Design a site like this with WordPress.com
Get started

Mambo Muhimu Unayoweza Kujifunza Kutoka Katika Kitabu Cha 7 Loss Secret Of Success

Habari ya leo mpendwa rafiki na msomaji wa mtandao wa Kessy Deo? Ni imani yangu kuwa uko salama na unaendelea vizuri. Hongera sana rafiki kwa zawadi hii ya leo. Leo nenda kaitendee haki siku hii ya leo lakini ni muhimu Sana kuitumia kwa kuzalisha mambo chanya kuliko hasi.

Image result for 7 LOST SECRETS OF SUCCESS BOOK JOE VITALE

Mpendwa rafiki, napenda kukualika katika makala yetu ya leo ili tuweze kujifunza kwa pamoja. Katika makala yetu ya leo nitakwenda kukushirikisha uchambuzi wa kitabu cha 7 Loss Secret of Success. Mwandishi Joe Vitale ana mengi aliyotushirikisha kupitia kitabu chake hivyo anatualika sisi tuweze kujifunza pamoja naye.

Na yafuatayo ni mambo 20 niliyojifunza katika kitabu cha 7 Loss Secret of Success kilichoandikwa na Joe Vitale. Karibu tuweze kujifunza wote kwa pamoja.

1. Biashara ni mwalimu mkubwa. Biashara inatufundisha mambo mengi. Kwanza inatukutunisha kukutana na watu wengi na waina mbalimbali. Biashara inatuwezesha kukabiliana na hofu mbalimbali. Kuna mambo mengi tunajifunza kupitia biashara.

2. Biashara inasaidia dunia. Biashara ndio tumaini la dunia. Fanya biashara katika usimamizi mzuri na kuwa huru kutoa huduma. Inatupasa tufikirie vitu ambavyo vitabadili dunia hata kama havijatokea vitakuja kutokea mfano,Barton alifikiria juu ya luninga hata kabla haijagunduliwa dunia. Hivyo basi, Kuwa na maono baade ni kitu kizuri sana.

3. Mteja ni mfalme. Je unamjua mteja wako? Kama unafanya kazi kwa bosi wako basi bosi wako ndio mteja wako. Je umeshamwambia mteja wako unauza nini? Au unatoa huduma gani? Waambie wateja wako unafanya nini tangaza ili ujulikane unatoa huduma gani?
Mwisho,ni muhimu kuwaambia wateja wako unauza nini au unatoa huduma gani.

4. Mungu ametengeneza dunia lakini hajakutengenezea dunia yako. Dunia yako unajijengea mwenyewe. Amekupa maghali za kila aina. Kilichobaki ni wewe kujenga dunia yako unayotaka.
Hivyo basi, kila mtu anajitengenezea dunia yake mwenyewe kwa lugha nyingine kila mtu anatengeneza maisha yake mwenyewe.

5. Kitabu ni maisha ya mtu. Kuacha kumbukumbu ya kitabu ni kusaidia watu leo na kesho. Hata ukifa kitabu chako kitakuwa kinafundisha dunia. Ukipata nafasi ya kuandika kitabu andika kwa faida ya kizazi cha leo na kesho. Na mchango wako hautasauliwa kamwe.

6. Vita ni shughuli iliyokosa tumaini. Hakuna mtu anayeshinda kwani kila mtu anapoteza vitu vingi na hasara kubwa. Vita vinarudisha maendeleo nyuma na kupoteza watu wengi wasiokuwa na hatia. Watu wenye ujuzi mbalimbali hupotea pia.

7. Kuonyesha biashara yako ni kutangazia watu. Ni kusaidia watu unafanya nini. Kwanini unatangaza biashara? Kwanza ni kufundisha watu kiundani kujua wewe unafanya nini na unatoa huduma gani. Hakuna mtu atakayejua bila kusema unatoa huduma gani.
Kwahiyo, kutangaza biashara ni kusaidia watu kujua kile unachofanya.

8. Watu wanapenda kuambiwa kwa mfumo wa stori. Kama unataka kuandika kitu na kuelimisha watu chochote andika. Hakuna mtu anayejua unachojua mpaka uwaambie. Hivyo basi, toa kile unachojua na kusaidia watu.

9. Tafuta mbinu nzuri ya kuhoji watu na kuwatatisha juu ya kitu fulani kuliko kutumia mbinu ya kutukana. Unauwezo wa kuwasilisha kitu kwa namna nzuri bils hata kwa njia ya matusi na watu wakakuelewa.

10. Utawezaje kuuza bidhaa ambayo hutumii? Utawezaje kuuza bidhaa ambayo hatawewe hauisapoti? Watu sio wajinga wanapenda kuona wewe mzalishaji kwanza wa kitu hiko unatumia na kukithamini na kukitangaza kitu hicho na siyo vinginevyo.

11. Kwenye kila kitu unatakiwa kuwa mwaminifu. Kama wewe ni mwandishi kuwa mwaminifu katika uandishi wako. Kama wewe ni daktari toa huduma yako ya utabibu kwa uaminifu wa hali ya juu. Uaminifu ni kitu muhimu sana katika maisha yetu kwenye kila kitu.

12. Hii ni kanuni ya asili ukipokea unapaswa kutoa. Kama umepata maarifa juu ya kitu fulani unapaswa na wewe kuyatoa. Toa nguvu yako uliyopewa. Toa muda wako na fedha kwa ajili ya wengine pale unapopokea kanuni ya asili ni kutoa.

13. Je umenoa kisu chako?
Maisha yanahitaji ujinoe kila siku katika nyAnja hizi zifuatazo;jione kiakili noa akili yako ili uweze kupata maarifa. Jione kimwili ili uweze kufurahia maisha. Unahitaji kuona roho yako ili kukua kiroho.
Maisha yanahitaji kujinoa kila idara. Noa malezi ya watoto kama bado ni butu. Noa uaminifu wako katika maisha ya ndoa.

14. Fanya kazi yako na kuiheshimu. Hakikisha unaisimamia mpaka upate ukamilifu wake. Juhudi,maarifa ,nidhamu na uaminifu vitakuletea ukamilifu wa kazi yako wenye matokeo bora kabisa.

15. Kabla hujafa hakikisha maisha yako ya huku duniani yamekuwa ya mchango mkubwa na yaliyoweza kugusa maisha ya watu wengi.
Kwa lugha nyepesi tunapaswa kurefusha wasifu wetu kabla hujafa na hapa tunazungumzia wasifu uligusa maisha ya watu siyo familia yako huo utakua ni ubinafsi.

16. Katika kuwa mtendaji kuliko kuwa mkosoaji.
Mtendaji au
mfanyaji huwa ni mtu wa kusonga mbele. Unapofanya kitu chochote tarajia kupata ukosoaji wowote. Kaza kamba na usikatishwe tamaa na mtu yoyote na kuwa kiziwi juu ya mambo wanayosema.

17. Unatakiwa kuamini na kumshirikisha Mungu juu ya mambo yako. Kama unalima amini unalima na utapata matokeo mazuri kabisa juu ya kile unachofanya. Kama huna imani ni sawa na hakuna unachokifanya.

18. Mambo yote unayofanya matokeo yake yanapimwa na uvumilivu. Watu wengi wanakosa uvumilivu katika safari zao na kushindwa kufika. Hakuna jambo linalotokea bila kusubiri. Ukitaka kupata mtoto lazima usubiri ndani ya miezi tisa ili upate matokeo ya kumpata mtoto. Huwezi kulazimisha ni lazima ufuate kanuni ya asili.

19. Tumia kanuni na mambo muhimu unayojifunza kila siku katika maisha yako. Kusoma ni kitu kingine na kutekeleza na kuishi uliyojifunza ni kitu kingine. Kuishi katika mabadiliko yoyote yanahitaji utayari wako katika mabadiliko.

20. Jina lako ndio linakutambulisha kwa kile ulichofanya. Je jina lako likitajwa watu watasikia nini kutoka katika jina lako? Mtu wa kulitengeneza jina lako ni wewe mwenyewe. Unahitaji kuishi maisha ya kujitoa kulingana na kile ulichonacho. Una vitu vingi vya kuwasaidia wenzako mbali na fedha .

Nakutakia kila la heri katika haya uliyojifunza leo. Penda ukurasa wetu wa Facebook ili tuzidi kuwa karibu zaidi na kuendelea kujifunza nenda chini kabisa utaona page yetu na like.

Rafiki na mwalimu wako,
Deogratius Kessy
0717101505/0767101504
deokessy.dk@gmail.com
Asante sana.

Published by Deogratius Kessy

Mwandishi,mwalimu na mjasiriamali. Unaweza kutembelea Blog yake ya www.kessydeo.home.blog kujifunza zaidi na unaweza kuwasiliana naye kwa namba 0717101505/0767101504 au kwa barua pepe deokessy.dk@gmail.com

Leave a comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: