Design a site like this with WordPress.com
Get started

Hii Ndio Zawadi Ya Kipekee Sana Uliyopewa Kutoka Kwa Mungu

Habari ya wakati huu mpendwa rafiki na msomaji wa mtandao wa Kessy Deo? Ni matumaini yangu uko salama na umeianza siku yako kwa ushindi. Rafik, tunamshukuru Mungu kwa zawadi ya siku hii ya leo hivyo tuitendee haki siku hii ya leo kwa kufanya mambo chanya kwa manufaa yako mwenyewe na manufaa ya dunia nzima. Napenda kukualika katika makala yetu ya leo tuweze kujifunza hivyo karibu sana rafiki tuweze kujifunza kwa pamoja mada nzuri niliyokuandalia siku hii ya leo.

Image result for parents is the gift from God

Mpendwa rafiki, leo tutakwenda kujifunza zawadi ya kipekee kutoka kwa Mungu iliyoweza kutuleta hapa duniani. Je ni zawadi gani hiyo? Nakusihi sana ungana nami mapaka mwisho wa makala hii ili uweze kujifunza mazuri niliyokuandalia leo. Rafiki, zawadi ya kipekee kutoka kwa Mungu tuliyoipata bila kuchagua ni wazazi. Wazazi ni zawadi kutoka kwa Mungu. Hakuna aliyechangua mzazi wala kuandika barua azaliwe na mzazi Fulani. Bali wote tunajikuta tumeshazaliwa na wazazi ambao tuna leo. Unatakiwa kuheshimu mzazi wako hata kama ana mapungufu kwani huwezi kumbadilisha ni mzazi wako tu.

SOMA;  Hizi Ndizo Sehemu Nne (4) Muhimu Za Kuchota Baraka Katika Maisha Yako

Baadhi ya watu wanawadharau wazazi wao na kuwaambia hata maneno ya kejeli na fedhea kama vile ungechelewa kidogo hata mimi ningekuzaa, wewe si mzazi wangu, wengine wanawakataa wazazi wao kutokana na maadhifu waliyokuwa nayo wazazi wao. Kuna wengine wazazi wao wanapata shida na wao wana nafasi nzuri ya kuwasaidia lakini wanashindwa kutokana na roho ya ubinafsi. Hata kama mzazi wako mmoja alikutendea vibaya, alikukataa na wewe hupaswi kumkataa atabaki kuwa mzazi wako tu. Unapaswa kulipa wema kwa ubaya na siyo ubaya kwa kubaya. Wengine wanatumia mpaka majina ya wazazi wao halafu wanashindwa kuwasaidia na kukataa sio wazazi wao je kama siyo mzazi wako mbona unatumia jina lake? Tafadhli naomba jiulize swali hili wewe unamchukia mzazi wako mmoja aidha unamchukia baba au mama, bila kuunganika kwa baba na mama wewe ungepatikana? ni swali tu la kawaida sasa je kwanini unachukia baba/mama wakati wote wameshiriki katika kuzaliwa kwako? Mama yako angewezaje kukuzaa bila muunganiko na baba yako? Wazazi wote ni sawa na kila mmoja anastahili heshima yake licha ya kuwa na udhaifu wake.

SOMA TENA;  Kiungo Hatari Cha Mwanadamu Kinachoongoza Kuuwa Watu Katika Jamii Zetu

Hatua ya kuchukua leo, kama ulikuwa una ugomvi na wazazi wako inuka leo nenda karudishe uhusiano ulivunjika na rudisha uhusiano wa awali. Msamaha ndio njia pekee ya kurudisha uhusiano wa awali na kuwa na falsafa ya ufagio kwa wazazi wako na siyo majivuno. Wasaidie na jitoe kwa moyo kuwasaidia wazazi wako ili ujichotee Baraka hapa duniani. Wapende na waheshimu wazazi wako licha ya kuwa na madhaifu yao. Waombee kwa Mungu hayo madhaifu yao na siyo kuwakataa.

Kwahiyo, wazazi ni zawadi kutoka kwa Mungu kama somo letu la leo lilivyotualika sisi sote kuwaheshimu na kuwapenda wazazi wetu kwani hakuna hata mtu mmoja aliyeandika barua ya kuzaliwa au kumchagua mzazi Fulani. Wazazi ndio msingi wa maisha yetu hapa duniani tunapaswa kuwasaidia na kuwajali kwa moyo kipindi wako hai na siyo kujitoa kwa mzazi kipindi cha msiba wakati amefariki jitoe kwa kumsaidia kwa wakati mzazi wako utabarikiwa kwani wazazi wamepewa mamlaka ya kubariki na kulaani.

Kama ulikuwa bado hujajiunga na mfumo wetu wa kupokea makala kwa njia ya email list jiunge leo ili uweze kupokea vitabu mbalimbali na makala mbalimbali. Pili, kama ulikuwa bado hujalaiki ukurasa wetu wa facebook fanya hivyo leo rafiki. Pia kama ulikuwa bado hujasoma kitabu kizuri cha funga ndoa na utajiri wahi mapema kujipatia nakala yako ambayo iko katika mfumo wa nakala tete yaani soft copy tuwasiliane kwa namba hii 0717101505/0767101504 kupata kitabu hiko. Mwisho, usisahu pia kumshirikisha na mwenzako makala hii nzuri uliyosoma leo. Hakikisha na mwenzako anapata maarifa haya mazuri.

Nakutakia kila la heri katika haya uliyojifunza leo. Endelea kutembelea mtandao huu kujifunza kila siku. Asante sana.
Rafiki na mwalimu wako,
Deogratius Kessy
0717101505 /0767101504 au deokessy.dk@gmail.com

Published by Deogratius Kessy

Mwandishi,mwalimu na mjasiriamali. Unaweza kutembelea Blog yake ya www.kessydeo.home.blog kujifunza zaidi na unaweza kuwasiliana naye kwa namba 0717101505/0767101504 au kwa barua pepe deokessy.dk@gmail.com

Join the Conversation

1 Comment

Leave a comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: