Design a site like this with WordPress.com
Get started

Washangaze Watu Leo Kwa Kuwafanyia Kitu Hiki Katika Maisha Yako

Habari ya wakati huu mpendwa rafiki na msomaji wa mtandao wa Kessy Deo? Ni matumaini yangu kuwa hujambo na unaendelea vizuri.  Hivyo basi, napenda kutumia nafasi hii kukualika katika makala yetu ya leo ili tuweze kujifunza wote kwa pamoja.

Rafiki, katika makala yetu ya leo tutakwenda kujifunza somo la kuwashangaza watu katika maisha yako hivyo nakusihi tuambatane pamoja  mpaka mwisho wa makala  hii.

Katika maisha yako pengine umekuwa ni mtu wa kufanya mambo kimazoea na siwezi kukulaumu kwa sababu ndio mfumo wa kuishi kimazoea katika jamii zetu.  Mfumo umetukaririsha kufanya mambo kimazoea bila hata ya kuhoji kwa nini unafanya hicho unachofanya. Unafanya tu kwa sababu kila mtu anafanya katika jamii yako.

Image result for SURPRISED PEOPLE

Mpendwa msomaji, leo nataka nikupe mbinu nzuri ya kuondoka katika mfumo wa kuishi maisha katika hali ya kimazoea. Njia nzuri ya kuondoka huko ni kubadilika kwa kuwashangaza watu kwa kufanya mambo tofauti. Anza na zoezi hili kwenye kila idara inayogusa maisha yako na anza kuwashangaza watu kwa kufanya mambo tofauti kabisa na watu wengine wanavyofanya.

SOMA; Amka Na Fanya Mabadiliko Haya Muhimu Kwenye Maisha Yako

Rafiki, kama hujawahi kutumia kanuni ya dhahabu katika maisha yako yaani golden rule basi leo washangaze watu kwa kuwatendea kama vile unavyotaka wewe kutendewa. Kama ulikuwa wewe ni mbinafsi na mdhulumi basi leo washangaze kwa kuwafanyia mema na endelea na hii tabia ya kuwashangza kila siku ndani ya mwezi mmoja utakuwa umeondoka katika kuishi katika mfumo wa kimazoea.

Mpendwa msomaji wangu, leo nenda kaishangaze familia yako kwa kukaa nayo, kula pamoja mezani na kufanya maongezi ya kifamilia. Washangaze kwa kuwapa muda wako leo hata watoto wako waone uwepo wako wewe kama mzazi. Kama hujawahi kuwaambia watoto wako maneno ya upendo basi leo washangaze kwa kuwaambia unawapenda, wakumbatie watoto wako waweze waweze kuhisi uwepo wako na ikiwezekana wabusu na waonyeshe upendo ambao hujawahi kuwapa tangu wazaliwe yaani washangaze.

Rafiki, kama wewe ni binadamu basi huwezi kukwepa mahusiano kama uko hai hapa duniani basi nakuomba leo nenda kawashangaze watu kwa kurudisha uhusiano uliovunjika. Kama kuna watu ulikuwa huongei nao basi washangaze leo kwa kuongea nao. Kama kuna watu ulishawaambia hutowasamhe washangaze kwa kuwafutia deni la msamha. Washangaze ndugu zako kwa kuwasiliana nao leo kama ulikuwa haujawahi kuwasiliana nao. Washangaze ndugu, jamaa, marafiki, mwenza wako leo kwa kuimarisha mahusiano yenu na kujenga mawasiliano yaliyo bora kati yenu.

Mpenzi msomaji, leo nenda kawashangaze watu kwa kutoenda kukaa baa na kaa nyumbani. Leo washangaze watu kwa kutoangalia tv na kusoma vitabu. Washangaze watu leo kwa kuwaambia maneno ya Baraka na siyo yale ya kulaani. Washangaze watu kwa kuacha kupiga majungu, kusengenya, umbea na badala yake anza kuwa mtu mwazi na msema kweli unayeongea bila unafiki kama ni nyeusi unasema nyeusi na kama ni nyeupe unasema ni nyeupe.

SOMA;Fahamu Kitu Muhimu Ambacho Familia Yako Inakosa

Rafiki, mambo ni mengi sana unayotakiwa kuwashangaza watu katika maisha yako iwe ni maeneo ya kazi, nyumbani, nyumba za ibada unatakiwa kwenda hatua ya ziada ambayo watu wengine hawaendi. Rafiki leo nataka nikuombe uanze kuwa rafiki wa kutafuta maarifa kwani utaweza kuwshangaza watu zaidi kwa kufanya mambo tofauti zaidi ya hapo. Anza leo kusoma vitabu na washangaze watu leo kujiunga na kundi makini na bora Tanzania la kusoma vitabu liitwalo Tanzania Voracious Readers  jiunge leo ili uweze kupata maarifa sahihi yatakayomulika kule uendako  na bonyeza hapa kujiunga na kundi hilo.

Hatua ya kuchukua; washangaze watu kufanya mambo tofauti na vile ulivyokuwa unafanya katika maisha yako. Kama ulikuwa unafanya kazi zako kwa kulipua leo fanya kwa umakini wa hali ya juu ili uwashangaze na wewe unaweza. Zoezi hili ni kila idara ya maisha yako unatakiwa kuwashangaza watu kila siku.

Angalizo, washangaze kwa kufanya mambo chanya na siyo hasi.

Mwisho, ili uondoke katika maisha ya mazoea huna budi kuwashangaza watu kwa kuamua kubadilika kwa vitendo kuanzia sasa. Amua sasa kubadilika kwani ndio wakati muhimu katika maisha yako.

Nakutakia kila la heri katika haya uliyojifunza leo. Endelea kutembelea mtandao huu kujifunza kila siku. Asante sana.

Rafiki na mwalimu wako,

Deogratius Kessy

0717101505 /0767101504 au deokessy.dk@gmail.com

 

Published by Deogratius Kessy

Mwandishi,mwalimu na mjasiriamali. Unaweza kutembelea Blog yake ya www.kessydeo.home.blog kujifunza zaidi na unaweza kuwasiliana naye kwa namba 0717101505/0767101504 au kwa barua pepe deokessy.dk@gmail.com

Leave a comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: