Design a site like this with WordPress.com
Get started

Huyu Ndiye Mkombozi Wa Maisha Yako Atakaye Kuletea Mabadiliko Kuanzia Sasa

Habari ya wakati huu mpendwa rafiki na msomaji wa mtandao wa Kessy Deo? Natumaini unaendelea vizuri kiafya lakini pia nategemea unaendelea vizuri kuboresha maisha yako. Kila siku ni siku ya kukua katika maisha yako usikubali siku ipite bila kufanya badiliko lolote katika maisha yako. Kua kimwili, kiakili na kiroho usiache wala kudharau vitu hivi vitatu muhimu katika maisha yako. Basi mpendwa rafki, nitumie nafasi hii kukualika tena katika makala yetu ya leo tuweze kujifunza wote kwa pamoja. Karibu sana rafiki tuweze kusafiri pamoja ili niweze kukushirikisha somo letu zuri la leo.

Image result for YOUR DECISION IS YOUR SUCCESS

Mpendwa rafiki, katika somo letu la leo tutakwenda kujifunza kitu muhimu kitakachokuletea ukombozi katika maisha yako. Mpendwa, maisha yako hayawezi kubadilika hata kidogo kama hufanyi kitu kitachoweza kukuletea ukombozi kwenye maisha yako. Ukombozi wowote kwenye maisha yako unaletwa na maamuzi yako. Mkombozi wa maisha yako atakaye badilisha maisha yako kunzia leo ni maamuzi yako mwenyewe. Maamuzi yako ndio ukombozi wa maisha yako unayoishi sasa na yale unayotegemea kuyaishi hapo baadae. Maisha unayoishi sasa ni maisha ambayo yametokana na maamuzi yako mwenyewe na huna wa kumlaumu mtu, huna sababu kumlaumu mzazi wako, huna sababu za kulaumu wanasiasa au mtu yoyote Yule.

SOMA;  Mambo Saba (07) Muhimu Niliyojifunza Kutoka Kwa Donald Trump

Rafiki, katika maisha yako napenda kukuambia hivi usikubali kufanyiwa maamuzi kwenye maisha yako,utakubali kufanyiwa maamuzi na watu wengine aidha ni wazazi au ndugu lakini kumbuka siyo wazazi au ndugu watakuja kuishi maisha yako. Mara nyingi huwa unapatwa na vita mbalimbali vya nafsi vikipigana ufanye kitu gani pale unapokuwa umeruhusu kila mtu kukupa ushauri au kufanyiwa maamuzi. Haijalishi umepata ushauri au umefanyiwa maamuzi juu ya kitu Fulani katika maisha yako lakini kumbuka ya kwamba ni muhimu kusikiliza sauti yako ya ndani inataka nini na wewe ndiye mtu unayejua ndani yako kuna nini. wewe ndio unajijua zaidi kuliko watu wengine hivyo kubali kufanya maamzi ambayo unayapenda na siyo kushurutishwa na mtu.

Maamuzi ya kushurutishwa ni sawa sawa na kufanya kitu ambacho hukipendi ambacho kitakupelekea manung’uniko kwemye maisha yako. Badala ya kufurahia maisha kwa kufanya kile uanchopenda unaanza kuishi maisha ya kutokuwa na furaha na unakuwa umejiandikisha kuishi maisha ya utumwa ambayo siyo chaguo lako. Unapoamua kufanya maamuzi katika maisha yako ni vema ukawa kiziwi usimsikilize mtu na wala huhitaji kuomba ruhusa wewe fanya kile ambacho unaona kitakusaidia maisha yako. Wapo watu wengi watakuja kukuhubiria maneno ya kukukatisha tamaa, utahubiriwa kila aina ya habari hasi unaijua wewe lakini ,mambo yakiwa mazuri watakuja kukuheshimu.

SOMA;  Amka Na Fanya Mabadiliko Haya Muhimu Kwenye Maisha Yako

Ukikubali kufanyiwa maamuzi hakuna mtu atakaye kuja kuishi maisha yako wengi waliokushauri watakuwa tu wanakuangalia bila msaada wowote hivyo rafiki, unapoamua kufanya maamzi ya kubadilika jaribu kusimama imara wewe kama wewe na usishau kumwomba Mungu kwani yeye ndiye rafiki wa kweli hawezi kukuacha hata ukiwa kwenye magumu gani.
Hatua ya kuchukua leo. Maisha ni maamuzi hivyo basi,kubali kujichagulia kufanya maamuzi sahihi kwenye maisha yako. Usiwape watu nafasi kukuamulia kila kitu kwenye maisha yako na wakati unajua kabisa maamuzi ya kufanyiwa ni utumwa. Fanya kile kitu ambacho unachopenda ndio utaweza kuishi maisha ya furaha na mafanikio hapa duniani.

Kwa kuhitimisha, somo letu la leo lilitualika kuwa mkombozi wa maisha yako atakayeweza kubadilisha maisha yako leo ni maamuzi yako. Maamuzi ndiyo chanzo cha kila kitu kwenye maisha yako. Fanya maamuzi sahihi leo kwa manufaa yako mwenyewe na manufaa ya dunia nzima. Unavyoamini na kuona wewe ni tofauti na mtu mwingine hivyo amini maamuzi yako na ishi maamuzi yako.

Kama ulikuwa bado hujajiunga na mfumo wetu wa kupokea makala kwa njia ya email list jiunge leo ili uweze kupokea vitabu mbalimbali na makala mbalimbali. Pili, kama ulikuwa bado hujalaiki ukurasa wetu wa facebook fanya hivyo leo rafiki. Pia kama ulikuwa bado hujasoma kitabu kizuri cha funga ndoa na utajiri wahi mapema kujipatia nakala yako ambayo iko katika mfumo wa nakala tete yaani soft copy tuwasiliane kwa namba hii 0717101505/0767101504 kupata kitabu hiko. Mwisho, usisahu pia kumshirikisha na mwenzako makala hii nzuri uliyosoma leo. Hakikisha na mwenzako anapata maarifa haya mazuri.

Nakutakia kila la heri katika haya uliyojifunza leo. Endelea kutembelea mtandao huu kujifunza kila siku. Asante sana.
Rafiki na mwalimu wako,
Deogratius Kessy
0717101505 /0767101504 au deokessy.dk@gmail.com

Published by Deogratius Kessy

Mwandishi,mwalimu na mjasiriamali. Unaweza kutembelea Blog yake ya www.kessydeo.home.blog kujifunza zaidi na unaweza kuwasiliana naye kwa namba 0717101505/0767101504 au kwa barua pepe deokessy.dk@gmail.com

Leave a comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: