Design a site like this with WordPress.com
Get started

Hili Ndilo Deni Unalodaiwa Na Dunia Unalopaswa Kulilipa Kabla Ya Kwenda Kaburini

Habari ya wakati huu mpendwa rafiki na msomaji wa mtandao wa Kessy Deo? Ni matumaini yangu hujambo na unaendelea vizuri rafiki yangu. Hongera kwa zawadi ya siku hii ya leo katika maisha yako itumie vizuri kuifanya dunia kuwa sehemu salama ya kuishi mimi na wewe. Aidha, natuamini umeanza siku yako kwa hamasa na ushindi mzuri. Mpendwa msomaji, napenda kukualika tena katika somo letu la leo ili tuweze kujifunza kwa pamoja. Nakusihi rafiki twende pamoja mpaka mwisho wa somo letu la leo ili tuweze kujifunza kupitia makala nzuri niliyokuandalia siku hii ya leo rafiki na msomaji wa mtandao wa Kessy Deo.

Image result for TALENT

Katika makala yetu ya leo tutajifunza deni unalodaiwa na dunia ambalo unapaswa kulilipa kabla ya kwenda kaburini. Je ni deni gani? Karibu rafiki nikushirikishe na tujifunze somo zuri la leo. Hivi rafiki, ulishawahi kujiuliza nani atalia wakati wewe umekufa? Mwandishi na mhamasishaji Robin Sharma ameandika kitabu chake kinachoitwa who will cry when you die? Akiwa na maana ya kwamba nani atalia wakati umekufa? Rafiki kaa chini katika sehemu tulivu na vuta picha ya siku yako ya mwisho na jiulize swali hili hapo ndipo utagundua kama unadaiwa na dunia au la. Rafiki,usiogope kusikia kifo kwani hakikwepeki na mtakatifu Agustino aliwahi kusema, kifo ni rafiki yetu ambaye tunaishi naye majumbani mwetu na kutembea naye. Hivyo basi, usiogope hakikisha unajiandaa vema kiroho na kuondoa mtupu ukiwa hudaiwi kitu na dunia.

SOMA;   Jambo Linalosubiriwa Kwa Hamu Na Watu Wengi Litokee Katika Maisha Yao

Rafiki, najua una kitu cha kipekee ambacho hakuna mtu mwingine anacho hapa duniani kwa mfano, hata kama wewe ni mchezaji mpira kila mtu ana namba yake na nafasi yake ndani ya uwanja ndio maana mko kumi na moja. Hakuna mtu anayeweza kuziba pengo lako zaidi ya wewe mwenyewe hata akitokea utasikia huyu anacheza mpira kama mtu Fulani lakini siyo ni kama hivyo nafasi yako ni kubwa sana sehemu yoyote uliyopo kuwa sehemu ya mabadiliko unayotaka kuyaona hapa duniani kama alivyowahi kusema mahatma gandhi.

Mpenzi msomaji, leo nataka kukukumbusha juu ya utumiaji wa talanta au vipaji ulivyopewa na Mungu bure kabisa ili kuisaidia dunia na wewe mwenyewe pia. Ni namna gani unatumia vipawa au talanta ulizopewa? Mpaka leo bado unatumia talanta yako peke yako kujinufaisha mwenyewe? Kama unafanya hivyo unakwenda kinyume na falsafa ya upendo na kanuni ya dhahabu. Je unatumia kipawa chako kwa manufaa yako na dunia nzima? Napenda kukusihi rafiki yangu kuwa kama ulikuwa hujatumia kipawa chako anza kukitumia leo chochote unachojua hapa dunia juu ya kipaji chako washirikishe na wenzako ili waweze kujua kwa kufanya hivyo ndio unakua unalipa deni unalodaiwa na dunia. Hivyo tumia kipaji chako ulichopewa na Mungu kuwa msaada kwako na kwa dunia nzima.

SOMA;  Hitaji Muhimu Ambalo Dunia Ya Leo inahitaji Kwa Wingi

Hatua ya kuchukua leo. Rafiki, una hazina ndani yako ambayo bado hujaigundua hivyo gundua kipaji chako na kuanzia sasa anza kutumia kipaji chako ulichopewa na Mungu bure kuwasaidia wengine. Usikae bure na kulalamika bali tumia muda wako kuifanya dunia kuwa sehemu bora ya kuishi kwa kila mmoja wetu.

Mwisho, somo letu la leo limetualika sisi sote kutumia vipawa vyetu tulivyopewa na Mungu. tunaalikwa kutumia vipawa vyetu vizuri hapa duniani kabla hatujaondoka duniani. Usikubali kufa na kipaji chako bali lipa deni kwa kushirikisha kipaji chako dunia. Wewe ni zawadi kwa wewe mwenyewe na wewe ni zawadi kwa dunia.
Kama ulikuwa bado hujajiunga na mfumo wetu wa kupokea makala kwa njia ya email list jiunge leo ili uweze kupokea vitabu mbalimbali na makala mbalimbali. Pili, kama ulikuwa bado hujalaiki ukurasa wetu wa facebook fanya hivyo leo rafiki. Pia kama ulikuwa bado hujasoma kitabu kizuri cha funga ndoa na utajiri wahi mapema kujipatia nakala yako ambayo iko katika mfumo wa nakala tete yaani soft copy tuwasiliane kwa namba hii 0717101505/0767101504 kupata kitabu hiko. Mwisho, usisahu pia kumshirikisha na mwenzako makala hii nzuri uliyosoma leo. Hakikisha na mwenzako anapata maarifa haya mazuri.

Nakutakia kila la heri katika haya uliyojifunza leo. Endelea kutembelea mtandao huu kujifunza kila siku. Asante sana.
Rafiki na mwalimu wako,
Deogratius Kessy
0717101505 /0767101504 au deokessy.dk@gmail.com

Published by Deogratius Kessy

Mwandishi,mwalimu na mjasiriamali. Unaweza kutembelea Blog yake ya www.kessydeo.home.blog kujifunza zaidi na unaweza kuwasiliana naye kwa namba 0717101505/0767101504 au kwa barua pepe deokessy.dk@gmail.com

Leave a comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: