Design a site like this with WordPress.com
Get started

Ifahamu Falsafa Pendwa Inayotafutwa Na Watu Wengi

Habari ya leo mpendwa rafiki na msomaji wa mtandao wa Kessy Deo? Ni matumaini yangu hujambo na unaendelea vizuri. Leo ni siku bora sana na ya kipekee kwetu hivyo tunaalikwa kumshukuru Mungu kwa zawadi ya siku hii ya leo kwani wengi walitamani kuiona siku hii ya leo lakini mimi na wewe tumeweza kustahilishwa kuiona tena siku hii ya leo.

Mpendwa rafiki, napenda kukukumbusha kila siku juu ya matumizi ya muda kwani muda ndio msema kweli wa mambo yote hapa duniani. Kama leo ulipanga kufanya kitu Fulani nakusihi inuka nenda kafanye usisibiri kesho au baadaye wala usisubiri kupewa rushusa na mtu Fulani bali thubutu bila kujali. Unaweza kulalamika huna hela lakini unaweza kushukuru tu kwa zawadi ya uhai na ukatumia talanta yako kuwa Baraka  kwa watu wengine.

Mpendwa msomaji, tuna mambo mengi yakufanya katika maisha lakini kila siku tunasema nikipata muda lakini kumbuka ya kwamba nikipata muda amekuwa akitajwa na kila mtu lakini hajawahi kuitika kwa mtu yeyote Yule akaenda bali ukitaka upate muda ni fanya sasa yaani just do it.

SOMA;Hiki Ndio Kitabu Kizuri Ambacho Watu Wengi Wanakipenda Na Wanaweza Kukiandika Katika Maisha Yao

Mpendwa rafiki na msomaji wa mtandao Kessy Deo, napenda nikualike tena katika makala yetu ya leo ili tuweze kujifunza wote kwa pamoja yale mazuri niliyokuandalia siku hii ya leo. Hivyo nakusihi sana uweze kuambatana na mimi hadi mwisho wa somo letu la leo.

Leo tutakwenda kujifunza juu ya falsafa pendwa inayotafutwa na watu wengi. Watu mbalimbali duniani wanajaribu kuunda vyama mbalimbali, mashirikia, jumuiya , makundi mbalimbali ili tu kujiunga kwa pamoja na kutafuta falsafa pendwa inayochochea maendeleo na kutafutwa na watu wengi ambayo ni umoja. Hili tunaliona hata katika dini zetu kwa mfano wakristu au waislamu wanajumuiya au vikundi vidogo vidogo vinavyowakutanisha kwa kusali pamoja  na hatimaye kuunda umoja.

Rafiki, kuna ile falsafa inayosema umoja ni nguvu na utengano ni dhaifu hii ni kweli kabisa yeyote ambayo haina umoja basi pamekufa au kudhoofika. Wafanyakazi wanaofanya kazi pamoja kama hawana umoja kwenye taasisi waliyopo hawezi kuleta maendeleo na ufanisi katika shirika, taasisi au kikundi husika. Watu wakisoma umoja basi kuna kuwa kitu kinachoendelea kuwatafuta ambacho ni ubinafsi.

SOMA;Haya Ndiyo Madhara Ya Ubinafsi Katika Jamii Yetu Ya Leo

Mpenzi msomaji, tunaona ni jinsi gani baba wa taifa mwalimu Nyerere alivyoweza kutuunganisha sisi watanzania wote kwa kutumia lugha ya Kiswahili. Ni mataifa mangapi duniani yanakosa kuelewana kwa sababu ya kukosa umoja? Kwenye koo zetu, jumuiya zetu, makundi mbalimbali yanashindwa kufika mbali kimaendeleo kwa sababu ya kukosa umoja. Hivyo basi, kumbe falsafa ya umoja ni falsafa yeye nguvu inayoweza kuchochea maendeleo sehemu yoyote ile.

Hatua ya kuchukua leo, anza kuwa na umoja kuanzia ngazi ya familia yako mpaka na watu wengine wanaokuzunguka. Kuwa na ushirikiano na umoja hata kwa mwenza wako, fanyeni mambo kwa umoja ndio utaona matunda ya umoja. Unapaswa kumsamehe aliyekukosea ili muweze kujenga umoja ni ngumu kuwa na umoja kama watu wanaishi na chuki zilizoumbika ndani mioyo.

Kwahiyo, falsafa ya umoja ndio falsafa pendwa inayotafutwa na watu wengi duniani kwa ajili ya kuleta maendeleo sehemu Fulani. Umoja unaleta amani, upendo na furaha lakini kinyume cha umoja huleta ubinafsi, chuki, wivu, ugomvi, masengenyenyo na kuanza kurushiana makombora ya umbea na nk.

Mpendwa rafiki na msomaji wa mtandao wa Kessy Deo, nakutakia utekelezaji mwema katika haya uliyojifunza leo. Ili tuendelee kuwa pamoja zaidi kila siku penda kutembelea ukurasa wetu wa facebook na jiunge na mtandao wetu.

Asante sana

Rafiki na mwalimu wako,

Deogratius Kessy

0717101505/0767101504 au deokessy.dk@gmail.com

Published by Deogratius Kessy

Mwandishi,mwalimu na mjasiriamali. Unaweza kutembelea Blog yake ya www.kessydeo.home.blog kujifunza zaidi na unaweza kuwasiliana naye kwa namba 0717101505/0767101504 au kwa barua pepe deokessy.dk@gmail.com

Leave a comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: