangulia wao kuishi hapa duniani na anashindwa kuhoji kwanini hali Fulani inamtokea katika maisha yake.

Ndugu rafiki, huhitaji mtaji kuthubutu kusema jambo ambalo linakuumiza katika maisha yako. Wengine wanakubali kuendelea kuteseka na maumivu moyoni na mtu anayemuumiza anamuona na anashindwa kuthubutu kumwambia ukweli. Usikubali kukaa na kitu moyoni bali jipe nafasi ya kuthubutu kupata suluhisho sahihi.

Mpendwa msomaji, haitoshi kuendelea kulalamika kwa watu wengine kuwa mwenza wako anakutendea ndivyo sivyo kwenye maisha yenu ya ndoa wakati unaweza ukajipa nafasi ya kuthubutu kumwambia ukweli leo. Kuthubutu kufanya jambo ambalo huku wahi kulifanya ni kama kuondoa laana katika maisha yako.

SOMA; Ujumbe Muhimu Sana Kwako Kutoka Kwa Papa Francis

Hatua ya kuchukua leo, nenda leo kaondoe laana kwa kuthubutu kufanya lile jambo ambalo linakuumiza au kukukera katika maisha yako. Kama ulikuwa hujawahi kujifunza maarifa mapya tofauti na elimu yako ya darasani embu leo thubutu kuondoa laana hiyo kwa kuanza kusoma au kujifunza maarifa mapya.

Kama wewe uliwahi kumwambia mwenzako hutomsamehe na hata ukifa asije kukuzika unaweza kuvunja laana hiyo leo kwa kuthubutu kumsamehe na kuondoa uchungu wote ulioumbika ndani ya moyo. Kwanini uendelee kumbeba mtu moyoni wakati Mwenyezi Mungu ametupa nafasi ya kusameheana? Kazi ni kwako chukua hatua leo kuvunja laana hiyo.

Kwahiyo, tumealikwa katika somo letu la leo tuweze kujipa nafasi muhimu katika maisha yetu ambayo ni kuthubutu bila kuogopa kitu chochote. Kwani kuthubutu kufanya jambo Fulani katika maisha yako ni kama kuondoa au kuvunja laana. Leo jipe nafasi muhimu ya kuthubutu ili uvunje laana ya vile ambavyo unashindwa kuvifanyia kazi kwenye maisha yako.

Mpendwa rafiki na msomaji wa mtandao wa Kessy Deo, nakutakia utekelezaji mwema katika haya uliyojifunza leo. Ili tuendelee kuwa pamoja zaidi kila siku penda kutembelea ukurasa wetu wa facebook na jiunge hapa na mtandao wetu  kwa kubonyeza maandishi yaliyokolezwa.

Asante sana

Rafiki na mwalimu wako,

Deogratius Kessy

0717101505/0767101504 au deokessy.dk@gmail.com

 

Published by Deogratius Kessy

Mwandishi,mwalimu na mjasiriamali. Unaweza kutembelea Blog yake ya www.kessydeo.home.blog kujifunza zaidi na unaweza kuwasiliana naye kwa namba 0717101505/0767101504 au kwa barua pepe deokessy.dk@gmail.com

Leave a comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: