Design a site like this with WordPress.com
Get started

Haya Ndiyo Machaguo Mawili Unayopaswa Kuchagua Mojawapo Ndani Ya Mwaka 2017

Habari mpendwa rafiki na msomaji wa matandao Kessy Deo? Natumaini uko salama mpendwa rafiki na msomaji wa mtandao huu. Napenda kutumia nafasi hii kututakia heri ya sikukuu ya mwaka mpya 2017. Natumaini  kama unasoma hapa basi ni dhahiri kabisa mimi na wewe tumeweza kustahilishwa tena kuuona mwaka mpya wa 2017 hivyo basi, ni vema na haki kumshukuru Mungu kwa zawadi ya mwaka mpya na siku hii ya leo.

whatsapp-image-2016-09-30-at-16-29-22

KUPATA KITABU CHA FUNGA NDOA NA UTAJIRI BONYEZA MAANDISHI HAYA

Mpendwa msomaji,  napenda kunukuu moja ya mistari ya nyimbo moja ya injili unaosema, ‘’ siyo kwamba nimekwisha fika au nimekwisha kamilika la! Bali ninakaza mwend …’’ kwanini nimenukuu wimbo huu? Kwa sababu ya kwamba wimbo huu unatualika sisi sote kwamba siyo kwamba sisi ndio tumekamilika zaidi au tunastahili zaidi ila la bali ni mapenzi ya Mungu tu kuwepo tena mwaka 2017 kwani wengi tulikuwa nao lakini hawakuweza kuvuka.

Nipende kuwapa pole wale wote waliopoteza ndugu zao, jamaa na marafiki katika mwaka 2016. Mwandishi wa kitabu cha sometimes you win sometimes lose  John Maxwell anatualika kwa kutuambia kuwa katika maisha yetu tuna wakati tunashinda na tuna wakati tunapoteza au tunashindwa. Hivyo basi, katika maisha yetu tunapaswa kuzipokea hali zote mbili kwani huwa zinakuja hata kama hutaki. Matatizo ni sehemu ya maisha yetu.

SOMA; Haya Ndiyo Madhara Ya Ubinafsi Katika Jamii Yetu Ya Leo

Aidha, mtunzi wa huo wimbo hapo juu anatualikwa tuendelee kukaza mwendo ili tuweze kufika kule tunakotaka kufika. Tusikate tamaa tuanze mwaka katika mtazamo chanya na tutarajie kupata matokeo chanya.

Kwahiyo, mpendwa rafiki, leo katika makala yetu ya leo napenda kukualika tuweze kujifunza machaguo mawili unayopaswa kuchangua ndani ya mwaka 2017. Karibu tuendele kuwa pamoja hadi tamati ya somo letu.  Katika mwaka huu 2017 rafiki una machaguo mawili tu na wala siyo mengi nayo ni;

  1. Kuendelea kuishi maisha kama vile ulivyokuwa unaishi yaani kwa kifupi ni kuendelea kusihi maisha yale yale ya kimazoea

Mpendwa msomaji, kama wewe unataka kuwa sehemu ya wanamafanikio unapaswa kujiuliza uendelee kubaki kwenye hatari au kwenda sehemu salama chaguo ni lako hakuna aliyekushikia fimbo ni wewe mwenyewe kuamua. Kama mwaka jana umeisha ulikuwa ni mtu wa kuahirisha mambo kila siku na mwaka huu una uamuzi tena kubadilika au kuendelea na yale yale maisha yako.

  1. Au unaweza kuchukua hatua SASA na kufanya mabadiliko. Hapa unaamua kufuata mfumo ambao wanamafanikio wengi wanaufuta hapa duniani. Kama ukibadilika ndio utaweza kuona mabadiliko kwenye miasha yako na kama hutobadilika usitegeme kupata matokeo bora kwenye maisha yako.

Hatua  ya kuchukua leo. Mpendwa msomaji leo unaanza ukurusa mpya wa maisha yako ndani ya siku ya kwanza katika  mwaka 2017. Je leo unakwenda kuacha alama gani hapa duniani? Umechagua kufanya nini leo kubadilika ua kuendelea na maisha yale yale? Leo chagua kubadilika na ingia katika kundi la watu chanya na acha kuishi maisha yale yale ya kimazoea. Swali la kujiuliza leo ni siku ya kwanza katika mwaka 2017 je unakwenda kuacha alama gani duniani?

SOMA; Huu Ndio Ugonjwa Unao Ua Watu Wengi Katika Safari Ya Mafanikio

Kwa kuhitimisha, tumealikwa kuweza kuchagua machaguo mawili katika maisha yetu ambayo ni kuamua kubadilika au kuendelea kuishi na maisha yale yale ya kimazoea. Mpendwa rafiki, kazi ni kwako kama wasemavyo mtandao wa Vodacom.

Mwisho, usisahu pia kumshirikisha na mwenzako makala hii nzuri uliyosoma leo. Pia, Hakikisha unapenda ukurasa wetu wa facebook kwa maarifa zaidi. Bonyeza hapa ili kuweza kupata kitabu kizuri cha kujisomea kwa lugha ya kiswahili.

Nakutakia kila la heri katika haya uliyojifunza leo. Endelea kutembelea mtandao huu kujifunza kila siku. Asante sana.

Rafiki na mwalimu wako,

Deogratius Kessy

0717101505 /0767101504 au deokessy.dk@gmail.com

 

Published by Deogratius Kessy

Mwandishi,mwalimu na mjasiriamali. Unaweza kutembelea Blog yake ya www.kessydeo.home.blog kujifunza zaidi na unaweza kuwasiliana naye kwa namba 0717101505/0767101504 au kwa barua pepe deokessy.dk@gmail.com

Leave a comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: