Design a site like this with WordPress.com
Get started

Kitu Pekee Ambacho Huwezi Kukimaliza Katika Maisha Yako

Habari ya wakati huu mpendwa rafiki na msomaji wa mtandao wa Kessy Deo? Natumaini uko vizuri na unaendelea vema kutimiza wajibu wako wa kila siku. Ni matumaini yangu kuwa umeanza wiki yako vizuri ukiwa na hamasa kubwa na mtazamo chanya wa kwenda kufanya mambo kubwa ndani ya juma hili. Rafiki, usisahau kutumia muda wako vizuri na kumbuka kuwa maisha yako hapa duniani ni muda hivyo utumie vizuri kuhakikisha kila siku umefanya jambo ambalo ni chanya.

whatsapp-image-2016-09-30-at-16-29-22

BONYEZA MAANDISHI HAYA KUPATA KITABU HIKI.

Mpendwa rafiki, napenda kukualika tena katika makala yetu ya leo tuweze kujifunza kwa pamoja kile ambacho nimeweza kukuandalia siku hii ya leo. Leo tutakwenda kujifunza kitu pekee ambacho huwezi kumaliza katika maisha yako. Mpenzi msomaji, je unajua ni kitu gani ambacho huwezi kukimaliza katika maisha yako? Nakusihi sana ungana nami katika safari hii mwanzo mpaka mwisho ili uweze kujua kile kizuri nilichokuandalia leo.

Kila mtu ambaye yuko hapa duniani basi kuna kitu ambacho hawezi kukikosa nacho ni matatizo. Kila mtu ana matatizo yake hapa duniani na hata hivyo haijalishi wewe ni tajiri au maskini lakini wote kila mmoja ana matatizo yake binafsi. Na kama kila mtu angesema aanike matatizo yake hadharani basi kila mmoja wetu angejiona afadhali ya yeye kuliko mwenzake. Unaweza ukajiona wewe ndio mwenye matatizo sana kuliko watu wengine kumbe kuna watu wana matatizo zaidi yako.

SOMA ;   Soma; Simulizi Nzuri Ya Kusisimua Yenye Mafundisho Mazuri Ndani Yake

Rafiki, hata siku moja usilinganishe matatizo yako na mtu mwingine unaweza ukasema wewe unaumwa sana lakini nenda hospitali utakuta watu wanaumwa zaidi yako. Je ni kitu gani cha kipekee ambacho huwezi kukimaliza? Jibu ni kwamba kitu pekee ambacho huwezi kukimaliza hapa duniani ni matatizo ya mtu. Matatizo ya mtu huwa yana malizwa na mtu mwenyewe. Hivyo rafiki, kumbuka matatizo yako yanamalizwa na wewe mwenyewe kwa sababu hakuna anayejua matatizo yako zaidi ya wewe mwenyewe.
Hatua ya kuchukua; unaweza kumaliza matatizo yako tu na siyo kumaliza matatizo ya mtu mwingine hivyo leo pambana kumaliza yale matatizo yako yanayokusumbua muda mrefu. Hata ukikazana kumaliza shida za mtu huwezi kuzimaliza.

Kwa kuhitimisha, tunaalikwa kuwa matatizo pekee ambayo huwezi kuyamaliza ni matatizo ya watu wengine. Matatizo ya mtu yanamalizwa na mtu mwenyewe kama mwenzako anaumwa huwezi kumsaidia kumeza dawa ili apone bali itamlazimu ameze dawa mwenyewe ili apone.

SOMA;  Huyu Ndiye Mkombozi Wa Maisha Yako Atakaye Kuletea Mabadiliko Kuanzia Sasa

Kama ulikuwa bado hujajiunga na mfumo wetu wa kupokea makala kwa njia ya email list jiunge leo ili uweze kupokea vitabu mbalimbali na makala mbalimbali. Pili, kama ulikuwa bado hujalaiki ukurasa wetu wa facebook fanya hivyo leo rafiki. Pia kama ulikuwa bado hujasoma kitabu kizuri cha funga ndoa na utajiri wahi mapema kujipatia nakala yako ambayo iko katika mfumo wa nakala tete yaani soft copy tuwasiliane kwa namba hii 0717101505/0767101504 kupata kitabu hiko. Mwisho, usisahu pia kumshirikisha na mwenzako makala hii nzuri uliyosoma leo. Hakikisha na mwenzako anapata maarifa haya mazuri.

Nakutakia kila la heri katika haya uliyojifunza leo. Endelea kutembelea mtandao huu kujifunza kila siku. Asante sana.
Rafiki na mwalimu wako,
Deogratius Kessy
0717101505 /0767101504 au deokessy.dk@gmail.com

Published by Deogratius Kessy

Mwandishi,mwalimu na mjasiriamali. Unaweza kutembelea Blog yake ya www.kessydeo.home.blog kujifunza zaidi na unaweza kuwasiliana naye kwa namba 0717101505/0767101504 au kwa barua pepe deokessy.dk@gmail.com

Join the Conversation

1 Comment

Leave a comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: