Design a site like this with WordPress.com
Get started

Huyu Ndiye Rafiki Muhimu Unayepaswa Kutembea Naye Katika Safari Ya Mafanikio

Habari mpendwa rafiki na msomaji wa mtandao wa Kessy Deo? Ni matumaini yangu kuwa hujambo na unaendelea vizuri. Hivyo basi napenda kutumia nafasi hii kukualika katika makala yetu ya leo tuweze kujifunza wote kwa pamoja. rafiki kujifunza kila siku ndio iwe falsafa ya maisha yako kwani hatujui vitu vingi ndio maana tunaalikwa kujifunza kila siku kama mwanafalsafa Socrate aliwahi kusema kwamba hekima ambayo anayo ni kwamba hajui kitu hivyo hekima yake ilikuwa  inamchochea zaidi katika kujifunza.

UTEKELEZAJI NDIYO RAFIKI YAKO KATIKA SAFARI YA MAFANIKIO

Mwingine hapo alipo anaweza kujisifu na kuwa na kiburi kwa sababu ya elimu aliyonayo hivyo kiburi kinamshawishi kwamba yeye anajua kila kitu na hana haja ya kujifunza. Kama uko katika hali hiyo uko sehemu ya hatari nakusihi sana ondoka na nenda sehemu salama.

Mpendwa msomaji, katika malengo mahususi ya somo letu la leo tutakwenda kujifunza na kumfahamu rafiki unayepaswa kutembea naye katika safari ya mafanikio. Je unamjua rafiki unayepaswa kutembea naye katika safari ya mafanikio yako? Tafadhali nakusihi sana uambatane na mimi mpaka mwisho wa makala yetu ili uweze kumfahamu rafiki yako.

Rafiki, huu ni mwanzo wa mwaka mpya huenda umeandika malengo yako mengi pamoja na mipango mbalimbali ya kukuwezesha kufanikisha ndoto yako. Ili mambo yako yote yaweze kuwa katika uhalisia unapaswa kutembea na rafiki huyu popote uendako kama unataka kupata mafanikio ya aina yoyote katika maisha yako.

SOMA; Jambo Linalosubiriwa Kwa Hamu Na Watu Wengi Litokee Katika Maisha Yao

Rafiki unayepaswa kutembea naye katika safari ya mafaniko yako ni utekelezaji au kwa lugha ya kikoloni wanasema implementation. Huwezi kufanikiwa kwa kitu chochote kama huna utekelezaji wa mambo. Ili maisha yetu yabadilike lazima tuyatekeleze yale ambayo tunapaswa kuyafanya kwa vitendo.

Imekuwa ni wimbo wa watu wengi kujiwekea malengo mengi katika maisha yao hususani mwanzo wa mwaka lakini inapofika mwisho wa mwaka anakuwa hajavuna chochote alichoandika kama alishindwa kutembea na rafiki huyu ambaye ni utekelezaji. Tunapozungumzia mafanikio tunagusa kila idara ya maisha yetu hili ni jambo muhimu ambalo unapaswa kulifahamu katika maisha yako. Mafanikio siyo kuwa na hela peke yake hivyo tunapaswa kujua ya kwamba mafanikio yamegawanyika katika maeneo tofauti.

SOMA; Hiki Ndio Kitabu Kizuri Ambacho Watu Wengi Wanakipenda Na Wanaweza Kukiandika Katika Maisha Yao

Kwahiyo, kama unataka kuboresha mahusiano yako na watu wengine basi anza kutembea na rafiki wa utekelezaji ili uweze kumaanisha kile unachosema. Kama unataka kubadili chochote katika maisha yako na kufanikiwa basi nakusihi sana tembea na utekelezaji kwani ndiye rafiki atakayekufikisha pale unapotaka kufika. Lakini tambua ya kwamba utaweka mipango na malengo katika maisha yako lakini kama hutotembea na rafiki huyu huwezi kupata mabadiliko yoyote chanya kwenye kile unachotarajia kupata.

Hatua ya kuchukua leo. Ili uweze kufanikiwa kwenye mambo yote uliyopanga unatakiwa kutembea na utekelezaji. Ukitembea na utekelezaji kwenye malengo na mipango yako hakika hatokuacha kama ulivyo. Epuka sababu nyingi ambazo hazijengi na tembea na utekelezaji anayejenga.

Kwa kuhitimisha, maisha ni safari hivyo ili uweze kufika pale unapotaka kwenda ni vema kutembea na utekelezaji. Unapaswa kuthubutu chochote unachopanga kwenye maisha yako ndio utaona matokeo lakini bila ya hivyo utaendelea kuchora sifuri katika maji na kamwe hutoweza kuiona.

Mwisho, usisahu pia kumshirikisha na mwenzako makala hii nzuri uliyosoma leo. Pia, Hakikisha unapenda ukurasa wetu wa facebook kwa maarifa zaidi.

 

Nakutakia kila la heri katika haya uliyojifunza leo. Endelea kutembelea mtandao huu kujifunza kila siku. Asante sana.

Rafiki na mwalimu wako,

Deogratius Kessy

0717101505 /0767101504 au deokessy.dk@gmail.com

 

Published by Deogratius Kessy

Mwandishi,mwalimu na mjasiriamali. Unaweza kutembelea Blog yake ya www.kessydeo.home.blog kujifunza zaidi na unaweza kuwasiliana naye kwa namba 0717101505/0767101504 au kwa barua pepe deokessy.dk@gmail.com

Leave a comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: