Design a site like this with WordPress.com
Get started

Muhimu; Maneno Hatari Ya Kuepuka Kumwambia Mtoto Yeyote Hapa Duniani

Habari mpendwa rafiki na msomaji wa mtandao wa Kessy Deo? Natumaini unaendelea vizuri na hongera kwa zawadi ya uhai hivyo ni vema na haki kumshukuru Mungu. Kumbuka pia, kuutumia vizuri muda wako wa siku hii ya leo.

Mpendwa msomaji, napenda kutumia nafasi hii kukualika tena katika makala yetu nzuri ya siku hii ya leo.

Mpendwa rafiki, leo tutakwenda kujifunza jambo muhimu la kuepuka kumwambia mtoto wako.
Kuna falsafa moja inasema mtoto ni malezi. Na adui mkubwa katika malezi ya watoto ni mzazi mwenyewe.

Katika malezi ya watoto tunapaswa kuzingatia maneno tunayowaambia watoto kwani yanaumba(affirmation words). Chochote unachomwambia mtoto kinaenda kukaa katika akili yake. Kama unamwambia maneno mabaya au mazuri yote mtoto anayapokea na kuweka akilini.

Mpendwa msomaji, kiukweli maneno ya wazazi wengine huwa yanawaathiri sana watoto kisaikolojia. Mpendwa rafiki, ngoja nikupe mfano kwa kile nilichoshuhudia Jana. Nilikutana na mama mmoja akiwa na mtoto wake jana sehemu fulani. Sasa mtoto huyo alikuja kwangu akanikuta natumia simu mara akaniambia naomba niangalie picha ya watoto wako kwenye simu. Kweli katika simu yangu nilikuwa nimesevu picha ya watoto katika kioo cha simu.

Mpendwa msomaji, nikampatia yule mtoto picha aone na baada ya kuona akaniambia hivi ” watoto wako wazuri”
Nikamjibu hivi asante mbona hata wewe ni mzuri sana rafiki yangu.
Akanijibu Mimi siyo mzuri.
Nikamuuliza tena kwanini wewe siyo mzuri?

Mtoto akanijibu, mama huwa aniambia Mimi ni mbaya niko kama nyani.
Nikamjibu mtoto, ooh pole sana mama yako alikuwa anakutania ila wewe ni mzuri kuliko mtu mwingine hapa duniani na wewe ni mtu muhimu katika dunia hii. Nikamuongezea na kumwambia duniani watu wote tumeumbwa kwa mfano na sura ya Mungu.

Mpendwa msomaji, yule mama yake baada ya kusikia vile mtoto wake alivyoongea alijihisi vibaya na kuona aibu.

Mpendwa rafiki, katika simulizi yetu natumaini utakuwa umejifunza kitu. Hapa tunajifunza kuwa ni jinsi gani wazazi au walezi wanavyowaua watoto wao kiakili yaani kisaikolojia.
Mtoto alikataa kukubali kirahisi kuwa yeye ni mzuri mama alimlea na kumjaza fikra hizo tokea akiwa mtoto mdogo na kwasasa mtoto huyo ana miaka mitano. Mtoto amekuwa na ugonjwa wa uwezo wa kukosa kujiamini na kujithamini yeye mwenyewe yaani lack of self esteem.

Hatua ya kuchukua leo, mwambie mtoto wako maneno ya hamasa kama vile mwangu wewe ni mzuri, unaakili, ni bora nk yaani mjengee maneno chanya ya kumjenga kiakili katika ukuaji wake.
Epuka kumwambia mtoto maneno hasi kama vile ni mpuuzi, mpumbavu, huna akili, au una Mwita majina ya bandia nyani wewe, mbwa na nk.

Mwisho, ili tujenge jamii bora tunatakiwa kujenga familia bora. Hivyo tuwalee watoto katika mtazamo chanya na kuwajengea uwezo wa kujiamini na kuwaaminisha kuwa mambo yanawezekana.

Nakutakia kila heri katika haya uliyojifunza leo. Tafadhali mshirikishe na mwenzako maarifa haya uliyopata.

Rafiki na mwalimu wako,
Deogratius Kessy
0717101505/0767101504
deokessy.dk@gmail.com
Asante sana.

Published by Deogratius Kessy

Mwandishi,mwalimu na mjasiriamali. Unaweza kutembelea Blog yake ya www.kessydeo.home.blog kujifunza zaidi na unaweza kuwasiliana naye kwa namba 0717101505/0767101504 au kwa barua pepe deokessy.dk@gmail.com

Leave a comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: