Design a site like this with WordPress.com
Get started

Njia Nzuri Ya Kumjibu Mtu Hasi Anayekukera Na Kukusumbua Katika Maisha Yako

Habari ya wakati huu mpendwa rafiki na msomaji wa mtandao wa Kessy Deo? Ni matumanini yangu uko vizuri rafiki na hongera tena kwa zawadi ya siku hii ya leo nakusihi rafiki itumie vizuri siku yako ya leo kwa kuzalisha mambo chanya na siyo hasi. Napenda kutumia nafasi hii tena kukualika mpendwa msomaji wa mtandao huu katika makala yetu ya leo ili tuweze kujifunza kwa pamoja makala nzuri niliyokuandalia leo.

Image result for to be silence is best way to answer ignorance people

Katika makala yetu ya leo tutakwenda kujifunza mbinu nzuri ya kumjibu mtu hasi anayekukera na kukusumbua. Hivyo basi, karibu mpendwa msomaji ili tuweze kujifunza kwa pamoja mwanzo wa makala hii mpaka mwisho ili uweze kujifunza makala nzuri ninilyokuandalia siku hii ya leo. Kila mtu anakutana na watu mwenye mtazamo hasi katika maeneo tofauti tofauti ni kweli kwamaba watu wenye mtazamo hasi huwa ni watu wasumbufu na wanaokera sana. wapo watu wanaosumbuliwa na watu hasi katika maisha yao nao wanaendelea kupambana nao kwa kurushiana maneno wakati kuna njia nzuri ya kuwajibu watu hasi wanaokusumbua na kukukera.

SOMA;   Hawa Ndio Watu Wenye Sifa Bora Za Kuwa Walimu Katika Jamii Zetu

Rafiki, njia nzuri ya kumjibu mtu hasi anayekusumbua na kukukera ni kumpuuza yaani ‘’unamwiignore’’ akiendelea kukusumbua kwa kukutumia jumbe mbaya kwenye simu, mitandao ya kijamii jibu unalotakiwa kumjibu ni kumpuuza na kukaa kimya na endelea na maisha yako mengine. Kwanini ujitese kisaikolojia kwa watu hasi wanaokusumbua mpaka kukunyima furaha wakati kuna njia nzuri ya kuwajibu? Mtu akikutukana njia nzuri ya kumjibu ni kukaa kimya na kumpuuza ukikaa kimya yeye ndio atajiona mjinga lakini ukimjibu wote mtaonekana wajinga. Kwa mfano, wakina dada huwa wanasumbuliwa sana na watu kama hawa kwa kutumiwa jumbe mbalimbali katika simu au mitandoa ya kijamii hivyo wewe usipate shinda kupambana na watu kama hawa akituma jumbe yoyote usijibu,akipiga usipokee na nk njia nzuri kabisa ya kujiepusha kutojichosha kiakili na mtu mwenye mtazamo hasi.

SOMA;   Kiungo Hatari Cha Mwanadamu Kinachoongoza Kuuwa Watu Katika Jamii Zetu

Wengine wale watu wa wrong namba wanabuni namba mbalimbali na wakikuta ni ya msichana basi anaanza kumsumbua msichana huyo. Matatizo haya kama ya wrong namba usihangaike nayo kabisa kuwajibu watu wa namna hii kwani ukiendelea kuwajibu watu hawa itapelekea hata kuharibu au kuvunja mahusiano yako na mtu wako wa karibu. Wakati mwingine unaweza kufanya jambo lako zuri katika jamii yako lakini wako watu ambao watakuja kuwapinga na kuwakosoa sasa wewe usikatishwe tamaa na watu hawaa bali kuwa tu kiziwi usisikilize keleleze zao na wewe endelea kuweka juhudi katika kile unachofanya katika maisha yako.

SOMA;   Huu Ndio Umuhimu Wa Kujenga Mahusaino Bora Katika Maisha Yetu
Hatua ya kuchukua leo, acha kujibu jumbe, au maoni hasi yoyote kuanzia sasa katika maisha yako. Chagua kujibu jumbe chanya tu na ukikutana na watu hasi au jumbe hasi njia nzuri ni kutokujibu kwa kupuuza na kukaa kimya. Mtu akikutukana wewe kaa kimya wala usihangaike kumjibu. Futa urafiki kwa wale watu ambao ni hasi na hawaendani na falsafa ya maisha yako.

Kwahiyo, somo letu la leo lilitualika kujua njia nzuri ya kuwajibu watu hasi katika maisha yetu ya kila siku ni kuwapuuza na siyo kurushiana makombora ya maneno. Watu hasi wametamalaki kila kona ya maisha yetu hivyo yakupasa kuwa makini na watu hawa. Wapuuze watu hasi ili maisha yako yaende mbele muda wetu ni mchache sana kuanza kujibizana na watu hasi katika maisha yetu.

Kama ulikuwa bado hujajiunga na mfumo wetu wa kupokea makala kwa njia ya email list jiunge leo ili uweze kupokea vitabu mbalimbali na makala mbalimbali. Pili, kama ulikuwa bado hujalaiki ukurasa wetu wa facebook fanya hivyo leo rafiki. Pia kama ulikuwa bado hujasoma kitabu kizuri cha funga ndoa na utajiri wahi mapema kujipatia nakala yako ambayo iko katika mfumo wa nakala tete yaani soft copy tuwasiliane kwa namba hii 0717101505/0767101504 kupata kitabu hiko. Mwisho, usisahu pia kumshirikisha na mwenzako makala hii nzuri uliyosoma leo. Hakikisha na mwenzako anapata maarifa haya mazuri.

Nakutakia kila la heri katika haya uliyojifunza leo. Endelea kutembelea mtandao huu kujifunza kila siku. Asante sana.
Rafiki na mwalimu wako,
Deogratius Kessy
0717101505 /0767101504 au deokessy.dk@gmail.com

Published by Deogratius Kessy

Mwandishi,mwalimu na mjasiriamali. Unaweza kutembelea Blog yake ya www.kessydeo.home.blog kujifunza zaidi na unaweza kuwasiliana naye kwa namba 0717101505/0767101504 au kwa barua pepe deokessy.dk@gmail.com

Leave a comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: