Design a site like this with WordPress.com
Get started

Njia Bora Ya Kumteka Na Kumfukuza Mteja Katika Biashara Yako

Habari mpendwa rafiki na msoamji wa mtandao wa Kessy Deo? Ni matuamini yangu kuwa uko salama na unaendelea vizuri katika maisha yako. Kama uko katika changamoto au wakati mgumu katika maisha yako pole sana endelea kukabiliana nayo na ujue ya kwamba hakuna hali ya kudumu katika maisha yako vumilia tu hilo nalo litapita na uatarudia katika hali yako ya kawaida. Tunamshukuru Mungu pia kwa zawadi ya siku hii ya leo kwa kunistahilisha kuandika makala hii na kukustahilisha wewe kuweza kuwa msomaji wangu kupitia mtandao huu. Nashukuru sana rafiki yangu kwa kuendelea kuwa pamoja na mimi kupitia mtandao huu hivyo basi, napenda kutumia fursa hii kukualika tena katika makala yetu ya leo.

whatsapp-image-2016-09-30-at-16-29-22

Katika makala yetu ya leo tutakwenda kujifunza njia bora ya kumvuta mteja na kumfukuza katika biashara yako. Karibu rafiki tuweze kujifunza wote kwa pamoja. Ili uweze kufanikiwa katika biashara yako unahitaji mbinu bora za kuweza kumshawishi mteja wako. Hivyo njia bora ya kumteka au kumvuta mteja wako katika biashara yako ni kutoa huduma bora. Mteja wako ukimpatia huduma bora na kumjengea uaminifu wa baishara yako na kuonesha kuwa unamjali tayari unakuwa umemteka kinamna hiyo.

SOMA;     Huyu Ndiye Chuma Ulete Anayewatesa Watu Wengi Katika Maswala Ya Kiuchumi

Na njia nzuri ya kumfukuza mteja wako ni kutoa huduma mbovu katika baishara yako. Kama unatoa huduma mbovu kwenye kitu chochote basi kumbuka hiyo ndio njia nzuri ya wewe kumfukuza mteja wako. Ili biashara yako iweze kukua na kuendelea unahitaji wateja hivyo ni muhimu sana kutoa huduma bora na kumfanya mteja ajisikie sehemu salama katika biashara yako na kumhakikishia kuwa yeye ndio uhai wa baishara yako. Hivyo kama unataka biashara yako ikue basi toa huduma bora na kama unataka baishara yako ife na toa huduma mbovu yoyote katika baishara yako. Wateja ndio uhai wa biashara yako na lengo la biashara yako ni kupata wateja siyo kuwafukuza hivyo toa huduma bora ili uweze kuwavuta.

Hatua ya kuchukua leo. Toa huduma bora kwenye biashara yako. Toa huduma bora hata kwa familia yako, mwenza wako, toa huduma bora kwa kazi unayoifanya mpaka mteja wako ajisikie hajawahi kupatiwa huduma kama hiyo uliyompa. Kama ni watoto wapatie huduma nzuri ya malezi ambayo hawatokuja kupata sehemu nyingine yoyote kama unahisi watu wanakosa tumaini la maisha wape tumaini la maisha, kama watu wanakosa upendo basi waonyeshe upendo kwa kuishi vema falsafa ya upendo.

SOMA;     Hii Ndio Njia Bora Ya Kuwaadhibu Waliotuudhi Na Kutuumiza Katika Maisha Yetu

Mwisho, somo letu la leo limeweza kutualika sisi sote kuweza kujitafakari katika zile huduma tunazotoa kwa wateja wetu. Je ni huduma gani bora au ni mbovu unayompatia mteja wako? Nafikiri ili tuweze kukua kimaendeleo tunahitaji huduma bora kwenye kila eneo la maisha yetu yaani kiroho, kimwili na kiakili.
Kama ulikuwa bado hujajiunga na mfumo wetu wa kupokea makala kwa njia ya email list jiunge leo ili uweze kupokea vitabu mbalimbali na makala mbalimbali. Pili, kama ulikuwa bado hujalaiki ukurasa wetu wa facebook fanya hivyo leo rafiki. Pia kama ulikuwa bado hujasoma kitabu kizuri cha funga ndoa na utajiri wahi mapema kujipatia nakala yako ambayo iko katika mfumo wa nakala tete yaani soft copy tuwasiliane kwa namba hii 0717101505/0767101504 kupata kitabu hiko. Mwisho, usisahu pia kumshirikisha na mwenzako makala hii nzuri uliyosoma leo. Hakikisha na mwenzako anapata maarifa haya mazuri.

Nakutakia kila la heri katika haya uliyojifunza leo. Endelea kutembelea mtandao huu kujifunza kila siku. Asante sana.
Rafiki na mwalimu wako,
Deogratius Kessy
0717101505 /0767101504 au deokessy.dk@gmail.com

Published by Deogratius Kessy

Mwandishi,mwalimu na mjasiriamali. Unaweza kutembelea Blog yake ya www.kessydeo.home.blog kujifunza zaidi na unaweza kuwasiliana naye kwa namba 0717101505/0767101504 au kwa barua pepe deokessy.dk@gmail.com

Join the Conversation

2 Comments

Leave a comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: