Design a site like this with WordPress.com
Get started

Mambo Muhimu Unayoweza Kujifunza Katika Kitabu Cha Smart Leaders Smarter Teams

Habari Mpendwa Rafiki na Msomaji wa mtandao wa Kessy Deo? natumaini uko vizuri rafiki na pole kwa changamoto unazopitia katika maisha yako.

Rafiki, karibu sana katika makala yetu ya leo ambapo leo nitakwenda kukushirikisha uchambuzi wa kitabu. Kitabu hiki kinatupa umuhimu wa viongozi kujenga timu imara ili waweze kufikia kile ambacho wanakitaka. karibu tujifunze rafiki.

Image result for smart leaders smarter teams
Mambo 20 niliyojifunza katika kitabu cha Smart Leaders Smarter Teams na Roger Schwarz ni kama ifuatavyo;

1. Wafanyakazi kufanya kazi kwa kujituma,ushirikiano,mahusiano mazuri huleta matokeo mazuri katika taasisi au kampuni.
Kubadilishana uzoefu,kuulizana maswali bila ya hofu ni njia nzuri ya kujifunza kwa wafanyakazi. Hivyo basi, kwa misingi hiyo wafanyakazi wanatakiwa kuwa na ushirikiano,kujenga mahusiano mazuri,kuulizana maswali ya kuwa na hofu huleta matokeo chanya katika kampuni au taasisi husika.

2. Mabadiliko ni uchaguzi wa mtu. Dunia inaweza kubadilika kila siku lakini uamuzi ni wako katika kubadilika.
Katika uongozi lazima ukubali mabadiliko. Na haitoshi tu kubadilika lazima ubadili kwanza mtazamo wako. Badili kwanza akili yako ili uweze kupata mabadiliko. Mafanikio yanaanza katika kubadili fikra hivyo jambo lolote la mabadiliko linahitaji ubadili mtazamo wako na kuwa chanya.

3. Zawadi kubwa kwa wafanyakazi wote wenye uwajibikaji katika kazi ni kutoa na kupokea uaminifu.
Uaminifu umeakuwa adimu katika dunia ya leo.
Uaminifu ni zaidi ya hela na uaminifu unatoka ndani ya mtu na siyo kuigiza.

4. Dhumuni na thamani ya kitu unachofanya ndio hamasa kubwa inayopelekea kufanya kazi kwa uwajibikaji.
Kama unafanya kazi hujui dhumuni au lengo la kazi,hujui thamani ya kazi yako ni ngumu kwako kukosa hamasa na uwajibikaji katika kazi.

5. Timu inahitaji muundo,mfumo na kanuni katika uongozi. Vitu hivi kwa pamoja vitapelekea timu kuwa imara lakini pia timu kuwa na tija katika uzalishaji.

6. Kama wewe ni mkurugenzi kiongozi unatakiwa uongoze bila ya upendeleo. Mtendee kila mtu uongozi sawa kulingana na mazingira.
Ukiwa ni mtu wa tofauti kwa kila mtu utagawa watu. Tenda sawa kwa wafanyakazi wote. Kama unaonesha uadilifu basi simamia uadilifu wako kwa watu wote hapo ndio utaonesha uongozi imara.

7. Katika uongozi ni nzuri kila mmoja kujifunza kitu kutoka kwa mwenzake. Mnakuwa mnaheshimiana kila mtu anatakiwa kuheshimu hisia za mwenzake katika kujifunza. (Mutual learning).
Kila mtu ana kitu cha kipekee ambacho mwenzake anaweza kujifunza. Katika kujifunza hutakiwi kuwa na umimi yani ubinafsi.

8. Ukitaka kushinda lazima uwe na kitu kinachoitwa malengo.
Malengo ndio kisababishi kinachokusuma wewe kutimiza kile ulichokiahidi mpaka unashinda.
Hivyo malengo yanamsaidia mtu kushinda.

9. Ubunifu ni hali ya kufanya kitu kuwa kipya. Katika kila kitu unachofanya huwa kinahitaji ubunifu. Kama ni uongozi nao unahitaji ubunifu. Kama mama ntilie x amepika chai yake na kuweka majani ya chai peke yake na mama ntilie y akaweka viongo vingi kama vile mdalasini,tangawizi,iliki nk hivyo mama y atakuwa amefanya ubunifu na chai yake itakua ya tofauti kuliko mama x.

10. Akili ya binadamu huwa inafanya kazi haraka kabla hata ya kufikiri. Tunatakiwa kufikiri kitofauti ili kupata majibu sahihi. Ni vema kubadili mfumo mzima wa kufikiri kila mara kwa kulisha akili zetu maarifa chanya kila siku. Akili ya binadamu ipo kama mfumo wa compyuta inatakiwa iwe inaapdetiwa mara kwa mara na njia nzuri ya kuapdet akili yako ni kulisha maarifa.

SOMA; Mambo Muhimu Niliyojifunza Katika Kitabu Cha New Whole Mind

11. Uwazi na shauku ya kutaka kujifunza na kujua vitu huwa inapelekea watu wa pande mbili kila mmoja kumwelewa mwingine. Mutual learning inasaidia kila pande kufaidika kama wewe unapenda kujifunza basi utakuwa na shauku ya kutaka kujua kutoka kwa mwingine na wewe utaweza kutoa kile ulichonacho kwa mwenzako.

12. Timu ya Utawala wa juu inatakiwa kushirikisha taarifa kwa wanachama wake. Timu ya utawala wa juu inatakiwa kuwa na ushirikiano mzuri na watu wanaowaongoza ili kuleta uongozi mzuri wenye tija.
Ushirikiano unaleta matokeo bora na timu kuwa imara.

13. Kiongozi unatakiwa kusoma zaidi mazingira,angalia uko katika hali gani na unatakiwa kufanya kitu gani. Kuna mazingira kiongozi unatakiwa uangalie na muda mwingine huruma inatakiwa itumike. Matendo ya huruma katika uongozi yanaongeza uaminifu.

14. Kiongozi unatakiwa kuvaa uhalisia wa mtu unayemwongoza. Mfano mtu ana maumivu unatakiwa uvae viatu vyake yaani ulichukue lile tatizo na ulifanye kama lako. Onesha mrejesho wa kumsaidia mtu aliyepatwa na tatizo.
Kwahiyo,kiongozi anatakiwa kujali watu wake na kuwasaidia pale wanapopatwa na tatizo.

15. Kusikiliza ni kazi kuliko kuongea. Mtu anapoongea kaa kimya,msikilize kwa masikio mawili na mwangalie kwa macho mawili.
Kiongozi kazi yako unasikiliza siyo kuongea. Huwezi kumsaidia mtu mwenye matatizo bila ya kumpa nafasi kujielezea.
Wewe kama daktari mwache mgonjwa akueleze shida yake ili ujuwe anaumwa nini na uweze kumtibu.

16. Timu imara yenye ushirikiano inakuwa na hali ya kujitoa,kusikilizana nk.
Hatimaye timu inaleta matokeo au uzalishaji wa hali ya juu sana.
17. Jinsi tunavyofikiri ndivyo tunavyoongoza.
Ni kweli kabisa mawazo yetu ndiyo yanaongoza ushirikiano na mawazo ya kila mmoja ndio yanaleta tija katika suala zima la uongozi.

SOMA;  Mambo Muhimu Unayoweza Kujifunza Kutoka Katika Kitabu Cha Lead To The Field

18. Katika mawasiliano yoyote kuna kitu lazima kiwepo nacho ni mrejesho(feedback).
Vivyo hivyo, katika uongozi panahitajika pawe na mawasiliano ambayo yana mrejesho mzuri.
Katika uongozi kama hakuna mawasiliano na mawasiliano ni hali ya kupashana habari. Katika kupashana habari lazima kuwe na mrejesho.

19. Kama timu lazima iwe na muundo ulibuniwa.
Timu inatakiwa iwe na malengo na mipango ya kuwaongoza katika kazi wanayofanya.
Kama timu ya uongozi ikiwa na muundo mzuri itapunguza hali ya sitofahamu na migogoro isiyokuwa na ulazima.
Hivyo,timu inatakiwa ina muundo uliobuniwa ambao ni mzuri katika uongozi.

20. Maswali unayouliza ni maswali ya aina gani?
Maswali yanatakiwa kuwa na tija na halisi.
Ukiuliza maswali ambayo hayahitaji jibu unakuwa unapoteza wakati. Uliza swali ambalo linahitaji kujibiwa na siyo swali ambalo halitaji jibu.
Kwahiyo,maswali ni muhimu ili kuweza kupata jawabu la swali. Uliza swali sahihi ili kupata jibu sahihi.

Mwisho, kama utakuwa unahitaji kitabu hiki kwa ajili ya kujifunza zaidi tuwasiliane kwani kitabu kizuri sana kwa kila mtu kama  ni kiongozi, mfanyakazi na n.k.  Endelea kutembelea mtandao huu kujifunza kila siku na like ukurasa wetu wa facebook chini kabisa ya makala.

Rafiki na mwalimu wako,

Deogratius Kessy

0717101505/0767101504

deokessy.dk@gmail.com

Asante sana

Published by Deogratius Kessy

Mwandishi,mwalimu na mjasiriamali. Unaweza kutembelea Blog yake ya www.kessydeo.home.blog kujifunza zaidi na unaweza kuwasiliana naye kwa namba 0717101505/0767101504 au kwa barua pepe deokessy.dk@gmail.com

Leave a comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: