Design a site like this with WordPress.com
Get started

Muhimu; Usiache Kusoma Hapa Kama Bado Hujajua Kiu Yako Ni Nini

Habari ya wakati huu mpendwa rafiki na msomaji wa mtandao wa Kessy Deo? Ni matumaini yangu kuwa uko salama na unaendelea kutimiza kusudi la maisha yako hapa duniani. Leo ni siku bora sana nay a kipekee kwetu hivyo tunapaswa kuitumia vizuri siku yetu ya leo kwa kujibidiisha katika yale mambo chanya na siyo hasi.

Mpendwa msomaji, napenda kukualika tena katika makala yetu ya leo ili tuweze kujifunza wote kwa pamoja. mpendwa rafiki, nashukuru kwa kuendelea kuwa msomaji wa mtandao huu wa Kessy Deo hivyo nakusihi sana tuendelee kuwa pamoja kila kadiri ya mapenzi ya Mungu.

Image result for YOUR PASSION

Rafiki, unapaswa kuwa na shukurani katika maisha yako kama wewe unalalamika huna kiatu kuna mwenzako hana hata mguu wa kuvalia hicho kiatu. Kwahiyo, ni vema kumshukuru Mungu kwa kile ambacho unacho sasa au kwa kiwango cha maisha ambacho unacho sasa kwani unaweza kulalamika juu ya maisha yako lakini kuna watu wengine wanatamani kile ambacho unacho wewe.

Mpendwa rafiki, karibu sasa katika makala yetu ya leo ambapo leo tutakwenda kujifunza wote kwa pamoja kiu yako ni nini? Kila mtu huenda akawa na kiu yake hapa duniani juu ya kupata kitu Fulani. Kiu zetu zinatofautiana kulingana na mtazamo wa mtu mwenyewe kiu yangu juu ya maisha yangu haiwezi kuwa sawa na wewe. Kama leo kila mtu angepewa nafasi ya kujua kile kilichokuwa moyoni mwake basi leo tungegundua ni jinsi gani kiu zetu za maisha ziko tofauti.

SOMA; Mambo Muhimu Unayoweza Kujifunza Kutoka Katika Kitabu Cha You Were Born Rich

Ndugu msomaji na rafiki yangu, huenda kiu yetu ikafanana wote  tukawa ni mafanikio lakini pia kila mtu anakiu Fulani ya mafanikio. Mwingine kiu yake ya mafanikio ni kuwa hela, mwingine kiu yake ni kua na mahela yaani kuanzia mamilioni hata mabilioni. Hivyo tunaona ya kuwa kiu ya mtu iko kama  ule msemo usemao mbuzi hula urefu wa kamba yake hivyo hata wewe kiu yako ndio itakufanya upate kile unachotaka katika maisha yako.

Rafiki, nafikiri ujua kiu ni nini mfano, katika hali ya kawaida mtu huwa anakiu ya maji ya kunywa sasa chukua mfano huu na kuelekeza katika kiu ya kupata vitu vingine pia. Kiu ni kama uteyari wako juu ya kupata kitu Fulani. Ili tufanikiwe ni lazima ujuwe unataka nini na kiu yako ni nini na utayari ukoje. Ukishakuwa na kiu au utayari hakuna sababu itakayo kuzuia kufika pale unapopataka.

Hatua ya kuchukua leo, anza leo kujua kiu yako katika maisha yako hapa duniani ni ipi? Una kiu ya kuacha alama gani hapa duniani? Je siku ukiondoka hapa duniani watu watakukumbukaje? Ni namna gani kiu yako itaweza kugusa maisha ya watu.

Kwahiyo, mara nyingi tunajiwekea ukomo katika maisha yetu sisi wenyewe. Wapo watu wamekaa na kiu zao huku wakisubiria ukamilifu kwa njia ya kulalamika. Fanya chochote hata kama ni kidogo muhimu tu ni kuwa na muelekeo wa kufika kule unakotaka kwenda.

Mpendwa rafiki na msomaji wa mtandao wa Kessy Deo, nakutakia utekelezaji mwema katika haya uliyojifunza leo. Ili tuendelee kuwa pamoja karibu zaidi kila siku penda ukurasa wetu wa facebook na jiunge hapa kwa kubonyeza maandishi yaliyokolezwa.

Asante sana

Rafiki na mwalimu wako,

Deogratius Kessy

0717101505/0767101504 au deokessy.dk@gmail.com

Published by Deogratius Kessy

Mwandishi,mwalimu na mjasiriamali. Unaweza kutembelea Blog yake ya www.kessydeo.home.blog kujifunza zaidi na unaweza kuwasiliana naye kwa namba 0717101505/0767101504 au kwa barua pepe deokessy.dk@gmail.com

Join the Conversation

2 Comments

Leave a comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: