Design a site like this with WordPress.com
Get started

Hivi Ndivyo Unavyoweza Kutumika Kama Baraka Kuendeleza Dunia

Habari ya leo mpendwa rafiki na msomaji wa mtandao wa Kessy Deo? Natumaini uko vizuri na umeianza siku vizuri kabisa ukiwa na mtazamo chanya wa kwenda kufanya makubwa kabisa katika maeneo yetu ya kazi na hatimaye kuijenga dunia na kuwa sehemu salama. Hongera pia kwa zawadi ya siku hii ya leo  rafiki yangu ni vema kutumia muda vizuri ili kuacha alama duniani.

whatsapp-image-2016-09-30-at-16-29-22BONYEZA HAPA KUPATA KITABU HIKO HAPO JUU

Napenda kutumia nafasi hii kukualika katika makala yetu ya leo tuweze kujifunza wote kwa pamoja. Hivyo karibu rafiki tuweze kusafiri wote kwa pamoja mpaka mwisho wa makala yetu.

Leo tutakwenda kujifunza wote kwa pamoja namna au jinsi ya kutumia Baraka ulizopewa  na Mungu kuendeleza dunia. Kwanza kabisa,  sisi binadamu tuna vitu vya kipekee ndani yetu ambavyo hata mtu mwingine hana. Kila mtu ana kitu cha ziada ambacho mtu mwingine hana,hata katika timu ya mpira kila mchezaji ana namba yake ya kipekee uwanjani. Mnaweza kuwa wote walimu lakini kila mwalimu anakitu chake cha ziada ambacho mtu mwingine hana.

Kumbe basi, sisi binadamu tumepewa talanta mbalimbali hivyo tunapaswa kuzitumia kwa kuzalisha au kundeleza dunia. Kila mtu anakitu cha kuchangia katika hii dunia bila kuhitaji mtaji wa pesa. Unachotakiwa ni kukubali kufanya na kuongoza bila kuwa na wadhifa au nafasi Fulani katika jamii. Angalia unaweza nini na nenda kasaidie watu kwenye kile unachoweza hivi ndivyo unavyoweza kutumika kama Baraka kwa watu wengine.

Mpendwa msoamji, tumia hicho ulichopewa na kufanya  kuwa Baraka kwa watu wote kuwa msaada kwa watu wote kulingana na kile ambacho Mungu amekupa. Paendeleze hapo ulipo sasa kama ni kazi basi tengeneza ajira nyingi ili uendelee kugusa maisha ya watu wengine. Kama una kampuni moja iendeleze kuzaa kampuni nyingine. Endeleza kile ulichonacho ili kiweze kuwafikia watu wengi zaidi ya hapo sasa.

SOMA; Hivi Ndivyo Unavyoweza Kugusa Maisha Ya Watu Wengine Hapa Duniani

Hatua ya kuchukua leo; umeiweka wapi talanta yako? Umeajiriwa? Umejiajiri? Au bado huna ajira? Unaitumiaje talanta yako kama Baraka uliyopewa na Mungu kuendeleza dunia? Tumia talanta yako kuiendeleza dunia. Usisubiri kupewa ruhusa wakati sahihi ni sasa na kuwa tayari kuongoza bila ya kuwa na cheo, nafasi au wadhifa Fulani bali anza na hicho ulichonacho.

Kwa kuhitimisha, binadamu tupo wengi duniani kuliko maendeleo yanayoonekana kwa macho. Mimi na wewe tunapaswa kuiendeleza dunia kwa kutoa mchango wetu hii ni pamoja na kutumia talanta au Baraka tulizopewa na MUNGU ili kuendeleza dunia. Lakini kumbuka rafiki ili tuiendeleze dunia tunapswa kuacha ubinafsi kwanza na tuangalie wengine.

Mpendwa rafiki na msomaji wa mtandao wa Kessy Deo, nakutakia utekelezaji mwema katika haya uliyojifunza leo. Ili tuendelee kuwa pamoja zaidi kila siku penda kutembelea ukurasa wetu wa facebook na jiunge hapa na mtandao wetu  kwa kubonyeza maandishi yaliyokolezwa.

Asante sana

Rafiki na mwalimu wako,

Deogratius Kessy

0717101505/0767101504 au deokessy.dk@gmail.com

 

Published by Deogratius Kessy

Mwandishi,mwalimu na mjasiriamali. Unaweza kutembelea Blog yake ya www.kessydeo.home.blog kujifunza zaidi na unaweza kuwasiliana naye kwa namba 0717101505/0767101504 au kwa barua pepe deokessy.dk@gmail.com

Leave a comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: