Design a site like this with WordPress.com
Get started

Muhimu; Haya Ndiyo Madhara Ya Kukimbiza Sungura Wawili Kwa Wakati Mmoja

Habari ya wakati huu mpendwa rafiki na msomaji wa mtandao wa Kessy Deo? Ni matumaini yangu kuwa u buheri wa afya. Hongera sana rafiki kwa zawadi ya siku ya leo hivyo ni vema kuutumia muda wetu vizuri katika mambo chanya yatakayoleta maendeleo katika jamii yetu.

Image result for if you chase two rabbits you catch neither

Mpendwa msomaji, napenda kutumia nafasi hii kukualika katika makala yetu ya leo ili tuweze kujifunza wote kwa pamoja. kwahiyo, nakusihi sana tuweze kusafiri wote kwa pamoja mpaka mwisho wa somo letu. Karibu sana mpendwa msomaji tuweze kujifunza wote kwa pamoja.

Katika makala yetu ya leo tutakwenda kujifunza kupitia methali ya wenzetu kutoka huko urusi. Warusi wanamethali yao moja ambayo nimeipenda leo tuweze kushirikishana wote kwa pamoja kupitia methali hii. Methali hii inasema hivi ‘’ if you chase two rabbits, you will catch neither one’’. Wakiwa na maana ya kwamba kama ukiwafukuza au kuwakimbiza sungura wawili kwa wakati mmoja basi hutomkamata hata mmoja.

SOMA;  Ifahamu Falsafa Pendwa Inayotafutwa Na Watu Wengi

Rafiki, tunashauriwa sana kufanya jambo moja kwa wakati mmoja ili uweze kupata matokeo mazuri. Kama umekaa unakula basi achana na mambo mengine kaa kimya kula chakula. Haipendezi huku unakula, unaangalia tv na unachat na simu. Tumia muda mmoja uliouchangua kwa lengo moja kwanza mpaka umalize siyo kushika vitu viwili kwa wakati mmoja.

Watu wengi wamekuwa wakiwafukuza sungura wawili kwa wakati mmoja na hatimaye wanakuja kuwakosa wote. Unakuta mtu ana malengo mengi na yote anataka kufanya kwa wakati mmoja na kupata matokeo mazuri. Kwa kufanya hivi utashangaa unashindwa yote kuyatimiza. Kama una mambo mengi unataka kufanya chagua jambo moja kwanza na mfanye ndio sungura wako mmoja unamkimbiza mpaka unamkamata. Lakini ukisema ufanye yote kwa pamoja utakosa yote badala yake kamilisha kwanza jambo moja.

Hatua ya kuchukua leo, usifanye mambo mawili kwa wakati mmoja fanya kwanza jambo moja kwa kwa wakati mmoja ndio utapata matokeo mazuri. Hata kama una mambo mengi chagua kimoja kwanza na komaa nacho kwanza halafu ukikimaliza tafuta kingine. Kufanya mambo mengi kwa wakati mmoja ni sawa na kukimbiza sungura wawili kwa wakati mmoja. Fanya jambo moja kwa wakati mmoja. (Success demands singleness of purpose – Vince Lombardi)

SOMA;  Haya Ndiyo Machaguo Mawili Unayopaswa Kuchagua Mojawapo Ndani Ya Mwaka 2017

Kwa kuhitimisha,Waswahili wanasema, mtaka yote kwa pupa hukosa yote kwa pupa na warusi wanasema ukiwakimbiza sungura wawili hutomkamata hata mmoja. Kwahiyo tunajifunza ili tufanikiwe katika malengo yetu tunapaswa kukomaa na jambo moja kwanza kwa wakati mmoja na siyo kufanya mambo mengi kwa wakati mmoja utajikuta unapoteza yote. Ufanisi ni kufanya kitu sahihi kwa wakati mmoja.

Mpendwa rafiki na msomaji wa mtandao wa Kessy Deo, nakutakia utekelezaji mwema katika haya uliyojifunza leo. Ili tuendelee kuwa pamoja zaidi kila siku penda kutembelea ukurasa wetu wa facebook na jiunge hapa na mtandao wetu  kwa kubonyeza maandishi yaliyokolezwa.

Asante sana

Rafiki na mwalimu wako,

Deogratius Kessy

0717101505/0767101504 au deokessy.dk@gmail.com

 

Published by Deogratius Kessy

Mwandishi,mwalimu na mjasiriamali. Unaweza kutembelea Blog yake ya www.kessydeo.home.blog kujifunza zaidi na unaweza kuwasiliana naye kwa namba 0717101505/0767101504 au kwa barua pepe deokessy.dk@gmail.com

Leave a comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: