Design a site like this with WordPress.com
Get started

Mambo Muhimu Unayoweza Kujifunza Kutoka Katika Kitabu Cha Emotional intelligence works

Habari mpendwa rafiki na msomaji wa mtandao wa Kessy Deo? Ni matumaini yangu kuwa uko salama na umeianza Siku yako kwa mtazamo chanya.
Leo ni siku ya kipekee sana kwetu hivyo tunamshukuru Mungu kwa zawadi ya siku hii ya leo kwa kuweza kutustahilisha kuvuta pumzi yake leo.
Napenda kutumia nafasi kukualika katika makala yetu ya leo. Leo tutakwenda kujifunza uchambuzi wa kitabu cha emotional intelligence works hivyo nitakushirikisha mambo machache kati ya mengi kupitia kitabu hiki.
Karibu sana tujifunze wote kwa pamoja. Kitabu hiki kimeandikwa na waandishi wawili nao ni Michael Kravit na Susan Schubert.

Mambo 20 niliyojifunza katika kitabu cha Emotional Intelligence ni kama ifuatavyo;

1. Kitu kinachomtofautisha binadamu na myama ni uwezo wa kufikiri. Binadamu ana utashi,ana uwezo wa kufikiri,kuamua na kufanya maamuzi sahihi. Kitu kinachomfanya binadamu awe binadamu ni kufikiri. Kufikiri ndio kazi ya binadamu.

2. Fikiri kabla ya kuongea ni usemi unaongeza umakini katika akili yako. Ni usemi unaokusaidia kuchuja mambo unayotaka kuongea. Haitoshi kufikiri kabla ya kuongea bali pia baada ya kuongea. Maneno huwa yanaweza kuleta athari kwa hadhira iliyokusudiwa hivyo ni muhimu kufikiria kabla hujaongea je hicho kitu unachotaka kuongea kina mantiki gani?
Fikiri kabla na baada ya kuongea.

3. Ubongo wako una sehemu kuu tatu zinazofanya kazi kwa ushirikiano kama timu ya washauri. Vitu hivyo ni
.hisia,mantiki na matendo halisi unayofanya bila kujifikiria au kujifunza.
Shabaha ya vitu hivi ni kukuweka salama na kukupa ushauri.
Kila mshauri ana ujuzi wake tofauti hivyo ni muhimu kuwaelewa wote ukiwa katika uhalisia wa mazingira.

4. Motisha ni kama nishati inayokupa nguvu na kukufanya utembee. Katika maisha ni vema kujua nini kinakusukuma wewe. Ukijua nini kinakusukuma basi hiyo ndio motisha kwako inayokupa nguvu ya kusonga mbele na kufanya kazi kwa hamasa.
Elewa kile kinachokupa motisha .

5. Kila binadamu ni muhimu kufikiria katika uwezekano. Katika hii dunia kuna watu wa aina mbili.
Pessimist hawa ni wale watu wanaoamini katika kushindwa. Yani wanafikiria kila kitu ni hatari hapa duniani. Wanaamini katika hali ya mtazamo hasi katika kila kitu. Je wewe uko upande huu?
Optimist ni wale watu wanaoamini katika uwezekano. Wanaona dunia ni sehemu ya kufurahia,salama na chanya kwao.

6. Mtu anayejua umuhimu wa kazi yake lazima atatengeneza maana. Atafanya kazi kwa hamasa,atawasaidia wengine ,ataongeza thamani katika eneo lake la kazi. Hivyo basi, ni muhimu kufanya kazi unayoipenda.

7. Optimist ni watu wanaojijali wao wenyewe na wengine. Hawana ubinafsi, wanawasaidia wengine katika nyanja mbalimbali. Kufanya maisha ya wengine kuwa bora, kila ambacho ni kizuri anawashirikisha wengine. Furaha yao ni kuona wao na watu wengine wakifanikiwa.

8. Kuimarisha mahusiano kuna leta athari chanya kwa afya yako. Kuwa na mahusiano mabovu ni sumu katika miili yetu. Kuwa na mawasiliano mazuri na wengine, simamia na kujizuia hisia zako kama vile hasira na msongo wa mawazo na kuwa huru kuzoea au kuendana na mazingira yoyote.

9. Ni muhimu kujua utamaduni wa jamii unayozungumza naye. Utamaduni wa jamii nyingine hauruhusu mwanaume na mwanamke kusalimiana kwa kushikana mkono. Masiliano ni muhimu kabla hujasalimiana mtu tambua kwanza utamaduni wake unaruhusu tabia ya kupeana mkono? au kukumbatiana ili usimkwaze mtu kulingana na tamaduni yake.

10. Kila binadamu ana tamaduni zake kulingana na jamii anayotoka. Kila mtu huwa ana lafudhi yake ambayo inamtofautisha na jamii nyingine. Mfano mkenya akiongea kiswahili na mtanzania akiongea kiswahili watu hawa wawili utaweza kuwatofautisha kwa lafudhi yao na kugundua kabisa huyu ni mtanzania au huyu ni mkenya. Hivyo kujua tamaduni za jamii nyingine ni nzuri utajifunza mambo mengi.

11. Msongo wa mawazo sugu unaweza kusaidia na vitu hivi kama vile mazoezi,mazoezi ni muhimu kwa afya ya nwili na akili,kujali,jijali wewe na wengine wasaidie wengine au shirikiana nao.
Kucheka nayo ni muhimu. Cheka mara nyingi uwezavyo kwani kucheka panakupa furaha na usikae katika hali ya kisirani. Msongo wa mawazo ni sumu mbaya kwa

afya kwani unaleta athari katika mwili wako.

12. Kama mwalimu unayemsaidia mtu kwa kumpatia maarifa huna budi kumuongoza na kumsimamia mtu huyo kwa kile unachomfundisha.
Muoneshe mtazamo chanya,mpe ushirikiano mzuri, jenga uhusiano mzuri na mwanafunzi wako jaribu kuvaa viatu vyake ili ajihisi upo sehemu yake na unamjali.

13. Optimism wanaamini wakati ujao ni bora kuliko sasa. Hawaogopi vikwazo wanavyokutana navyo. Wanaamini inawezekana licha changamoto za kila siku.

14. Pessimism ni watu wanaokimbia changamoto,walalamikaji wakubwa.
Wakosoaji wakubwa. Wanaruhusu kila habari hasi hivyo zinasababisha kuendelea kujichim
bia shimo. Ukiona mtu ni rafiki wa vitu hasi yupo sehemu ya hatari ya kushambuliwa na magonjwa ya mtazamo hasi.
Kwahiyo, ni vema kuchukua hatua ya kubadilika.

15. Kufanya kazi kitimu kunaongeza ufanisi.
Kuna ongeza uzalishaji. Kufanya kazi kitimu mnakuwa mna malengo sawa,ushirikiano hivyo kila mmoja anajitoa kuhakikisha mnafikia malengo mliyojiwekea.

16. Miongoni mwa changamoto zinazoweza kujitokeza katika timu ya kazi ni kutoaminiana.
Mawasiliano mabovu,ubinafsi nk.
Kwahiyo, ni muhimu kujua changamoto pia katika timu weki.

17. Wanachama bora katika timu wanatakiwa wame imara na wenye nguvu. Wame watu wenye shauku kubwa na hamasa na wanaoamini katika uwezekano.
Kinyume na hapo ni changamoto.

18. Katika jamii watu wanahitaji elimu. Waelimishe kuhusiana na mbinu za mawasiliano katika kijami. Mawasiliano ni muhimu hivyo usipojua kuwasiliana na watu ndani ya jamii yako ni shida. Siyo kila mtu anajua namna ya kuwasiliana na watu.

19. Wasaidie watu katika kutatua changamoto. Wasikilize, wape ushauri juu ya tatizo linalowasumbua. Fanyia utafiti hayo matatizo yao. Wahudumie kwa kuwajali na kuwapenda. Dawa ya matatizo ni kupatiwa suluhu.

20. Katika kuendesha vikao ni muhimu kuzingatia moja vitu vituatavyo:
Kufahamu hadhira yako, fahamu majina yao usimwite mtu wewe,fahamu dini,jinsi zao na hata lugha zao.
Jiandae kuwapatia huduma muhimu kama ikiwezekana kama chakula nk.
Andaa mazingira ya kufanyia kikao na wape nafasi ya kuchagua kukaa katika nafasi anayopenda kulingana na mpangilio wa ukaaji.

Asante sana rafiki na endelea kutembelea mtandao huu kujifunza kila siku na usisahau kujiunga na mtandao huu lakini pia kupenda ukurusa wetu wa Facebook.

Rafiki na mwalimu wako,
Deogratius Kessy
0717101505/0767101504
deokessy.dk@gmail.com

Published by Deogratius Kessy

Mwandishi,mwalimu na mjasiriamali. Unaweza kutembelea Blog yake ya www.kessydeo.home.blog kujifunza zaidi na unaweza kuwasiliana naye kwa namba 0717101505/0767101504 au kwa barua pepe deokessy.dk@gmail.com

Join the Conversation

1 Comment

Leave a comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: