Design a site like this with WordPress.com
Get started

Hivi Ndivyo Unavyoweza Kugusa Maisha Ya Watu Wengine Hapa Duniani

Habari ya wakati huu mpendwa rafiki na msomaji wa mtandao wa Kessy Deo? Ni imani yangu kuwa uko salama rafiki na huku ukiendelea na kupambana na maisha. Endelea kupambana rafiki ili uweze kupata kile unachokitaka hapa duniani.

Hata kama unakumbana na changamoto kiasi gani usikate tamaa kwani maisha ni kama shule na changamoto ndio mitihiani ya shule. Hivyo kama unavyojua ukiwa shule ili uweze kuendelea na darasa la mbele lazima kwanza ufanye mtihani wa darasa ulilopo na ufaulu ndio uendelee na darasa lingine.

Image result for HOW TO TOUCH LIFE OF PEOPLE

Kwahiyo, katika maisha changamoto ni sehemu ya maisha yetu ya kila siku na ili tuende mbele na kupiga hatua lazima sasa tukutane na changamoto. Pole sana rafiki kwa changamoto unazokutana nazo hivyo basi kwa mfano huo hapo juu zichukulie kwa mtazamo chanya na sehemu ya kawaida katika maisha.

Rafiki, napenda kukualika tena katika makala yetu ya leo ili tuweze kujifunza wote kwa pamoja hivyo nakusihi rafiki yangu tuweze kuambatana wote kwa pamoja mpaka mwisho wa makala hii. Mpendwa msomaji, leo tutakwenda kujifunza kutoacha kufanya kile unachofanya sasa katika maisha yako. Kama ulikuwa unapenda kutabasamu kila siku basi usiache kutabasamu kuna mtu anahitaji tabasamu lako, kuna mtu anafarijika pale anapoona unatabsamu na kumpa furaha.

Kama wewe ni mtu mwenye roho ya upendo basi usiache kusambaza upendo kwa watu wengine. itumie falsafa ya upendo kikamilifu katika maisha yako bila kujali mtu. Usiache kuishi katika falsafa ya upendo kwani kuna mtu alisha zoea upendo wako. Kwahiyo wewe endelea kufanya kile unachofanya kwani kuna mtu unamgusa maisha yake bila ya hata wewe kujua.

SOMA;  Moto Wa Hamasa Utakaokuwezesha Kupata Nafasi Ya Kazi Sehemu Yoyote Duniani

Mpendwa msomaji, kupitia haya tunayofanya kila siku ndio tunavyogusa maisha ya wengine. kama wewe ulikuwa unawapa watu elimu kupitia kile unachoandika basi usiache kuandika kwani kuna watu unawagusa maisha yao hata kama hawakuambii. Kama umezoea kupita njiani na kusalimia watu basi usiache kumsalimia mtu unayekutana naye kwani kuna mtu anatamani kusalimiwa hakuna hata mtu wa kumsalimia.

Nakumbuka siku moja, kuna mtu alikwenda kumsalimia mzee mmoja ambaye yeye ni omba omba barabarani Yule mzee aliposalimiwa alishukuru sana na kujiona mtu wa kuthaminiwa kwani siku nzima watu walimpita bila hata ya kumsalimia lakini mtu Yule aliyekwenda kumsalimia alikuwa faraja kwake.

Kuna vitu vingine unavyoweza kufanya na kugusa maisha ya watu bila hata kuwa na mtaji. Kama wewe unaelimu ya sheria wafundishe watu kile unachojua kuhusu sheria kwa kufanya hivyo unakuwa unagusa maisha ya watu wengine. kama unacheza mpira endelea kucheza mpira kwani kuna mtu unamburudisha kulingana na uchezaji wako. Siyo mpaka watu wakuambie unawagusa maisha yao wewe fanya usiache kwani kuna wengine hata kama unawagusa maisha yao hawawezi kukuambia.

SOMA; Mambo Muhimu Unayoweza Kujifunza Kutoka Katika Kitabu Cha Failing Forward

Hatua ya kuchukua, usiache kufanya kile unachofanya kwani kupitia hicho unachofanya ndicho kinakuwezesha kugusa maisha ya watu hapa duniani. Usisubiri malipo wala shukrani bali wewe fanya bila kujali na timiza mapenzi yako hapa duniani.

Kwa kuhitimisha, kuna mambo madogo unayoweza kuyadharau katika maisha yako lakini kumbe ndiyo yale mambo ambayo yanayogusa maisha ya watu kuliko unavyofikiria. Unaweza kuongeza thamani hata kwa kumwambia mteja wako asante sana na karibu tena, unaweza kugusa maisha ya watu wengine hata kwa kuwahamasisha na kuwa tia moyo ili wasiendelee kukata tamaa ya maisha hapa duniani.

Mpendwa rafiki na msomaji wa mtandao wa Kessy Deo, nakutakia utekelezaji mwema katika haya uliyojifunza leo. Ili tuendelee kuwa pamoja zaidi kila siku penda ukurasa wetu wa facebook na jiunge hapa kwa kubonyeza maandishi yaliyokolezwa.

Asante sana

Rafiki na mwalimu wako,

Deogratius Kessy

0717101505/0767101504 au deokessy.dk@gmail.com

 

Published by Deogratius Kessy

Mwandishi,mwalimu na mjasiriamali. Unaweza kutembelea Blog yake ya www.kessydeo.home.blog kujifunza zaidi na unaweza kuwasiliana naye kwa namba 0717101505/0767101504 au kwa barua pepe deokessy.dk@gmail.com

Leave a comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: