Design a site like this with WordPress.com
Get started

Jifunze Mambo Muhimu Ya Malezi Kwa Watoto Katika Kitabu Cha Selfish Reasons To Have More Kids

Habari ya wakati huu mpendwa rafiki na msomaji wa mtandao huu wa Kessy Deo? Ni imani yangu kuwa uko salama na unaendelea vizuri kutimiza wajibu wako. Napenda kukukaribisha tena siku hii ya leo niweze kukushirikisha yale mazuri niliyokuandalia. Ambapo leo nitakushirikisha mambo niliyojifunza katika kitabu cha selfish reasons to have more kids.
Mambo Niliyojifunza Katika kitabu cha SELFISH REASONS TO HAVE MORE KIDS Na Bryan Caplan ni kama ifuatavyo ;

Image result for selfish reasons to have more kids

1. Watoto wanahitaji mwongozo wa maisha kutoka kwa wazazi.
Unawezaje kua na mtoto halafu humpatii hata masaa ya kukaa nae na kumsikiliza?
Watoto wanahitaji muda wa wazazi kuwaonyesha njia ipasayo. Mfano, kama mzazi ulimkataza mtoto kufanya kitu fulani ambacho siyo sahihi kufanya hatoweza kurudia siku nyingine tena.
Lakini mtoto akikosa mwongozo wa kukemewa katika mabaya ataendelea kuyafanya kwani ataona ni sehemu ya maisha yake.
Hivyo basi,mtoto ni malezi.

2. Watoto wanaleta furaha katika maisha.
Usiwe mbinafsi wa kutokua na watoto na kama umri wako wa kua na familia umefika basi fanya hivyo.
Kuna sababu za kibailojia zitakubana sana mbeleni kama umri wako umeenda halafu bado tu huchukui hatua ya kufanya.
Faida ya kua na watoto utaiona pale unapokua mzee na kuwa na watoto ni kupanda mbegu bora ambayo utakuja kuivuna baadaye.

3. Kumekuwa na mitazamo hasi pale mtu anapotaka kua mzazi na kuambiwa maneno mbalimbali na jamii. Mfano,watoto watakufanya usilale,watoto watakufanya ubadilike na kauli nyingi kama hizo.
Mitazamo hii ndio inawafanya watu kuogopa kua na familia.
Kwahiyo,napenda kuwaondoa hofu kwamba familia haiwezi kukufanya ukose usingizi wala ubadilike.
Kubadilika kwa mtu ni maamuzi ya mtu na tabia ya mwenyewe.

SOMA;  Hii Ndio Faida Ya Kutumia Falsafa Ya Imani Ya Kidini Kwenye Malezi Bora Ya Watoto

4. Watu wenye watoto wanakua na furaha ukilinganisha na watu wasio na watoto.
Watoto wanaleta faraja lakini pia furaha katika familia.
Hivyo basi,maisha ni furaha na watoto ni faraja katika familia.

5. Wanatafiti wengi wakiwauliza wazazi ni nini wanafurahia kwa watoto watakuambia jinsi wakiwaona wakila,jinsi wanavyofanya nao mazoezi.
Jinsi wanavyocheza nao na nk.
Hivyo, kulingana na tafiti wazazi wenye watoto wanaonekana kua na furaha ukilinganisha na waliokua peke yao.

6. Kuna vitu muhimu vya kuzingatia katika malezi ya mtoto navyo ni;
Usingizi,kama mzazi hakikisha mtoto wako anapata muda wa kulala usingizi wa kutosha.
Nidhamu,usimamizi katika shughuli zao.
Watoto wanahitaji wazazi wao sana ili kuelezea hisia zao wanapokuwa wamefanya mambo yao.

7. Kuna msemo unasema mama asipokua na furaha hakuna anayekua na furaha.
Usemi huu unadhihirisha kwamba mama analeta furaha ya familia. Mama akiwa na furaha katika familia anawaambukiza wanafamilia wote furaha.
Watoto wanapokua wanamuona mama ni mtu mwenye furaha muda wote, uso wake ni wa furaha muda wote anawafanya watoto pia kua na furaha na kuona dunia ni mahali pazuri kuishi.

8. Watoto wa mapacha wanaofanana wako tofauti sana na watoto wa mapacha wasiofanana.
Kuwa tofautisha watoto hawa wanaofanana inakuwa si rahisi sana wengine huwa wanatumia alama ya kuzaliwa ili kuwa tofautisha.
Watoto ni zawadi kutoka kwa Mungu hivyo wapokee kama walivyo.

9. Wazazi wanatakiwa kuwapenda watoto wao. Kujali afya za watoto wao na kuhakikisha wanakula vizuri.
Wazazi wanatakiwa kuwazuia watoto kutojiingiza katika uvutaji tumbaku ,sigara na vilevi.
Mzazi kuvuta sigara mbele ya watoto ni alama ya picha hasi kwa watoto.
Kama mzazi epuka kufanya vitu ambavyo watoto wanaweza kuathirika kitabia hatimaye kuharibu afya.

10. Kukosa upendo na msaada kwa watoto wanapokua wadogo inapelekea watoto kukosa furaha katika maisha yao ya ukubwani.
Hivyo basi, walee watoto kwa upendo na msaada wakati wakiwa wadogo ili baadae wawe na furaha.

11. Wazazi waliofanikiwa wanakua na watoto waliofanikiwa kwasababu mtu aliyefanikiwa anapenda kumsaidia mwenzake kua kama yeye.
Mzazi anamsaidia mtoto wake katika masomo hususani katika kazi za nyumbani yaani home work.

12. Fanya kitu ambacho unapenda katika maisha yako siyo kile ambacho watu wanachopenda wewe kufanya.
Mzazi unatakiwa kumletea mtoto katika maadili yanayomfaa na siyo kumlea mtoto kulingana na jamii inavyotaka.
Mzazi chanya atamlea mwanae katika malezi chanya.

13. Je unatamani kumuona mtoto wako akifanikiwa?
Kama ndio msaidie kumpa mwongozo na kufanya ndoto zake kuwa katika hali ya uhalisia.
Kuwa mwalimu wa kwanza wa mtoto wako na hakikisha unamfundisha kuvua samaki na siyo kumpa samaki.

SOMA;  Haya Ndio Makosa Kumi Na Moja (11) Wanayofanya Wazazi Au Walezi Katika Malezi Ya Watoto

14. Mwalimu wa kwanza wa malezi kwa mtoto ni wazazi.
Lakini pia, jamii ina mchango mkubwa ka
tika kuchangia malezi ya mtoto. Sio kila kitu mtoto wako ataweza kujifunza kwako.
Kuna mambo mengine atajifunza kwa jamii ndio maana kuna umuhimu wa kuwa na familia bora ili kujenga taifa bora.
Familia ni mama wa jamii nzima. Hivyo msingi wa jamii ni familia.

15. Mfundishe mtoto falsafa ya imani.
Kama ni mkristu,muislam nk mfundishe mwanao misingi ya imani yako.
Jambo la muhimu la kuzingatia ni wewe kuyaishi kwa vitendo yale unayomfundisha mtoto.
Hivyo ongoza kwa mfano.

16. Wazazi wanahitaji watoto wakue wakati wao wenyewe hawakui.
Unataka mtoto wako abadilike wakati wewe mwenyewe haubadiliki.
Unataka maisha ya mtoto wako ya badilike wakati ya kwako hajabadilika.
Anza kubadilika kwanza wewe na wengine watafuata.

Nakutakia kila la heri katika haya uliyojifunza leo. Mshirikishe na mwenzako ili naye aweze kujifunza maarifa haya.
Rafiki na mwalimu wako,
Deogratius Kessy
0717101505/0767101504
deokessy.dk@gmail.com
Asante sana.

Published by Deogratius Kessy

Mwandishi,mwalimu na mjasiriamali. Unaweza kutembelea Blog yake ya www.kessydeo.home.blog kujifunza zaidi na unaweza kuwasiliana naye kwa namba 0717101505/0767101504 au kwa barua pepe deokessy.dk@gmail.com

Leave a comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: