Design a site like this with WordPress.com
Get started

Fahamu Kitu Muhimu Ambacho Familia Yako Inakosa

Habari ya wakati huu mpendwa rafiki na msomaji wa mtandao wa Kessy Deo? Natumaini uko salama na umekuwa na mwisho mzuri wa juma na kama leo ndio mwisho wa juma basi ndio mwanzo mzuri wa maandalizi ya juma au wiki ya kesho. Leo ni siku nzuri ya kufanya tathimini ya wiki nzima yaani mipango na malengo uliyojiwekea imeendaje. Hivyo mpendwa rafiki napenda kukualika tena katika makala yetu ya leo tuweze kujifunza kwa pamoja. Leo nitakwenda kukushirikisha makala nzuri niliyokuandalia hivyo nakusihi ungana nami mpaka mwisho wa makala hii.

whatsapp-image-2016-09-30-at-16-29-22

BONYEZA MAANDISHI HAYA KUPATA KITABU CHA FUNGA NDOA NA UTAJIRI

Mpendwa msomaji, najua kila siku unapambana ili kuhakikisha unapata kile unachokitaka na katika hali ya kawaida huwezi kupata kitu bila kufanya kitu. Hivyo ili uweze kupata kitu ni lazima uweze kufanya kitu hii ni kama sheria ya asili kabisa katika maisha yetu ya kila siku. Leo nataka kuwakumbusha wazazi kuwa ni muhimu sana kutenga muda wako angalau hata siku za mwisho wa juma kukaa na familia yako na kuzungumza nayo ili uweze kupata mrejesho wa mambo yanavyokwenda katika familia yako. Najua watu wengi huwa wanawaacha watoto na wasaidizi wa ndazi na wakirudi nyumbani wanakosa hata muda wa kukaa na familia kujua nini kinaendelea. Licha ya kuwa na majukumu mengi na unatafuta sana lakini kama familia yako ikiwa haiko sawa hata kile unachotafuta kinakuwa hakina maana.

SOMA;   Muhimu; Kabla ya Kuanza Wiki Ya Kesho Unahitaji Kuwa Kitu Hiki Ili uweze Kufanikisha Mambo Yako

Tumia fursa ya leo kukaa na familia yako na wahoji mambo mbalimbali jua ni sehemu gani ina changamoto ili uweze kuitatua. Watoto wanapitia mapito makubwa sana wanapata majeraha ya moyo kwa kunyimwa haki zao za msingi ndani ya familia. Ndani ya familia baba ana hamsini zake na mama ana hamsini zake nyumba inakuwa haina amani wala furaha na watoto nao wanashindwa kupewa muda kuwaelezea wazazi wao yale yanayowasibu. Kaa hata na msaidizi wako wa kazi kuna mambo anayo atakuambia kama ukimpa nafasi na kumhoji vizuri. Kaa na watoto wahoji kama muda ambao haupo huku nyuma wanafanyiwa nini hoji na pata ukweli tathimini nao. Kama wiki nzima ulikosa kukaa mezani na kula na familia yako jaribu leo kufanya hivyo kaa na familia yako kuleni pamoja, ongeeni pamoja.

SOMA;   Fanya Tathimini Hii Muhimu Sana Kabla Hujaenda Kulala Leo

Hatua ya kuchukua. Weka ratiba ya kuzungumza na familia yako kila mwisho juma au kila siku kama una nafasi ya kufanya hivyo. Tenga muda wa kujenga na kuimarisha mahusiano yako na familia yako. Tenga muda wa kukaa na mwenzi wako, na watu wa karibu kwako. Kuna mambo mengi yanayotokea katika familia yako unapokuwa haupo nyumbani hivyo bila kutenga muda wa kukaa na familia huwezi kujua nini kinaendelea.

Mwisho, tunaalikwa sisi sote kutenga muda wa kukaa na familia zetu, na watu wengine wa karibu kwetu. Familia ndio msingi wa maisha hivyo usipofuatilia mwenendo wa familia yako mwisho wa siku utakuja kukuta imeenda mrama. Kinga ni bora kuliko tiba licha ya kuwa na majukumu mengi usisahu familia yako kwani yote unayofanya kama familia yako haina amani, furaha na upendo vitu unavyotafuta vinakuwa havina maana. Maisha ni mahusiano mazuri yanayotawaliwa na falsafa ya upendo.

Kama ulikuwa bado hujajiunga na mfumo wetu wa kupokea makala kwa njia ya email list jiunge leo ili uweze kupokea vitabu mbalimbali na makala mbalimbali. Pili, kama ulikuwa bado hujalaiki ukurasa wetu wa facebook fanya hivyo leo rafiki. Pia kama ulikuwa bado hujasoma kitabu kizuri cha funga ndoa na utajiri wahi mapema kujipatia nakala yako ambayo iko katika mfumo wa nakala tete yaani soft copy tuwasiliane kwa namba hii 0717101505/0767101504 kupata kitabu hiko. Mwisho, usisahu pia kumshirikisha na mwenzako makala hii nzuri uliyosoma leo. Hakikisha na mwenzako anapata maarifa haya mazuri.

Nakutakia kila la heri katika haya uliyojifunza leo. Endelea kutembelea mtandao huu kujifunza kila siku. Asante sana.
Rafiki na mwalimu wako,
Deogratius Kessy
0717101505 /0767101504 au deokessy.dk@gmail.com

Published by Deogratius Kessy

Mwandishi,mwalimu na mjasiriamali. Unaweza kutembelea Blog yake ya www.kessydeo.home.blog kujifunza zaidi na unaweza kuwasiliana naye kwa namba 0717101505/0767101504 au kwa barua pepe deokessy.dk@gmail.com

Leave a comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: