Design a site like this with WordPress.com
Get started

Mambo Muhimu Ya Kuepuka Ili Yasikuharibie Siku Yako Ya Leo

Habari ya wakati huu mpendwa rafiki na msomaji wa mtandao wa Kessy Deo? Ni matumaini yangu hujambo na unaendelea vizuri pia. Ni jambo la kumshukuru Mungu kwa zawadi ya siku hii ya leo hivyo basi, tunaalikwa kutumia vizuri muda wetu wa leo kuzalisha mambo chanya na siyo hasi. Rafiki, karibu tena katika makala yetu ya leo tuweze kujifunza kwa pamoja na leo nimekuandalia somo zuri tutakalo kwenda kujifunza wote kwa pamoja hivyo nakusihi tuende pamoja mpaka mwisho wa makala hii.

Image result for people who talking themselves about issue

Katika somo letu la leo tutajifunza mambo ya kuyaepuka ili yasikuaribie siku yako. Je una unajua ni jambo gani? Karibu tuweze kujifunza rafiki, katika sehemu nyingi ambazo watu wanafanya kazi wanakutana na mambo mengi ambayo yanaweza kuwaharibia siku kabisa. Leo nitakushirikisha jambo moja la kuepuka katika sehemu yoyote ile uliyopo nalo ni kubishana. Kubishana imekuwa ni desturi ya watu wengi hususani maeneo ya kazi ambapo watu wamekusanyika au vikundi mbalimbali vilivyokutana kwa ajili ya jambo Fulani. Baadhi ya mada wanazokua wanabishania ni kama vile siasa, michezo yaani mipira, dini na mambo yanayotokea katika jamii.

SOMA; Jambo Linalosubiriwa Kwa Hamu Na Watu Wengi Litokee Katika Maisha Yao

Kubishana huku kuna pelekea madhara mengi sana katika utendaji wa kazi na hatimaye ufanissi wa kazi unapungua kabisa kutokana na kubishana. Kubishana inawafanya watu kukosa umakini wa kazi zao na kufanya kazi zao kwa kiwango cha chini. Kubishana kunapelekea upotezaji wa muda kwa watu wengi kwa mfano, badala ya watu wafanye kazi na kuwajibika katika wajibu wao wanaanza kubishana na kusahau wajibu wao wa kazi ni upi. Muda mwingi watu wanautumia katika kubishania mambo badala ya kufanya kazi.

Madhara mengine ya kubishana ni huleta ugomvi. Baada ya watu kubishana na upande mmoja kushindwa ugomvi unaanza kutokea kwani unakuta watu wengi wakiwa katika mabishano huwa wanaongozwa na hisia hivyo ni rahisi kupatwa na hasira na matokeo yake mtu anafanya maamuzi ya hasira na baadae inakuja kumgharibu. Hivyo kubishana ni dalili ya mtu mwenye mtazamo hasi kama wewe ni mtu makini na una mambo yako ya kufanya huwezi kukaa na kubishania siasa, mipira nakadhalika.

SOMA TENA; Muhimu; Kabla ya Kuanza Wiki Ya Kesho Unahitaji Kuwa Kitu Hiki Ili uweze Kufanikisha Mambo Yako

Hatua ya kuchukua leo. Epuka kubishana kuanzia leo juu ya jambo lolote lile katika maisha yako. Kabla ya kuanza kubishana rejea katika taratibu za kazi sehemu uliyopo au katika malengo yako na ratiba ulizojiwekea siku husika je kuna utaribu unaoruhusu kubishana? Au katika malengo yako ulijiwekea kubishana ni moja ya vipaumbele vyako? Au kabla hujaanza kubishana jiulize kwanza umemaliza kazi au majukumu yako? Wewe kama ni mtu makini na mtu chanya epuka kubishana na mtu. Kubishana ni ujinga kwani kila mtu anakua anaangalia upande wake na kila mtu anataka ashinde kwa kile anachokiamini na hatimaye mshindi hapatikani.

Kwa kuhitimisha, mabishano hayana maana katika maisha yetu hivyo tunaalikwa wote kuepuka mabishano katika maisha yetu. Mabishano huleta migogoro mingi sehemu za kazi na katika jamii zetu. Mabishano ni ishara ya mtu hasi na huwezi kupata mabadiliko katika maisha yako kupitia kubishana au kulalamika bali kwa kufanya kazi ndio unaweza kuleta mabadiliko katika maisha yako na kufanya dunia kuwa sehemu salama kuishi kwa kila mmoja wetu.

Nakutakia kila la heri katika haya uliyojifunza leo. Endelea kutembelea mtandao huu kujifunza kila siku na washirikishe na wenzako maarifa haya. Asante sana.
Rafiki na mwalimu wako,
Deogratius Kessy
0717101505 /0767101504 au deokessy.dk@gmail.com

Published by Deogratius Kessy

Mwandishi,mwalimu na mjasiriamali. Unaweza kutembelea Blog yake ya www.kessydeo.home.blog kujifunza zaidi na unaweza kuwasiliana naye kwa namba 0717101505/0767101504 au kwa barua pepe deokessy.dk@gmail.com

Join the Conversation

1 Comment

Leave a comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: