Design a site like this with WordPress.com
Get started

Mambo Muhimu Niliyojifunza Katika Kitabu Cha Secrets Of The Richest Man Who Ever Lived

Habari ya wakati huu mpendwa rafiki na msomaji wa mtandao wa Kessy Deo? Natumaini uko vizuri rafiki yangu. Hivyo basi, karibu katika makala yetu ya leo tuweze kujifunza kwa pamoja. Leo nitakushirikisha mambo muhimu niliyojifunza katika cha Secrets Of The Richest Man Who Ever lived kilichoandikwa na Mudock.
Hiki ni kitabu kilichoandikwa kwa kutumia mifano ya maisha mfalme sulemani.
Mambo 20 niliyojifunza katika kitabu cha secrects of the Richest man who ever lived ni kama ifuatavyo; karibu tujifunze;

Image result for secrets of richest man who ever lived

1. Watu wenye ndoto kubwa huwa hawaeleweki na watu.
Watu huwa hawawaelewi kabisa.
Unatakiwa usielekewe na watu. Mtu ambaye haeleweki duniani ni yule mtu ambaye anafanya mambo ambayo siyo ya kawaida. Mtu anayefanya mambo tofauti, anayekwenda mbali kuliko watu wengine,anayefanya mambo ambayo watu wengine hawafanyi.

2. Watu ambao wana ndoto kubwa duniani ndio wale ambao wanatoa ajira na wenye kipato kikubwa.
Mara nyingi watu wenye ndoto kubwa, ambao hawaeleweki ndio watu wanaoleta mapinduzi katika hii dunia. Watu ambao wanafanya hii dunia kua sehemu salama ya kuishi.
Mimi na wewe, ndio tunafanya dunia kua sehemu salama /mbaya ya kuishi.
Timiza wajibu wako ili dunia iwe mahali bora.

3. Ili kutimiza ndoto yako kwanza unapaswa kujua nini unataka. Mfano,mfalme Suleimani alijua nini anataka. Lakini pia, unatakiwa kua na shauku katika kile unachofanya.
Maumivu uliyokua nayo wakati uliopita yanaondolewa na shauku uliyonayo leo.
Kua na shauku na jua unataka nini ni moja wapo ya siri ya mafanikio ya watu wengi.

SOMA; Mambo Saba (07) Muhimu Niliyojifunza Kutoka Kwa Donald Trump

4. Ili ukamilishe ndoto yako unatakiwa kuwa na njaa ya mafanikio.
Katika hali ya kawaida njaa huwa inakusukuma na kukusumbua kwenda kutafuta chakula kilipo.
Hivyo basi, wewe kama mwanamafanikio njaa ya kutafuta ndio nishati yako kuu ya kukuwezesha wewe kutimiza malengo yako uliyojiwekea.
Kua na ndoto ya tofauti inahitaji upate watu wa kukusaidia na kukupa hamasa. Huwezi kufanya kila kitu peke yako bali unahitaji watu wakukusaidia kufanikisha ndoto yako ambayo siyo ya kawaida.

5. Linapotajwa jina la Henry Ford unapatwa na picha gani katika akili yako? Je lipotajwa jina mfalme suleimani unapatwa na picha gani? Mfalme suilemani yeye ni mtu aliyeomba hekima na akapewa vyote.
Hivyo basi, tunajifunza kua Hekima na busara ni kitu muhimu sana duniani.
Kosa vitu vyote lakini siyo kukosa hekima.
Hekima itakuletea vyote unavyotaka hapa duniani.
Tafuta kwanza hekima nayo hekima itakuletea mali,marafiki wazuri na vyote utAkavyo katika hii duniani.
Kukosa hekima ni sawa na meli kukosa nahodha baharini.

6. Siri ya tajiri ambaye hakuwahi kutokea duniani nyingine ni kujiamini.
Unatakiwa kua na uwezo wa kujiamini na kuamini kua Mungu amekupa mazuri juu yako yako.
Usiogope bali jiamini na nenda katekeleze kile ambacho unacho ndani yako.
Fanya kwa moyo wako wote ili utoe hazina uliyonayo.

7. Katika safari ya mafanikio unatakiwa kuyakubali madhaifu yako au changamoto zako.
Kukubali tatizo ndio msingi wa kwanza katika kutatua tatizo.
Hakuna aliyekamilika na mt. Thomas Aquinas aliyewahi kusema mtu aliyekamilika duniani hakuna bali Mungu pekee ndiye aliyekamilika.
Huenda hapo ulipo una maadhaifu huna budi kuyakubali na kuyafanyia ufumbuzi yakinifu.
Kutokubali udhaifu wako ni utumwa wa hali ya juu.
Hivyo basi, furahia changamoto zinazokukabili na zinazokutokea katika maisha yako.

SOMA; Mambo Muhimu Niliyojifunza Katika Kitabu Cha 10- Minutes Toughnesss

8. Ni vema watu kujua malengo yako unafanya nini hii itakufanya ujitume zaidi.
Ukiwaambia watu kua mwaka huu nitatoa kitabu basi watu watakua wanakusumbua na kukuulizia vipi umefikia wapi?
Angalizo, siyo kila jambo unapaswa kuwaambia watu. Mambo mengine yanahitaji usiri.
Hivyo basi, kuna mambo ya kumwambia mtu na kuna mambo ya binafsi ya siri unabaki nayo mwenyewe.

9. Katika safari ya mafanikio unahitaji kua na rasilimali muhimu ambayo ni watu.
Unatakiwa kuwapenda watu na kuwathamini watu kwani ndio rasilimali itakayoweza kutimiza ndoto zako.
Usiwadharau watu bali wekeza katika watu na utafaidika.

10. Unapokua mwanamafanikio unatakiwa kuwaathiri watu wanaokuzunguka yaani uwaathiri wawe kama wewe.
Kama unalima basi waamasishe watu wengine kufanya kile unachofanya.
Saidia watu wapate kile wanachokitaka na wewe utafanikiwa.

11. Kama wewe ni mwanamafanikio unatakiwa uwe na sifa ya kuwa msikilizaji bora au mzuri.
Wasikilize watu wanataka nini.
Usidharau watu wanapotaka kukuambia kitu.
Wape muda mzuri wa kuwasikiliza. Huenda ukapata kitu cha kujifunza kupitia watu hao. Hivyo basi, kusikiliza ni moja siri ya mafanikio.

12. Kama watu wamefanya vitu vizuri wapongezi hadharani au kwa kumwambia binafsi.
Kuwa na tabia ya kupongeza watu pale wanapofanya vizuri.
Epuka kumsema mtu mbele ya kadamnasi. Bali mfuate akiwa peke yake na umwambie kua ulienda vibaya.
Kumsema mtu hadharani ni fedhea kubwa. Kwani hitaji la kwanza la mwanadamu ni kuthaminiwa.
Hivyo basi,wathamini watu na wewe utathaminiwa.

13. Waandikie watu kile unachotaka kufanya badala ya kuwaambia kwa mdomo.
Kama unawafanyakazi wako pendelea kutoa maelekezo ya jinsi ya kufanya kazi fulani kwa maandishi.
Maandishi ni rahisi kwa mtu yoyote kukumbuka ukilinganisha na kuwaambia watu kwa mdomo.
Kama una maono yako,matarajio yako yaweke katika maandishi na itakusaidia sana.
Utamaduni wa kuandika na kuyaweka mambo yako katika maandishi ni mzuri sana.

14. Unatakiwa kuwa na mipango na malengo. Weka malengo na mipango yako ya siku katika maandishi.
Kuna faida nyingi za wewe kuweka kila kitu katika maandishi.
Kuweka mambo katika maandishi inakuwa inakupa picha yako ya kule unapotaka kwenda.
Ni rahisi kukumbuka na kufanya mrejesho.
Unapoandika unakua unajiwekea mkataba binafsi wa kutekeleza mambo yako.

15. Zawadi ambayo mwanadamu amepewa hapa duniani ni muda.
Muda ndio fedha katika dunia.
Unapotaka kuanzisha uhusiano na mtu huhitaji kua na fedha. Bali unahitaji kuwekeza rasilimali muda na mtu ili kuanzisha uhusiano.
Muda ni mali.
Ukitaka kuonana na mtu na kupashana habari kitu kinachoweza kuwaunganisha na kua pamoja ni muda.
Poteza fedha lakini usipoteze muda wako.

SOMA;   Hii Ndio Zawadi Ya Kipekee Sana Uliyopewa Kutoka Kwa Mungu

16. Unapowaahidi watu katika muda unatakiwa kuwa mwaminifu.
Kuwa mwaminifu katika muda. Ukiahidi watu utafika saa mbili fanya hivyo na kama ukichelewa kufanya hivyo waombe watu samahani.
Heshimu muda wa mtu na atakuheshimu. Ukimpotezea mtu muda huwezi kumlipa thamani ya muda wake.

17. Kumbuka kufanya mapatano ya kitu fulani.
Kukubaliana na mwenzako,mwajiri,waajiri wako juu ya kitu fulani.
Usifanye jambo bila makubaliano na mtu.
Kukubaliana ni taarifa zenye nguvu.
Na katika makubaliano yenu kumbuka kusikiliza ndio silaha kubwa sana katika kufikia muafaka.

18. Katika kufanya maamuzi unatakiwa usifanye maamuzi ukiwa umechoka.
Pata muda mzuri wa kupumzika na akili yako itakua huru kufanya maamuzi.
Fanya makubaliano kwa muda mrefu ili kupata matokeo mazuri.
Epuka kufanya makubaliano yoyote juu kwani itakugharimu baadae.

19. Unapotaka kutoa hukumu au kusuluhisha jambo angalia pande zote za shilingi.
Sikiliza pande zote mbili kwanza wanasemaje.
Baada ya kusikiliza pande zote mbili itakusaidia sana kufanya maamuzi. Utaweza kuchunguza kiini cha tatizo.
Matokeo mazuri ya maamuzi yako unayapata katika kusikiliza.

20. Unapaswa kukumbuka migogoro mbalimbali haikosekani kwa watu. Kuna watu wana mitazamo tofauti. Unatakiwa kuwajua vizuri watu.
Usipowaelewa utapata shida.
Waamini watu lakini wachunguze pia.

Nakutakia kila la heri katika haya uliyojifunza leo. Tafadhali washirikishe na wengine maarifa haya mazuri.
Rafiki na Mwalimu wako,
Deogratius Kessy
0717101505/0767101504
deokessy.dk@gmail.com

Published by Deogratius Kessy

Mwandishi,mwalimu na mjasiriamali. Unaweza kutembelea Blog yake ya www.kessydeo.home.blog kujifunza zaidi na unaweza kuwasiliana naye kwa namba 0717101505/0767101504 au kwa barua pepe deokessy.dk@gmail.com

Leave a comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: