Habari ya leo mpendwa rafiki na msomaji wa mtandao wa Kessy Deo? Ni matumaini yangu kuwa uko vizuri na unaendelea vema kufanya kazi zako za kila siku. Hongera sana rafiki yangu kwa zawadi ya siku hii ya leo. Leo ni siku bora sana kwetu hivyo basi tuitumie vizuri kwa manufaa yetu na wengine pia. Kumbuka katika masaa 24 una namba hizi 1440 ambazo ni dakika na sekunde 86400 ndani ya masaa yako 24.
Mpendwa rafiki, kwanza nakushukuru kwa kuendelea kuwa pamoja nami kila siku kupitia mtandao pendwa wa Kessy Deo. Hongera sana rafiki juu ya hili pia, napenda kukualika kujiunga na mtandao wetu kwa njia ya mfumo wa email yaani barua pepe kwa kubonyeza HAPA ili tuendelee kuwa karibu zaidi. Kwanini ujiunge? Unajiunga ili uweze kupokea makala,vitabu na maarifa( mafunzo) mbalimbali.
Mpendwa rafiki, hongera sana kama utakua umeshajiunga na mtandao wetu kwa njia ya kupokea mafunzo kupitia mfumo wetu wa email. Napenda kutumia nafasi hii kukualika katika makala yetu ya leo ili tuweze kujifunza wote kwa pamoja. Hivyo basi, kufahamu ni nini nimekuandalia siku hii ya leo nakusihi sana karibu tusafiri pamoja mwanzo hadi mwisho wa somo letu la leo karibu mpendwa msomaji.
Mpendwa msomaji, malengo mahususi ya somo letu la leo ni mbinu bora ya kukusaidia wewe kushinda kabisa kuahirisha mambo (procrastination). Kuahirisha mambo amekuwa ni adui wa muda wetu na amekuwa akiua ndoto za watu wengi sana. kila siku watu wanaoahirisha mambo wanaongezeka na kadiri mtu anavyoweka malengo na mipango yake ya siku lakini bado anaendelea kuahirisha mambo.
SOMA; Hiki Ndicho Kinachowamaliza Watu Wengi
Kwahiyo, ndugu msomaji, watu wamekuwa ni mabingwa wa kusaliti ndoto zao kupitia kuahirisha mambo. Wengine wanapanga leo nitafanya kitu Fulani lakini anaahirisha na kushindwa kufanya. Mwaka huu umeanza wengi wamekuwa na mbwembwe kwamba wanakwenda kubadilika na kuanza kuishi maisha mapya na wengi waliandika malengo mengi lakini mpaka sasa wengi wamesharudi katika maisha yao ya mazoea.
Pengine mtu alijiwekea ndani ya mwaka huu nitakuwa nafanya mazoezi kila siku na kupunguza kula hovyo lakini huenda mtu alijaribu ndani ya siku mbili lakini tayari amesharudi katika maisha yake ya zamani. Kukosa msimamo na mfumo mzuri wa maisha ndiyo chanzo cha yote haya cha kuahirisha mambo.
Sasa swali la kujiuliza kama kila siku unaahirisha mambo je dawa yake ni nini ili uweze kuacha? Jibu; kama kuna jambo linakusumbua kila siku na unashindwa kulifanya na kila siku unaahirisha sasa leo nimekuletea dawa nayo ni; unapoamka tu asubuhi fanya kile kitu unachokiahirisha kila siku. Unapoamka wewe acha kwanza mambo mengine anza kufanya lile jambo ambalo unashidwa kulifanya kila siku. Kwa mfano, kama ulikuwa unasema kila siku nitasoma kitabu basi anza nalo kabla hujafanya mambo mengine kwa kutumia mbinu hii itakusaidia kushinda kabisa kuahirisha mambo.
SOMA; Huyu Ndiye Rafiki Muhimu Unayepaswa Kutembea Naye Katika Safari Ya Mafanikio
Hatua ya kuchukua leo; kama unasumbuliwa na kuahirisha mambo basi dawa nzuri kufanya hicho pale tu unapoamka kutoka kitandani. Hii mbinu inaitwa Eat that frog first strategy tafuta kitu unachokiaahirisha sana na tumia mbinu hii utafanikiwa.
Mwisho, somo letu leo limetualika sisi sote kuweza kutumia mbinu hii ya kufanya kile kitu ambacho kinakusumbua katika kuahirisha kila siku na kifanye tu pale unapoamka na utaweza kufanikiwa. Chochote kinachokusumbua katika kuahirisha kianze kufanya cha kwanza pale tu unapoamka asubuhi kutoka kitandani.
SOMA; Hiki Ndio Kitabu Kizuri Ambacho Watu Wengi Wanakipenda Na Wanaweza Kukiandika Katika Maisha Yao
Mpendwa rafiki na msomaji wa mtandao wa Kessy Deo, nakutakia utekelezaji mwema katika haya uliyojifunza leo. Ili tuendelee kuwa pamoja zaidi kila siku penda kutembelea ukurasa wetu wa facebook na jiunge hapa na mtandao wetu kwa kubonyeza maandishi yaliyokolezwa.
Asante sana
Rafiki na mwalimu wako,
Deogratius Kessy
0717101505/0767101504 au deokessy.dk@gmail.com