Design a site like this with WordPress.com
Get started

Kitu Muhimu Unachopaswa Kuwa Nacho Makini Kwenye Maisha Yako

Habari mpendwa rafiki na msomaji wa mtandao wa Kessy Deo? Ni matumaini yangu kuwa hujambo na unaendelea vizuri kutimiza wajibu wako wa kila siku. Leo ni siku nyingine ya kipekee kwetu tumepewa zawadi hii bure kabisa hivyo basi, ni muhimu kuitumia vizuri siku yetu ya leo.

Mpendwa rafiki, napenda kukualika tena katika makala yetu ya leo tuweze kujifunza kwa pamoja ambapo leo tutakwenda kujifunza kitu muhimu unachopaswa kuwa nacho makini kwenye maisha yako. Je unajua ni kitu gani rafiki? Basi, nakusihi tusafiri pamoja mpaka mwisho wa makala yetu ya leo ili tuweze kujifunza kwa pamoja yale mazuri niliyokuandalia siku hii ya leo.

Image result for people has got no sign to them if is bad or kind

Mpendwa msomaji, hakuna mtu mwenye alama usoni ya kumtambulisha kuwa huyu ni mtu mwema au mbaya. Ukimwangalia mwezako usoni unaona alama yoyote usoni mwake? Jibu ni hapana. Nyuso zetu zinaweza kuvaa sura ya huruma lakini huruma ya mtu inaonekana ndani ya moyo wa mtu. Mtu anaweza kukuchekea lakini moyoni mwake anakuwazia mabaya siyo kila mtu kwa kumwangalia utajua ni mwema.

SOMA;Kitu Ambacho Binadamu Hapendi Kuambiwa Katika Maisha Yake

Rafki, kitu muhimu unachopaswa kuwa nacho makini hapa duniani basi ni kuwa makini sana na binadamu. Usipokuwa makini na binadamu utakuwa unalia kila siku kwa kuumizwa. Kama ingekuwa tupewa uwezo wa kuona mioyo ya wenzetu basi tusingekuwa tunadanganyana na wote tungekuwa tunasema ukweli kwani kila mmoja angekuwa anaona moyo wa wenzake. Uwe makini na binadamu kwenye maisha yako kwani hakuna aliyekuwa na alama usoni ya kuashiria kuwa yeye ni mwema.

Watu wengine wanaweza kuja kwako kukuomba msaada nakujifanya wanashida kweli na ukamsaidia lakini huyo huyo uliyemuonea huruma ndio anakuja kukutapeli au kukuibia. Katika zama hizi teknolojia imekuwa sana na kila siku watu wanabuni njia mpya za kutapeli hivyo basi, ni muhimui sana kuwa makini na binadamu.

Usimwamini mtu mara moja bali jipe muda wa kumchunguza na kujiridhisha vizuri ndio ufanye maamuzi juu ya kitu Fulani. Unaweza ukawa na huruma ya kusaidia lakini huruma inakuja kukuponza. Siyo watu wote wanakuja kwako kwa wema, wengine wanakuwa na lengo baya na wewe.

SOMA;  Soma; Simulizi Nzuri Ya Kusisimua Yenye Mafundisho Mazuri Ndani Yake

Hatua ya kuchukua leo, usimwamini mtu mara moja kwenye maisha yako. Jipe muda wa kumchunguza kwanza na usifanye maamuzi ya haraka haraka bali jipe muda wa kujiridhisha kwa taarifa muhimu kabla hujafanya maamuzi. Kuwa mwaminifu,mwadilifu, kuwa mtu sahihi na epuka uongo, utapeli kwenye maisha yako. Kuwa kweli nayo itakuweka huru, na kuwa mtu sahihi na watu sahihi watakufuata.

Mwisho, somo letu la leo lilitualika kuwa makini na binadamu katika maisha yetu kwani binadamu hawana alama usoni. Wanaweza kuvaa sura yoyote usoni lakini mioyoni mwao hawako hivyo. Mtu anaweza kukuambia anakupenda lakini moyoni mwake anakuchukia hivyo tuwe makini kwani nyuso zetu hazidhihirishi kile kilichopo moyoni.

Kama ulikuwa bado hujajiunga na mfumo wetu wa kupokea makala kwa njia ya email list jiunge leo ili uweze kupokea vitabu mbalimbali na makala mbalimbali. Pili, kama ulikuwa bado hujalaiki ukurasa wetu wa facebook fanya hivyo leo rafiki. Pia kama ulikuwa bado hujasoma kitabu kizuri cha funga ndoa na utajiri wahi mapema kujipatia nakala yako ambayo iko katika mfumo wa nakala tete yaani soft copy tuwasiliane kwa namba hii 0717101505/0767101504 kupata kitabu hiko. Mwisho, usisahu pia kumshirikisha na mwenzako makala hii nzuri uliyosoma leo. Hakikisha na mwenzako anapata maarifa haya mazuri.

Nakutakia kila la heri katika haya uliyojifunza leo. Endelea kutembelea mtandao huu kujifunza kila siku. Asante sana.
Rafiki na mwalimu wako,
Deogratius Kessy
0717101505 /0767101504 au deokessy.dk@gmail.com

Published by Deogratius Kessy

Mwandishi,mwalimu na mjasiriamali. Unaweza kutembelea Blog yake ya www.kessydeo.home.blog kujifunza zaidi na unaweza kuwasiliana naye kwa namba 0717101505/0767101504 au kwa barua pepe deokessy.dk@gmail.com

Leave a comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: